Vigogo ndani ya ofisi hawataki kijana afanye maamuzi kupitia baba yake

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,188
Legacy ya maisha ya kijana wako unaiandaa mzazi na wazazi wengi mnawekeza kwenye elimu na siyo assets, ila asset kijana huzikuta kama matokeo katika utendaji wako.

Mpambano wa legacy unaanzia ulipoonjeshwa utamu wa mali, mzazi umekuwa meneja mkubwa, leo kijana bado hajawa na mali tayari umempa cheo cha chini yako naye anaitwa boss mtoto.

Huyu lazima aungane na wewe pale anapoona kuna mtu ofisi hiyohiyo anataka kumkwamisha kufanya maamuzi au jambo lolote zuri au baya, maana vigogo wote waliopo hapo wanaona kijana wa jana inakuwaje anataka kufanya maamuzi kiasi hiki?.

Mtifuano unaanzia hapo ile legacy ya mtoto ambao ulipaswa achague mwenyewe akiwa mkubwa but mzazi amelazimisha kijana aingie kwenye zizi ambalo labda haikuwa haiba yake.

Vigogo ndani ya ofisi hawataki kijana afanye maamuzi na kijana kupitia babaake anaamua liwalo na liwe haiwezekani hawa, nitawaonyoosha tu.

Huku chini na nje mesenja na madereva hawajui nini kinaendelea ila wanapata fununu nao wanaingia kwenye kusubili atakaye dondosha mfupa wao waokote bado kundi kubwa zaidi la wananchi.

Yangu ni hayo tu kuelekea nchi ya ahadi.
 
Ndiyo maana nikabandika.

Ukishindwa kufungua hiyo fasihi au siku hizi mnaita code nitafute baadae.
Yeye haoni Makonda, Sabaya na watoto wa mwendazake (watoto katika uongozi), walivyofikia hatua hadi ya kuwadharau wenye vyeo vya juu yao? Rejea Makonda akiwaambia mawaziri kuwa hata mkuu wenu....
 
Unamsema Kheri James, Ole Sabaya, Daudi Albert Bashite, Ally Hapi, Albert Chalamila na Mpwa kwa mafumbo mkuu?

Ila mmoja ameshaomba radhi tayari, bado hao wengine.
 
Maslahi na ukubwa!
Mzee wetu kakata moto now ameamua kupambana na huyu Madame kisa na mkasa hatujui.

That why wachambuzi na mimi nikiwepo tunaona huyo chigogo ni vigogo waliokosa nyadhifa na ndiyo wanapeleka hasira kwa kila tawala ya nchi hii kisa madaraka.
 
Back
Top Bottom