Vigogo wa Chama cha Walimu (CWT) waburuzwa Mahakamani Kisutu kwa ufisadi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
991
1,000
VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
 
Shapu

JF-Expert Member
Jan 17, 2008
2,103
2,000
Duu yaani kwa sasa nimeshindwa kuelewa sasa hawa TAKUKURU wanatakiwa ku deal na nini. Kwa hiyo hata kama nimempa mama watoto hela ya matumizi ya chakula cha familia akaamua kuichepusha na kwenda kusukia wigi namripoti TAKUKURU then wanamfikisha mahakamani fasta.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
12,375
2,000
Kila siku nasema CWT ni janga kubwa sanaaa, na kama ni aina ya ugonjwa basi ile CANCER ya moyo.

Halafu hicho kiwango cha billion13 nadhani kuna typing error, watakua wameacha sifuri moja.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,481
2,000
Wapuuzi wakubwa hai! Badala ya kupigania haki za wanachama, wao wanawaza kupiga tu!

Nitashangaa sana iwapo hawatakula mvua za kutosha gerezani, ili iwe funzo kwa wapigaji wengine.
 
Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,746
2,000
Hii ina maana kuwa wote wawili walidanganya wakajilipia hizo fedha na kwenda kuangalia mchezo wa mpira na siyo malipo ya kazi inayohusu CWT?.
 
mtolewa

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
538
500
Kila siku nasema CWT ni janga kubwa sanaaa, na kama ni aina ya ugonjwa basi ile CANCER ya moyo

Halafu hicho kiwango cha billion13 nadhani kuna typing error, watakua wameacha sifuri moja
Janga na kansa nchi hii Ni CCM . Siku ikipata dawa na magonjwa mengine yote nyemelezi yatapona. CCM Ni chama Cha magaidi
 
Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
804
1,000
Jiulize kwa nini wakati wa CORONA shule zilifungwa mikutano kadha wa kadhaa ilizuiliwa isifanyike na ikawekwa masharti ya kujikinga. Ila CWT walikusanyika kiwilaya hadi kitaifa na ukapigwa mkutano mkuu chini ya ulinzi mkali hadi jamaa wa kitengo walikuwamo.
Kama sio kufaidika na rasilimali za CWT basi serikali ya CCM inanufaika na CWT inavyoendeshwa. Hapa ni ngumu hao jamaa kuonekana GUILTY na hata ikiwa kulipa faini wataipangua mapema mnoo hii kesi.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,302
2,000
CWT imeanza kuliwa siku nyingi sana toka enzi za Margareth Sitta akiwa Mwenyekiti wao na Marehemu mmoja Hivi kada wa ccm akiwa katibu wao mkuu!! Cwt ni pango la wezi.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,022
2,000
VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Hiyo Tsh 13 Milion ni peanut tu, tuambieni Dr Kigwangala anafikishwa lini Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Tsh 170 Milion.

Other wise TAKUKURU itaendelea kuwa ni Taasisi ya Kupambana na RUSHWA za Wanyonge (TAKURUWA)
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,794
2,000
VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Hawa ndo wale wanaowaletea walimu matisheti ya yanga na TLP
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,727

TaKukuru niwakumbushe cha kuongezea na kwa kusaidia watumishi anbao ni walimu wetu, kuna magari used zaidi ya 210 yaliagizwa na kuingizwa nchini kutolea Japan,ili kutumiwa na makatibu wa cwt nchi nzima. Fuatilieni yalikuwa na ufisadi uliotukuka. Kuanzia kuagizwa kwake hadi ununuzi wake.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
56,293
2,000
Kila siku nasema CWT ni janga kubwa sanaaa, na kama ni aina ya ugonjwa basi ile CANCER ya moyo

Halafu hicho kiwango cha billion13 nadhani kuna typing error, watakua wameacha sifuri moja
Walitumia zaidi ya mln 13
Au nimesoma vibaya hapo

Ova
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom