Vigogo wa Benki Kuu wanyang'anywa mabenzi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,399
2,000
Date::12/3/2008
Vigogo wa Benki Kuu wanyang'anywa mabenzi

WAKATI uchunguzi wa ufisadi katika ujenzi wa majengo pacha (Twin Towers) ukifanyika, Gavana wa Benki Kuu (BoT) amezuia matumizi ya magari manne ya kifahari aina ya Mercedese Benz yaliyokuwa yakitumiwa na baadhi ya wakurugenzi na gavana huko nyuma.

Hatua ya kuzuia mabenzi hayo ambayo yanagharimu takriban Sh1 bilioni, imekuja wakati BoT katika siku za karibuni imekumbwa na tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Duru za uchunguzi kutoka ndani ya BoT ambazo zimethibitishwa na Gavana Profesa Benno Ndulu, zinaonyesha magari hayo ya kifahari kwa sasa yapo katika yadi ya benki hiyo kwa ajili ya matumizi maalumu.

Hivi sasa wakurugenzi wa BoT pamoja na Gavana Ndulu wanatumia gari aina ya Toyota Land Cruiser VX ili kubana matumizi.

Kwa mujibu duru hizo za uchunguzi wa Mwananchi, mabenzi hayo yalikuwa yakitumika zaidi na vigogo wa BoT wakiongozwa na aliyekuwa Gavana marehemu Daud Ballali.

Gazeti hili limebaini zaidi kwamba, marehemu Ballali alikuwa akibadili matumizi ya mabenzi kila mara pamoja na vigogo wengine.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, taarifa za kitaalamu zinasema VX inaingizwa nchini kwa thamani ya Sh100 milioni huku Mercedese Benz ikigharimu takriban Sh250 milioni.

Uchunguzi umebaini pia kuwa gharama za matumizi ya benzi kwa mafuta ni kubwa karibu mara mbili ikilinganishwa na gari aina ya Vx.

Wakati Benzi ikitumia lita moja kwa kati ya kilomita sita hadi saba, Vx hutumia lita moja kwa kati ya kilomita 6 hadi tisa, wakati gharama za vipuri vyake, kwa mfano taa ya nyuma ya benzi ni Sh 1 milioni wakati Vx ni Sh 400,000 hadi 500,00, ikiwa ni mara mbili ya benzi.

Uchunguzi huo wa kitalaamu unaonyesha kwamba wakati benzi hufanyiwa matengenezo (Service) makubwa kwa kila kilomita 10,000, Vx linahitaji matengenezo hayo baada ya kutembelea umbali wa kilomita 5,000.

Katika matengenezo hayo benzi linagharimu kati ya Sh3 hadi 4.5 milioni na Vx kati ya Sh1.5 hadi Sh 2 milioni kwa viwango vya matengenezo ya serikali.

Katika uchunguzi huo, imethibitika kwamba baada ya Profesa Ndulu kuingia madarakani Januari 9, mwaka huu, alizuia matumizi yasiyo ya ya lazima ya magari hayo kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Imethibitika pia kuwa Profesa Ndulu ambaye amekuwa akiisafisha BoT, mara nyingi amekuwa akitumia gari aina ya Toyota Landcruiser Vx na kwamba huku siku moja moja ndipo hutumia benz tena katika matukio maalum hasa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa duru hizo za habari za uchunguzi za Mwananchi Jumapili, gavana baada ya kuingia na kukuta benki ikinuka ufisadi wa aina mbalimbali, alianza kuisafisha ikiwa ni pamoja na kubana matumizi.

Alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Ndulu alikiri kuzuia matumizi ya magari hayo pasipo na sababu za msingi.

"Ni kweli yapo mabenzi manne, yamekaa nilichozuia ni matumizi yasiyokuwa na msingi kwa magari hayo," alisema gavana Profesa Ndulu.

Hata hivyo, gavana Ndulu alisema magari hayo hutumika wakati wa wageni wa BoT wa kimataifa wanaokuja kwa mwaliko maalumu wa benki hiyo kama vile Shirika la Fedha la Duniani (IMF) au Benki ya Dunia (WB).

Gavana Ndulu alisema wakati mwingine kunapokuwa na matumizi ya msingi ndipo magari hayo hutumika.

Tangu kuingia gavana Ndulu BoT imekuwa katika mabadiliko ya kutaka kuirejesha heshima na imani yake kwa wananchi, ambayo ilitoweka kutokana na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya.

Ukiacha EPA, kashfa nyingine ni ya matumizi ya zaidi ya Sh500 bilioni kwa ujenzi wa majengo pacha ya ghorofa 18 na ajira tata za watoto 16 wa vigogo.

Hata hivyo, hadi sasa tayari suala la EPA linashughulikiwa na maafisa wa BoT wanaodaiwa kuhusika katika sakata hilo walipandishwa kizimbani.

Suala lingine lilikuwa ajira tata za watoto wa vigogo ambali lishachunguzwa na kumalizwa, huku ukaguzi majengo pacha ukiendelea kufanywa na Kampuni ya wazalendo.

Magari hayo ya kifahari ambayo yalinunuliwa BoT ni sehemu ya magari 40,000 ya serikali, ambayo miongoni mwao 15 ni kati ya Vx na GX ambayo yanapaswa kupunguzwa.

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
615
0
wow, kubana matumizi na kuamua kutumia VX!! duh, haya kama hayo ndio ya kujifunga mkanda basi nadhani sisi wa vi-corrola ndio tulie tena.... maswali swali kichwani mwangu sasa ni,
1. Je ina maana hakuna gari muafaka la kutumiwa na hao wakurugenzi?
2. je, wana safari za mikoani ambazo labda zinahitaji magari hayo ya VX?
3. je hizo benzi zilikuwa 4x4 au ni saloon? kama ni saloon, je kwa nini hawakuagiza magari saloon ambayo ni chipa to run?

ngoja nikapumzike manake sijui tuendapo ni wapi!
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067

Watumie Mark II
 
Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Waandishi uchwara washashikishwa wanafanya upambe tu hapo, yaani wanaacha ku focus kwenye issues wanaangalia cosmetics.
 
Sober

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
289
0
"Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, taarifa za kitaalamu zinasema VX inaingizwa nchini kwa thamani ya Sh100 milioni huku Mercedese Benz ikigharimu takriban Sh250 milioni."

Kwa ujumla ujumbe tumeukubali pamoja na dramatization ya facts kuhusu hizo bei...DT Dobie na International Motors wote wapo hapo mjini, kwanini waandishi wanapata uvivu hata kupiga simu?... Juzi juzi tu hapa kuna mtu alikua anataka Landcruiser Gx na akaambiwa ni over 110m kuiweka barabarani, sembuse Vx ambayo ni ya juu zaidi.
 
Indume Yene

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
2,925
1,225
Kusema kuwa Tangu Prof. Ndullu aingie BoT amekuwa akisafisha UFISADI.........Huu ni UDAKU tu. Kwani huo ufisadi wote unatokea yeye alikuwa wapi?? Naamini alikuwa hapohapo BoT akiwa msaidizi wa Balali. Kwa hiyo utumbo wote aliokuwa anafanya Balali na huyo Ndullu alikuwa ni mmoja wa washirika wa FISADIz. Msimpe sifa hasiyostahili, na yeye anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068

Let him clean "his" mess first and then he will be taken care of.
 
Indume Yene

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
2,925
1,225
Let him clean "his" mess first and then he will be taken care of.

Tunapowaachia kuendelea kushika utamu wa madaraka ndipo wanaendelea kuficha madhambi yao kwa ku-destruct ushahidi. Naamini kuna watu wengi wanaoweza kufanya hiyo kazi ya ugavana endapo na huyo Fisadi Ndullu naye atawajibishwa. Hata JK anajua kuwa jamaa ni mchafu lakini kamuweka makusudi ili afunike upupu waliofanya SISIEMU kuhusu EPA na mengineyo.
 
Mpanda Merikebu

Senior Member
Dec 27, 2007
170
195
Kusema kuwa Tangu Prof. Ndullu aingie BoT amekuwa akisafisha UFISADI.........Huu ni UDAKU tu. Kwani huo ufisadi wote unatokea yeye alikuwa wapi?? Naamini alikuwa hapohapo BoT akiwa msaidizi wa Balali. Kwa hiyo utumbo wote aliokuwa anafanya Balali na huyo Ndullu alikuwa ni mmoja wa washirika wa FISADIz. Msimpe sifa hasiyostahili, na yeye anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Mkuu Indume Yene,

Nafikiri maoni yako ni mashambulizi yasiyo ya makini kwa gavana Ndullu. Hata kama yeye alikuwa ni kati ya manaibu gavana, mwenye usemi wa mwisho alikuwa ni gavana. Hata kama Ndullu hakupenda vile Ballali alivyokuwa anaendesha BoT, angemshtaki kwa nani wakati Ballali huyo huyo ndio alikuwa mwenyekiti wa bodi?

Ninachotaka watu watambue ni kuwa kwetu sisi watazamaji, ni rahisi sana kusema kuwa jambo fulani lingetendeka kwa namna fulani. Lakini ukiwa wewe ndio mhusika mwenyewe, utaona mambo kwa namna nyingine.

Haidhuru hata kama Ndullu naye aliiendesha BoT kifisadi wakati magari haya yaliponunuliwa, je hastahili sifa kwa kujirekebisha? Je ungependelea aendelee kutumia haya mabenzi na pengine kuongeza mengine?

Ni wajibu wetu kukemea uovu unapotokea na ni wajibu wetu kutoa heko/sifa pale inapostahili. Sisi wote ni binadamu na tuna mapungufu kila kukicha. Uzuri wetu (wa kuwa wanadamu) ni kuwa tuna ufahamu wa kujifunza pale tulipopungua na kujisahihisha.

Wasalaam!
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,670
2,000
Date::12/3/2008
Vigogo wa Benki Kuu wanyang'anywa mabenzi

WAKATI uchunguzi wa ufisadi katika ujenzi wa majengo pacha (Twin Towers) ukifanyika, Gavana wa Benki Kuu (BoT) amezuia matumizi ya magari manne ya kifahari aina ya Mercedese Benz yaliyokuwa yakitumiwa na baadhi ya wakurugenzi na gavana huko nyuma.

Hatua ya kuzuia mabenzi hayo ambayo yanagharimu takriban Sh1 bilioni, imekuja wakati BoT katika siku za karibuni imekumbwa na tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Duru za uchunguzi kutoka ndani ya BoT ambazo zimethibitishwa na Gavana Profesa Benno Ndulu, zinaonyesha magari hayo ya kifahari kwa sasa yapo katika yadi ya benki hiyo kwa ajili ya matumizi maalumu.

Hivi sasa wakurugenzi wa BoT pamoja na Gavana Ndulu wanatumia gari aina ya Toyota Land Cruiser VX ili kubana matumizi.

Kwa mujibu duru hizo za uchunguzi wa Mwananchi, mabenzi hayo yalikuwa yakitumika zaidi na vigogo wa BoT wakiongozwa na aliyekuwa Gavana marehemu Daud Ballali.

Gazeti hili limebaini zaidi kwamba, marehemu Ballali alikuwa akibadili matumizi ya mabenzi kila mara pamoja na vigogo wengine.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, taarifa za kitaalamu zinasema VX inaingizwa nchini kwa thamani ya Sh100 milioni huku Mercedese Benz ikigharimu takriban Sh250 milioni.

Uchunguzi umebaini pia kuwa gharama za matumizi ya benzi kwa mafuta ni kubwa karibu mara mbili ikilinganishwa na gari aina ya Vx.

Wakati Benzi ikitumia lita moja kwa kati ya kilomita sita hadi saba, Vx hutumia lita moja kwa kati ya kilomita 6 hadi tisa, wakati gharama za vipuri vyake, kwa mfano taa ya nyuma ya benzi ni Sh 1 milioni wakati Vx ni Sh 400,000 hadi 500,00, ikiwa ni mara mbili ya benzi.

Uchunguzi huo wa kitalaamu unaonyesha kwamba wakati benzi hufanyiwa matengenezo (Service) makubwa kwa kila kilomita 10,000, Vx linahitaji matengenezo hayo baada ya kutembelea umbali wa kilomita 5,000.

Katika matengenezo hayo benzi linagharimu kati ya Sh3 hadi 4.5 milioni na Vx kati ya Sh1.5 hadi Sh 2 milioni kwa viwango vya matengenezo ya serikali.

Katika uchunguzi huo, imethibitika kwamba baada ya Profesa Ndulu kuingia madarakani Januari 9, mwaka huu, alizuia matumizi yasiyo ya ya lazima ya magari hayo kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Imethibitika pia kuwa Profesa Ndulu ambaye amekuwa akiisafisha BoT, mara nyingi amekuwa akitumia gari aina ya Toyota Landcruiser Vx na kwamba huku siku moja moja ndipo hutumia benz tena katika matukio maalum hasa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa duru hizo za habari za uchunguzi za Mwananchi Jumapili, gavana baada ya kuingia na kukuta benki ikinuka ufisadi wa aina mbalimbali, alianza kuisafisha ikiwa ni pamoja na kubana matumizi.

Alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Ndulu alikiri kuzuia matumizi ya magari hayo pasipo na sababu za msingi.

"Ni kweli yapo mabenzi manne, yamekaa nilichozuia ni matumizi yasiyokuwa na msingi kwa magari hayo," alisema gavana Profesa Ndulu.

Hata hivyo, gavana Ndulu alisema magari hayo hutumika wakati wa wageni wa BoT wa kimataifa wanaokuja kwa mwaliko maalumu wa benki hiyo kama vile Shirika la Fedha la Duniani (IMF) au Benki ya Dunia (WB).

Gavana Ndulu alisema wakati mwingine kunapokuwa na matumizi ya msingi ndipo magari hayo hutumika.

Tangu kuingia gavana Ndulu BoT imekuwa katika mabadiliko ya kutaka kuirejesha heshima na imani yake kwa wananchi, ambayo ilitoweka kutokana na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya.

Ukiacha EPA, kashfa nyingine ni ya matumizi ya zaidi ya Sh500 bilioni kwa ujenzi wa majengo pacha ya ghorofa 18 na ajira tata za watoto 16 wa vigogo.

Hata hivyo, hadi sasa tayari suala la EPA linashughulikiwa na maafisa wa BoT wanaodaiwa kuhusika katika sakata hilo walipandishwa kizimbani.

Suala lingine lilikuwa ajira tata za watoto wa vigogo ambali lishachunguzwa na kumalizwa, huku ukaguzi majengo pacha ukiendelea kufanywa na Kampuni ya wazalendo.

Magari hayo ya kifahari ambayo yalinunuliwa BoT ni sehemu ya magari 40,000 ya serikali, ambayo miongoni mwao 15 ni kati ya Vx na GX ambayo yanapaswa kupunguzwa.

Kichwa cha habari kinasema wamenyang'anywa mabenzi na mimi baada ya kuisoma habari yote naona ni kwamba matumizi ya mabenzi hayo yamepunguzwa....Na madai ni kwamba yatatumika wakati muhimu tu.
Wasipokuwa makini wanaweza wakawa wameongezea matumizi badala ya kupunguza kwasababu hicho kipimo cha "Wakati muhimu" kinaweza kisizingatiwe...Ama matukio yasiyo ya muhimu yanafanywa ya muhimu ni jambo la kawaida kwenye ufujaji wa pesa za umma.
Na pia hawaja specify kama hayo magari ni ya diesel ama petrol kwasababu hapo issue inakuwa tofauti sana tena inapokuja kwenye vipuri ndiyo utofauti mkubwa sana kati ya magari ya diesel na petrol.

Vipi kuhusu gharama za insurance? Kama wanataka kuzungumzia kuhusu kuprevent ufujaji wa pesa za umma basi wanahitaji darasa.
 
Kinyambiss

JF-Expert Member
Dec 2, 2007
1,374
1,225
Huu ni ujinga tuu.. This is PR thing.. everyone knows it, Spare za benz while more expensive, last much longer than VX parts. I own a merc and a VX na zote zinakula mafuta mbaya, tena bora merc..lol.. In short Benno hataki kuonekana kuwa yeye na ma Director wenzake wanatanua... an BOT wanatumia S class na E class merc... non of which cost 250 million.. especially considering the fact that serikali hailipi ushuru.. this article ni UDAKU..
For 250 million u can get a used rolls royce phantom.
 
Lunanilo

JF-Expert Member
Feb 15, 2008
370
195
Kusema kuwa Tangu Prof. Ndullu aingie BoT amekuwa akisafisha UFISADI.........Huu ni UDAKU tu. Kwani huo ufisadi wote unatokea yeye alikuwa wapi?? Naamini alikuwa hapohapo BoT akiwa msaidizi wa Balali. Kwa hiyo utumbo wote aliokuwa anafanya Balali na huyo Ndullu alikuwa ni mmoja wa washirika wa FISADIz. Msimpe sifa hasiyostahili, na yeye anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.

Prof Ndulu has never worked under Balali. Never.
 
PatPending

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
490
170
So much inaccuracies as far as the vehicles' information is concerned. Unless they are talking about Merc with 4L plus engines, Mercs are generally more fuel efficient than the gas guzzling LCs. Kama kweli Ndullu anataka kupunguza matumizi mbona haanzi na kupunguza idadi ya magari na madereva kwa ajili yake na manaibu wake pekee?
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,300
2,000
Mkuu Pundit, nakubaliana na wewe hawa jamaa wameshikishwa kidogo wanaacha kuzungumzia issues za msingi wamekwenda kwenye peripherals!! Tujadili uwezo wa kampuni ambazo huyu gavana ameziajili kufanya uchunguzi wa Twin Towers!! Huyu mwalimu wa chuo cha Ardhi anayemiliki hiyo Mekon kweli ana uwezo wa kufanya hiyo kazi? Huyu architect yuko karibu sana na watu wa ccm na safari nyingi za wafanya biashshra wazarendo wanaosafiri na muungwana huwa anajumuishwa na pia ana close links na Lowassa sasa hapo mnategemea ripoti gani jamani? Kwanini wasiwape internationally recognized firm ambayo haiwezi kuyumbishwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom