Vigogo wa ccm wahusishwa na wizi wa madini ya bauxite na uharibifu wa mazingira same | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wa ccm wahusishwa na wizi wa madini ya bauxite na uharibifu wa mazingira same

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by simon james, Jun 21, 2012.

 1. s

  simon james JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa muda mrefu wananchi wa Same wamekuwa wakilalamika wizi na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wawekezaji wanao chimba bauxite kijiji cha Marieni kata ya Chome wilaya ya Same bila kupata majibu. Leo kupitia Gazeti la Raia mwema toleo la 244 juni 20 - 26 Wizi huu umeanikwa wazi huku ikionyesha kuwa Mwekezaji anailipa Halmashauri ya wilaya ya Same T Sh 1,000/= kwa tani moja huku yeye akisafirisha tanikwa tani kupeleka Kenya akiuza tani moja kwa dola $2500/= Licha ya serikali kujidai inalinda mazingira kwa kuwafukuza wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao walikuwa wanafanya uchimbaji maeneo hayo ya msitu kwa upande mwingine serikali wamekuwa wakimlinda mwekezaji huyo ambaye inasemekana aliuziwa mkataba na mtu anayejulikana kama Abdullah Seleman ambaye ni diwani CCM Kata ya Makanya. Ambaye aliuza mgodi mwaka 2009 kwa thamani ya sh Milion 500 kwa mwekezaji toka Arusha. Hata hivyo mwandishi wa habari hii alipo mpigia simu mwekezaji huyo alisema , nanukuu "swala hili hata waziri mkuu, Mizengo Pinda analifaham na usinipopezee muda wangu" source Raia mwema toleo Na 244 Juni 20- 26 page 12, 13. Tujiulize kuwa ni kwanini uharibifu wa mazingira ufanywe wakati viongozi wa serikali chini ya Mkurugenzi wakiwa kimya? Na ni kwanini mwekezaji awe na kiburi cha kumtaja Pinda? Na kweli Mbunge wa Same magharibi (CCM)hajui wizi huu au na yeye ni mwana hisa?
   
Loading...