VIGOGO TIE WAFYEKWA: Ni kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye vitabu vya kujifunzia

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
735
b1a1ce9f587423d8f2521253196e12ce.jpg

==========
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Waziri Ndalichako ametangaza hatua hiyo kufuatia kuibuka kwa mjadala bungeni leo jioni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia. Miongoni mwa makosa yaliyobainika kwenye vitabu hivyo, ni kurasa ulioandikwa kuwa Dodoma ndio mji mkubwa Tanzania.

Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Wabunge walitishia kuzuia kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu hadi hapo wizara itakapotoa uamuzi wenye mantiki katika kutatua tatizo hilo lililozua mvutano mkubwa.

“Kwa mamlaka niliyonayo, namuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako

Baada ya waziri kutoa agizo hilo, wabunge waliridhia kupitisha bajeti ya wizara hiyo.
 
Sawa tu, maana elimu yetu haina mbadala ni lazima weredi uzingatiwe na uzalendo.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo Jumatatu jioni amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Hilo wala halisaidii kimsingi. Kwa nini uadhibu watu kwa kufanya kazi uliyowapa ambayo HAWAIWEZI? Hata hapo wamejitahidi sana. Suala la msingi ni kuwa hiyo kazi hawaiwezi. Nyie mlisema Taasisi ndio PEKEE watakaokuwa wakiandika vitabu kwa ajili ya shule - sasa si mliamini kuwa wanaweza? Sio wao walioomba kufanya kazi hiyo. Halafu kulikuwa na mbwembwe nyingi kwamba, wana waandishi waliobobea nk. ------- Kama bado wanaamini katika uamuzi wao basi waseme pia kuwa hakuna anayeruhusiwa kuwa na kampuni ya simu, viwanda, mashamba, nk, bali ni mashirika ya serikali pekee ndiyo yatakayofanya shughuli hizo. ----- STATE MONOPOLY WILL NEVER WORK. Watajifunza lini?
 
Huyo aliyewafyeka naye anatakiwa kufyekwa maana sheria inasema yeye pia anahusika kuruhusu kuchapishwa hivyo vitabu. Iweje awawajibishe wenzie? Yeye anawajibishwa na nani?
 
Mchakato wa uandishi wa vitabu na uchapishaji wake ni process ili kupata kitabu chenye ubora.Kuwatumbua hao jamaa haitosaidia kupata kitabu kisicho na makosa.Nipo huku kisarawe nabugia chaki wakati ni mbobezi katika hayo mambo ya uchapishaji.Tupatieni hizo nafasi mama Ndalichako na hayo mambo madogo Mpaka waje wachina?.
 
Hilo wala halisaidii kimsingi. Kwa nini uadhibu watu kwa kufanya kazi uliyowapa ambayo HAWAIWEZI? Hata hapo wamejitahidi sana. Suala la msingi ni kuwa hiyo kazi hawaiwezi. Nyie mlisema Taasisi ndio PEKEE watakaokuwa wakiandika vitabu kwa ajili ya shule - sasa si mliamini kuwa wanaweza? Sio wao walioomba kufanya kazi hiyo. Halafu kulikuwa na mbwembwe nyingi kwamba, wana waandishi waliobobea nk. ------- Kama bado wanaamini katika uamuzi wao basi waseme pia kuwa hakuna anayeruhusiwa kuwa na kampuni ya simu, viwanda, mashamba, nk, bali ni mashirika ya serikali pekee ndiyo yatakayofanya shughuli hizo. ----- STATE MONOPOLY WILL NEVER WORK. Watajifunza lini?
WAALIMU TUSAIDIENI,KUNA VITABU VYA KIADA NA ZIADA,NAAMINI HAWAJAZUIA WATU WENGINE KUTUNGA AU KUCHAPA VIATBU VYOTE NAAMINI WAMEAMUA KUWA NA SARE YA VITABU KWENYE SHULE,HASA ZA SERIKALI NA HASA VITABU VYA KIADA.
NACHOKIONA KWA HARAKA NI KWAMBA WATUNZI MAHILI WA ZAMANI WENGI WAMESTAFU NA NDO HAO WAPO SEKTA BINAFSI BAADA YA SERIKALI YA AWAMU ZILIZOPITA KURUHUSU KILA SHULE KUCHAGUA MTUNZI.
 
PIA UMAKINI HAUKUWEPO KWENYE KAZI NZIMA
WAALIMU TUSAIDIENI,KUNA VITABU VYA KIADA NA ZIADA,NAAMINI HAWAJAZUIA WATU WENGINE KUTUNGA AU KUCHAPA VIATBU VYOTE NAAMINI WAMEAMUA KUWA NA SARE YA VITABU KWENYE SHULE,HASA ZA SERIKALI NA HASA VITABU VYA KIADA.
NACHOKIONA KWA HARAKA NI KWAMBA WATUNZI MAHILI WA ZAMANI WENGI WAMESTAFU NA NDO HAO WAPO SEKTA BINAFSI BAADA YA SERIKALI YA AWAMU ZILIZOPITA KURUHUSU KILA SHULE KUCHAGUA MTUNZI.[/QUOTE
 
WAALIMU TUSAIDIENI,KUNA VITABU VYA KIADA NA ZIADA,NAAMINI HAWAJAZUIA WATU WENGINE KUTUNGA AU KUCHAPA VIATBU VYOTE NAAMINI WAMEAMUA KUWA NA SARE YA VITABU KWENYE SHULE,HASA ZA SERIKALI NA HASA VITABU VYA KIADA.
NACHOKIONA KWA HARAKA NI KWAMBA WATUNZI MAHILI WA ZAMANI WENGI WAMESTAFU NA NDO HAO WAPO SEKTA BINAFSI BAADA YA SERIKALI YA AWAMU ZILIZOPITA KURUHUSU KILA SHULE KUCHAGUA MTUNZI.[/QUOTE Uamuzi waliopitisha Conservative3 ni kuwa ni TET peke yao ndio wanaoruhusiwa kuandika vitabu vya kiada (vitabu rasmi vya kutumika kwenye kila somo). Wengine wote ruksa kuandika vya ziada. Shida ni kuwa kigezo cha kufikia uamuzi huu kilikuwa kwamba watu wengine ni makanjanja (hawana uwezo wa kuandika vitabu bora) --- jambo ambalo ni uongo mkubwa - matokeo yake TET ndio wanaodhihirisha kuwa wao ndio hoi kabisa.
 
Back
Top Bottom