Vigogo Tanzania-wamkumbatia Mgiriki aliyefukuzwa nchini

E

engmtolera

Verified Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
5,111
Likes
85
Points
145
E

engmtolera

Verified Member
Joined Oct 21, 2010
5,111 85 145
Haya tena

kama kawaida watoto wa vigogo na vigogo wameamuwa kumkumbatia Mgiriki aliyefukuzwa nchini Tanzania,inasemekana wanamtafutia vibari vya kufanyia kazi hapa Tanzania ili aweza kusafirisha na kuuwa wanyama wetu atakavyo

hivi hawa wanaojiita watoto wa vigogo wanania gani na nchi hii? jamani tuamke ikiwezekana tupambane hadi kieleweke tumechoka na hao wanaojiita vigogo
 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Likes
101
Points
145
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 101 145
Haya tena

kama kawaida watoto wa vigogo na vigogo wameamuwa kumkumbatia Mgiriki aliyefukuzwa nchini Tanzania,inasemekana wanamtafutia vibari vya kufanyia kazi hapa Tanzania ili aweza kusafirisha na kuuwa wanyama wetu atakavyo

hivi hawa wanaojiita watoto wa vigogo wanania gani na nchi hii? jamani tuamke ikiwezekana tupambane hadi kieleweke tumechoka na hao wanaojiita vigogo
Miaka 12 tokea Baba wa Taifa kututoka,

Kumekuwa na matukio mbalimbali ya ajabu ajabu sana esp kwa viongozi wetu huko serikalini hii ni wazi kabisi walikuwa wana nidhamu ya woga wakati wa mwalimu au watataka kutuambia mwalimu alikuwa dictator? au?? Nadhani kuna baadhi ya viongozi walipo sikia baba wa taifa hatunae tena ndani ya nafsi zao waliona ndio mahali pa kuwa finyanga watanzania sasa na kuwaacha maskini am sorry to say this lakini in valid sense kwajinsi ya wakati wa mwalimu alivyo kuwa hai na hayupo sasa inajionyesha wazi kabisa kunautofauti wa mambo na viongozi wetu walikuwa ni waoga kuthubutu kufanya jambo na walikuwa wakijua fika yakimfikia Mwalimu anawaumbua tena hadharani.

Ingawa sipingi kuwa mwalimu nae alikuwa anamapungufu yake laki ya hawa viongozi wetu wa sasa ni mapungufu makubwa na yanawanyonya wananchi badala ya kuwajenga eg viongozi wa sasa wao sera yao kuu ni kukimbilia wawekezaji nasio kutafuta mbinu mbala za kujitegemea kwa angalau 40% sisi wenyewe twakalia kuwaza misaada na hata misaada tuipatayo twala sasa hapo si upuuzi kabisa huo kwanini wananchi wasi lalame?na kuwaambia viongozi wao ukweli . kitu kidogo tu kama hiki cha kumfukuza raia ambae hatakiwi yet wanamtetea?
 
R

Rodgers

Senior Member
Joined
Nov 25, 2009
Messages
139
Likes
61
Points
45
R

Rodgers

Senior Member
Joined Nov 25, 2009
139 61 45
Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa aina ya uongozi tuliokuwa nao sasa hata iweje hautaweza asilani kuifanya Tanzania ijetegemee japo kwa asilimia 40% kama mwenzangu alivyoshauri. Kwa wale ambao kwenye miaka ya 1980 na kuendelea walikuwa na umri wa ufahamu ni dhahiri kuwa watakubaliana namimi kuwa walao tulishaonyesha uelekeo. Mathalani Tanzania ya nyakati hizo ilikuwa inamiliki kiwanda cha ku-assemble SCANIA pale Kibaha (TAMCO) , tairi zilizokuwa zinatumika zilizalishwa hapahapa na Kiwanda cha General Tiyers, spring zilitoka TASIA , Radiators zilitoka Afro cooling, Batteries zilitoka Yuasa - Yote hayo yalikuwa makampuni ya Kitanzania ambayo yote kwa sasa yamefungwa. Pia tulikuwa na viwanda -vya ku- assemble Radio aina ya National & Philips.
Kwa upande mwingine kiwango cha matumizi ya Trekta kwenye kilimo pia kilianza kutoa uelekeo badala ya hizi Power Tiller zinazopigiwa upatu kisanii.

Leo hii Tanzania inasafirisha magogo ya (Hardwood) nje ya nchi na fedha inayoingia tunaagiza Tooth-pick (Fedhehaaaaa!!!!!!!!!!!!) Tanzania nchi inayomiliki asilimia 17% ya vyanzo vyote vya maji baridi duniani inakabiliwa na tatizo kubwa la maji kuanzia mijini hadi vijijini. Kiwango cha watu wasiojua kusoma na kuandika kilipungua hadi asilimia 9.6% kwenye miaka ya '80 leo kimepanda na kufikia asilimia 32%

hali hii itaendelea hadi lini. ni sisi wenyewe wa kuhamua
 
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
8,212
Likes
4,351
Points
280
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
8,212 4,351 280

Hapo mkuu umenena!

Yaani TZ ya wakati huo ilionesha mwelekeo wa kuelekea kwenye mafanikio. Ghafla tumaini letu likatoweka! Sasa tunahaha na hawa wasanii wetu sijui lini tutafika? Mataili yalikuwa yenye ubora wa juu, redio za Philips na National zilikuwa za kiwango, springs nazo usiseme sasa yote yamebaki historia.

Bila kuwang'oa hawa mafedhuri hapa hatuchomoki. Mzee wa kulialia amebaki kupiga projo tu na power tillers zake hapo kilimo lini kitainuka? Wawekezaji wameigeuza nchi yetu shamba la bibi, tena bibi mwenyewe yule kikongwe hasa!

Tunaomba tupate mtu mmoja tu wa kutupa mwongozo!!
 
Forum statistics

Threads 1,236,877
Members 475,318
Posts 29,270,623