Vigogo kitanzini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
JK, kama kweli una nia ya kuwashughulikia mafisadi basi Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyetu na wale tusiokuwa na vyama tutakuunga mkono katika juhudi zako za kupambana na ufisadi na kuutokomeza kabisa. Wananchi tutafurahi kuona mafisadi wote wanafunguliwa mashtaka na kufilisiwa pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha utajiri wao umepatikana kwa njia za haramu. Pia tutafurahi kuona aliyekuwa Gavana wa BoT Balalli anarudishwa haraka nchini ili kujibu tuhuma za ufisadi dhidi yake.

Tunataka kuona Tanzania ambayo haitakuwa na
watu ambao wako juu ya sheria na hata wakifanya madhambi sheria haiwagusi.


Vigogo kitanzini

na Ratifa Baranyikwa na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SASA ni dhahiri kuwa Rais Jakaya Kikwete amedhamiria kuandika historia mpya kwa kuwa rais wa kwanza wa Tanzania kumfikisha mahakamani mtangulizi wake.

Ingawa hatua hiyo inaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa inaweza kuwa na athari mbaya kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na serikali anayoiongoza, inabaki kuwa nguzo yake kuu ya kurejesha imani kwa wananchi wanaotaka kuona akitekeleza ahadi zake kama ambavyo amekuwa akiahidi mara kwa mara.

Tamko la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Alhamisi, Aprili 24, bungeni Dodoma, kuwa inafuatilia taarifa za tuhuma kuhusu matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu, na iwapo ikithibitika kuwa walitenda makosa, watachukuliwa hatua zinazostahili, linaonyesha kuwa sasa Mkapa anaweza kufikishwa mahakamani.

Katika kuonyesha dhamira ya dhati ya serikali yake kuhakikisha inatekeleza matakwa ya wananchi ya kutaka kuwepo uchunguzi kwa viongozi wa juu serikalini wanaotuhumiwa kutumia madaraka yao vibaya, Rais Kikwete jana aliwaambia waandishi wa habari kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, kuwa juhudi za kupambana na vitendo vya rushwa zinaendelezwa bila ajizi.

Rais Jakaya Kikwete, ambaye jana aliongoza mamia ya Watanzania kuadhimisha miaka 44 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, sherehe zilizofanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam bila kuwepo kwa mtangulizi wake, Mkapa, aliwaomba wananchi kushirikiana na serikali yake katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa Ikulu, alisema mafanikio ya mapambano yanayoonekana hivi sasa yanategemea zaidi ushirikiano wa wafanyakazi na akawataka kuwa mstari wa mbele katika harakati hizo.

Aidha, aliwataka kuzingatia kujiepusha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa, kwa sababu nao wananung’unikiwa na umma kujihusisha navyo.

Taarifa hiyo ambayo Kikwete anaeleza kuwa hatakuwepo katika maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi, ilieleza kuwa wafanyakazi wakiipiga vita rushwa, vigogo wanaodaiwa kupokea rushwa watapata wakati mgumu wa kufanikisha vitendo vyao viovu.

“Rais amewaomba wafanyakazi wafanye mambo matatu, kwanza, wajiepushe wao wenyewe na vitendo vya rushwa….wakatae kutumika katika vitendo vya rushwa…na wasaidie kutoa taarifa za rushwa ili zifanyiwe kazi na wahusika wabanwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ya Rais Kikwete.

Tamko hili la Rais Kikwete ambaye jana alitangaza kutohudhuria sherehe za Mei Mosi kutokana na kuwa safarini katika nchi za Uganda na Ethiopia, limetafsiriwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa hatua yake ya kwanza ya kuuthibitishia umma wa wafanyakazi kuwa hakuna kiongozi atakayesalimika kama atabainika kuhusishwa na rushwa.

Aidha, walieleza kuwa Rais Kikwete amelazimika kutoa tamko hilo ili kupoza dukuduku la wafanyakazi kuonyesha hasira yao kwa serikali katika maadhimisho hayo, jambo linaloweza kuzidi kujenga taswira mbaya kwa serikali yake.

Pamoja na Mkapa, tamko la Waziri Mkuu Pinda, sambamba na lililotolewa jana na Rais Kikwete, yanonyesha kuwa viongozi wengine waandamizi walio katika hatari ya kufikishwa mahakamani iwapo tuhuma zinazoelekezwa kwao zitathibitika kuwa kweli, ni pamoja na Andrew Chenge na Basil Mramba, ambao walikuwa mihimili na washauri wa karibu wa Mkapa wakati wa utawala wake.

Tayari Chenge ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri hivi karibuni ameanza kuchunguzwa kwa tuhuma za kuhusika na kashfa za rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo Tanzania iliuziwa na Kampuni ya BAE ya nchini Uingereza.

Wachambuzi wameeleza kuwa iwapo Mkapa na Chenge watathibitika kuhusika na makosa ya jinai, basi haitakuwa rahisi kwa Mramba kuachwa pembeni kwa sababu alikuwa mshauri mkuu wa masuala ya fedha wa Mkapa.

Katika hatua nyingine, kutoonekana na ukimya wa sasa wa Mkapa umeanza kuzusha hisia tofauti miongoni mwa jamii.

Mkapa jana pia hakuonekana katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya Muungano huku viongozi wengine wastaafu wakihudhuria sherehe hizo.

Ukiacha Mkapa, viongozi wastatafu waliohudhuria ni Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Haikufahamika hasa sababu za kutohudhuria kwa Mkapa katika sherehe hizo, ikiwa ni mara ya pili kukosekana katika matukio makubwa ya kitaifa na yale yanayokihusu chama chake, ambacho alikuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka kumi.

Mkapa hakuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika Butiama, mkoani Mara mwishoni mwa Machi, mwaka huu.

Wadadisi na wachambuzi waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili walieleza kushangazwa kwao na kutoonekana kwa Mkapa katika matukio hayo makubwa ya kitaifa na kichama na kudai kuwa huenda kunasababishwa na uzito wa tuhuma zinazomkabili.

Baadhi ya tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkapa ni pamoja na kumiliki Kampuni ya kuzalisha umeme ya Tanpower Resources Ltd, ambayo ilishinda zabuni ya kununua mradi wa kuzalisha umeme kutoka mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ulioko Mbeya.

Madai hayo ambayo ni miongoni mwa yale yaliyoelezwa kuchunguzwa na Serikali, yanaelezwa kuwa huenda ni moja kati ya mambo yanayomkosesha raha kiongozi huyo na kumfanya ashindwe kujumuika na viongozi wenzake hata katika masuala muhimu.

Aidha, sherehe hizo za muungano ambazo jana zilifanyika kwa mbwembwe za aina yake, hazikuhudhuriwa pia na viongozi wengine wa vyama vya siasa.

Watu wengine mashuhuri ambao hawakuhudhuria sherehe hizo ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Andrew Chenge.

Matukio ya jana yalivuta hisia za wengi katika sherehe hizo zilizoanza majira ya saa 4:05 asubuhi, baada ya Rais Kikwete kuwasili uwanjani hapo akiwa katika gari la wazi pamoja na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange.

Wakati akiingia uwanjani, rais aliweza kuvumilia mvua iliyokuwa ikinyesha.

Sherehe hizo pia zilipambwa na mbwembwe za helikopta za jeshi pamoja na ndege za usafirishaji zilizopita uwanjani hapo zikitokea upande wa kaskazini mwa uwanja huo.

Katika kuadhimisha sherehe hizo, Rais Kikwete jana alitoa msamaha kwa wafungwa 3,300.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, kwa vyombo vya habari, ilisema msamaha huo utahusu wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya miaka mitano.

Alisema msamaha huo utawahusu wafungwa wazee na wenye umri zaidi ya miaka 40, lakini hauwagusi wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, waliokamatwa na dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, wanaotumikia kifungo cha maisha, kujamiana na wenye makosa ya kuwapa mimba wanafunzi.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 11 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Mkapa lazima tumfunge, tusipomfunga yeye basi watoto wake. Haiwezekani ukala pesa za masikini halafu mtu aachwe hivi hivi. Huyu lazima jeuri yake tuikomeshe. Rais kikwete akishindwa atuambie sisi wananchi ili tumshughulikie. Pesa yote anayopewa ya kustaafu haimtoshi mpaka analiibia taifa kiasi hiki!!!!!! BASILI MRAMBA TUNAJUA NDO ANAMILIKI KIBO HOTELI PALE ARUSHA. HUYU NAYE LAZIMA ACHUNGUZWE. ALIZITOA WAPI HIZO HELA WAKATI UKOO WAKE NI MASKINI KAMA WATANZANIA WENGINE. KUZAA WATOTO NA MAMA MKAPA NDO IKAWA DILI YA WAO NA MKAPA KUTUIBIA. LAZIMA TUWAKOMESHE. RAIS ASIPOWAKOMESHA, WANANCHI TUKO TAYARI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

na Methew, Dar, - 27.04.08 @ 10:43 | #8968

Mkapa lazima tumfunge, tusipomfunga yeye basi watoto wake. Haiwezekani ukala pesa za masikini halafu mtu aachwe hivi hivi. Huyu lazima jeuri yake tuikomeshe. Rais kikwete akishindwa atuambie sisi wananchi ili tumshughulikie. Pesa yote anayopewa ya kustaafu haimtoshi mpaka analiibia taifa kiasi hiki!!!!!! BASILI MRAMBA TUNAJUA NDO ANAMILIKI KIBO PALACE HOTELI PALE ARUSHA. HUYU NAYE LAZIMA ACHUNGUZWE. ALIZITOA WAPI HIZO HELA WAKATI UKOO WAKE NI MASKINI KAMA WATANZANIA WENGINE. KUZAA WATOTO NA MAMA MKAPA NDO IKAWA DILI YA WAO NA MKAPA KUTUIBIA. LAZIMA TUWAKOMESHE. RAIS ASIPOWAKOMESHA, WANANCHI TUKO TAYARI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

na Methew, Dar, - 27.04.08 @ 10:45 | #8969

WALE WANAOBAINIKA,
WASULUBISHWE, WASULUBISHWE,
KAMA WANVYOTUSULUBISHA

MASHULE HAYANA MADAWATI
HOSPITALI HAZINA MADAWA
MADAKTARI WETU WAMEKATA TAMAA
WALIMU WETU WAMEKATA TAMAA
VIONGOZI SAFI WASIOKUWA MAFISADI WANAKATA TAMAA

SHERIA NA HAKI VIACHIWE VICHUKUE MKONDO WAKE

VYOMBO VYOTE VYA DOLA VIACHIWE VIFANYE KAZI KIKAMILIFU, KWA KUFUATA SHERIA BILA KUINGILIWA

HAYA YAKITEKELEZWA, WANANCHI TUTAREJESHA IMANI

TUTAFANYA KAZI KWA JUHUDI KUBWA
TAIFA LITASONGA MBELE KIUCHUMI

MH RAIS TEKELEZA,
UMMA WA WATANZANIA SAFI UPO NYUMA YAKO
VIONGOZI WAKONGWE WA ZAMANI WAPO NYUMA YAKO
JUMUIA ZA KIMATAIFA ZIPO NYUMA YAKO
VYOMBO VYOTE VYA DOLA VIPO NYUMA YAKO

INAWEZEKANA

JITENGE NA MAFISADI

na G.A. Kilimwano, Kijitonyama, DSM, - 27.04.08 @ 11:07 | #8973

kikwete raisi wangu mpenzi lazima uondowe uvivu kwa huyu mkapa katutowa kapa watanzania sasa atakula jeuri yake kiongozi huyu ni jeuri ***** fisadi kauwa watu bila hatia watu walikuwa wanaandamana kwa amani kudai haki yao ya kikatiba leo kwa ujeuri wako tu umewauwa sasa mungu kakupa laana na kweli sasa bora chizi kwa dhamani kuliko muwaji wewe ewe mwenyezimungu endelea kumuadhiri huyu fisadi

na king, tz, - 27.04.08 @ 11:19 | #8978

Mzee huyu kwanza atengwe kanisani anakosali, maana kuungama kwa Padri haitoshi kama hatajitokeza kuwaomba msamaha watanzania walio wengi na kurudisha migodi ya Mbeya jambo ambalo anaweza kulifanya na umma ukafikilia kumsamehe.

Majina ya mashule na majengo yaliyoitwa kwa jina lake, bila ridhaa ya watanzania ambao aliwakosea yabadilishwe, maana jina limenajisika ktk jamii.
Amemsaliti Nyerere ambaye nusura sehemu zingine alitaka kupigwa mawe kwa kulitetea jina lake,baada ya kufa 'Mkapa'akajichafua na kibaya ZAIDI akawachafua wasaidizi wake wa karibu ambao 'walianza kula bila kunawa' na kusugua midomo chini kama 'nguruwe mwitu'.

Kumfunga haitasaidia,maana atakuwa sehemu maalumu,jambo muhimu ni kuchukua alivyovichukua na kumtenga ktk jamii.

Kiongozi mmoja katika visiwa vidogo vya 'SAMOA' alipoukosea umma alitengwa bila kualikwa au kuhudhuria sherehe mpaka alipoomba msamaha kwa umma!.

Alipoingia madarakani alitangaza mali alipotoka ameona mzigo wa kutangaza, alishinikiza kuuza nyumba za watanzania ktk maeneo muhimu ya nchi na kusababisha usumbufu kwa walio nunua pindi nguvu ya UMMA/ saa ya ukombozi itakapofika na wananchi kuzidai kwa nguvu!

na Bwato Mwende Kihulo, NewZeland, - 27.04.08 @ 12:23 | #8982

MH RAIS
ILI KUKWEPA LAWAMA,
JITENGE PEMBENI NA HAWA MAFISADI

CHAPA KAZI, ONGOZA WATANZANIA BILA HOFU YOYOTE

ONGOZA TAIFA KWA UADILIFU NA UNYOFU,
HII NDIYO ILIYOKUWA SIRI YA JK NYERERE KUWA MAARUFU

WAKONGWE NA MASHUJAA WA TAIFA HILI WALIOKUWA SAFI WOTE WAPO NYUMA YAKO (KINA KAWAWA, MSUYA, WARIOBA, SALIM n.k.)

CHA MSINGI ACHIA VYOMBO VYA DOLA VIFANYE KAZI BILA KUINGILIWA, USIUMIZE KICHWA CHAKO

UNAPOJARIBU KUWALINDA UTAJICHAFUA

KAMA ILIWEZEKANA KUREJESHA MALI YA WATANZANIA KUTOKA MIKONONI MWA WAKOLONI, KWA NINI ISIWEZEKANE KUREJESHA MALI YA WATANZANIA KUTOKA MIKONONI MWA MAFISADI?

LAKINI

SHERIA IFUATWE

na R. Shenawi, Ubungo, DSM, - 27.04.08 @ 13:06 | #8987

INGEKUWA VIZURI AKAMSHITAKI ILI NA YEYE AKIMALIZA MUDA WAKE WA URAIS ASHUGHULIKIWE VILEVILE.ILA HAKUNA LOLOTE LITAKALOFANYIKA MNAZUGWA TU WADANGANYIKA MAANA WAMESHAWAJUA MNAPENDA SANA STORI BILA VITENDO.KWANI WALIOKWISHA WAJIBIKA KUNA NINI TENA?MTABAKIA KUSIKIA TUME IMEWASILISHA MAPENDEKEZO ILA TUMEUNDA KAMATI KUSHAURI KISHA TUUNDE TASK FORCE KUIMPLIMENTI..WAJINGA NYIE UTAIBANAJE SERIKALI ILIYOPITA WAKATI YEYE MWENYEWE KIKWETE ALIKUWA MMOJA WA SERIKALI HIYO?MSHITAKI MKAPA UONE KAMA KUNA ATAKAE SALIMIKA KTK SERIKALI ILIYOPITA.UTALALAMIKIA VIPI MIKATABA MIBOVU WAKATI WAWEKEZAJI WALITAFUTWA NA KIKWETE NA BALOZI ZAKE AKIWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE?UTAMTENGA VIPI NA MIKATABA MIBOVU?
MKAPA ANAAKILI NDIO MANA HATAKI KUONGEA NA MAKANJANJA MANA ANAWAJUA WALIVYOMABINGWA WA KUGEUZA MANENO.PALE MMEKWAA KISIKI MANA NA YEYE ALIKUWA KWENYE TAALUMA HIYO ANAUJUA USANII WOTE, WACHEZEENI WAKINA CHENGE WASIOJUA UJANJA WENU.KWASASA HATA WAANDISHI MNACHEZESHWA NGOMA MSIOIJUA KUMCHAFUA MKAPA ILA MJUE WALIOLIANZISHA HILO WANALIPWA VIZURI KAZI KWENU NYIE MLIODANDIA TU NA KUSHABIKIA.MWISHONI MTAONA HAYA MAANA HAKUNA HATA MOJA MNALOLIFIKIRIA LITATOKEA.

na chadu, rahaleo, - 27.04.08 @ 13:13 | #8989

Tunasubiri nini kumweka msalabani huyu Mkapa si tayari tumejua ametuibia Kiwira Coal Mine, kaanzisha ANBEN katuibia KIlimanjaro International Airport na mkewe na mdudu mengine tumpeleke akalindwe na Zombe huko gerezani ametuibia mno roho inauma sana

na Mponjoli, Arusha, - 27.04.08 @ 13:19 | #8992

Chadu, rahaleo, - 27.04.08 @ 13:13 | #8989,

Kwa taarifa yako Zambia iliwezekana kumshitaki Chiluba kwa tuhuma za ufisadi na nchi sasa inasonga mbele.

Usitake kutisha watu.
Ulimwengu unakwenda ukibadilika. Uliwengu wa leo siyo wa jana. Kama unadhani haiwezekani basi itawezekana

Watanzania wa leo siyo watanzania wa jana

Tuhuma hizi za ufisadi hazivumiliki

Nahisi kwamba NA WEWE NI FISADI

na chadudu, rahakesho, - 27.04.08 @ 13:26 | #8993

Thinking the unthinkable,sinking the unsinkable MV Ufisadi

na gonga, maswa, - 27.04.08 @ 13:50 | #8998

Jamani watanzania msidanganywe na hawa wasanii kwani hakuna lolote litakaloendelea hapa ni kudanganyana na siku zisonge mbele, utasikia kamati imegundua mambo mengi halafu itaundwa kamati ya kupendekeza mambo mengi yafanikishwaje baada ya hapo pindisha atasema apewe muda ili acheki kama ni jinai au madai baada ya hapo atasema wanapesa nyingi ukiwapeleka mahakamani watakushinda then litaachwa na kuibuliwa lingine na sisi watanzani tulivyo mashabiki tutusahau hili na kuamia kwenye jipya,kwa mtazamo wangu kikwete hana sera za kuleta maendeleo hivy hili msioji sana anafanya nini juu ya maendeleo ya nchi anatumia ufisadi kuteka mawazo yetu na tumesahau kuhoji serikali imefanya nini mpaka sasa hivi kwani kilakitu hakiendi sawa. 0757-670808

na mtanganyika, tanganyika, - 27.04.08 @ 14:55 | #9005
 
JK anakwepa maswali magumu, what a bus****. Hizo safari ni muhimu kuliko kuwaambia waliomchagua uso kwa uso.

Kwanini anaona haya na kutumia vibaraka wake? Je, huko anakokwenda nani analipia safari yake? kweli tumepata mkwere.
 
Hizi ahadi zimekuwa mbona nyingi ,sasa inaonyesha WaTz tumeanza kushika kasi ya kuongozwa kwa ahadi.
Kuna watu waliohusika na kuzjiuzulu na hawa wa sasa wameanza kukata miezi na hakuna jipya,hivi wakishajiuzulu ndio yamekwisha ,sasa hapa sijui kwa Mkwapa kutatendeka kitendo gani cha ushujaa ,maana haieleweki yeye atajiuzulu kitu gani ?? Hongera Watanzania wote waliojumuika katika sherehe za muungano ila kudumu kwa Muungano isiwe kisingizio cha kuwauwa Wapemba.
 
Mimi bado ninayo matumaini na JK pamoja na kwamba kavuruga sehemu nyingi. Kifupi tatizo kubwa la nafasi yake (rais) ni pale anapojiuliza nani msafi?..
Binafsi nipo radhi kumsamehe yeye kwa yote yaliyokwisha tokea in exchange ya Mafisadi na kura yangu ataipata hata kama haitaweza badilisha matokeo mwaka 2010.
 
Binafsi nipo radhi kumsamehe yeye kwa yote yaliyokwisha tokea in exchange ya Mafisadi na kura yangu ataipata hata kama haitaweza badilisha matokeo mwaka 2010.

Hebu fafanua hii 'exchange ya mafisadi na kura yako'
 
aaaagh hizo ni danganya toto za CCM, hakuna kushitakiwa wala hakuna mtu atakayefikishwa mahakamani.
hiyo ishu na nyingine nyiingi zilizotangulia ambazo mpaka sasa watanzania hawajapata mustakabali wake zitapigwa danadana mpaka mtasahau mlipoanzia...
 
watanzania hawajapata mustakabali wake zitapigwa danadana mpaka mtasahau mlipoanzia...

Son, mpaka kieleweke! hasahau mtu kitu this is 2008 and not 1947!...mpaka kieleweke mwanangu tumechoka na usanii. Si unakumbuka JK alisema mwacheni Mzee wetu astaafu kwa amani?...Tukalala naye mbele kumhoji kila kona magazeti kutoa details za ufisadi uliofanywa na mafisadi, mpaka kabadilisha msimamo sasa usemi wake umekufa na Pinda juzi kadai wanafuatilia tuhuma dhidi ya Mkapa. Ballali alitamka sijiuzulu ng'o sasa hivi kaikimbia nchi. Karamagi, Lowassa na Chenge wote hawa wameangushwa kwa nguvu ya umma, taratibu tu tutapambana na ufisadi mpaka tuutokomeze.

Kama anafikiri Watanzania tutasahau basi ameula wa chuya atakuwa Rais wa kwanza Tanzania kukaa madarakani kwa term moja tu.
 
Mimi bado ninayo matumaini na JK pamoja na kwamba kavuruga sehemu nyingi. Kifupi tatizo kubwa la nafasi yake (rais) ni pale anapojiuliza nani msafi?..
Binafsi nipo radhi kumsamehe yeye kwa yote yaliyokwisha tokea in exchange ya Mafisadi na kura yangu ataipata hata kama haitaweza badilisha matokeo mwaka 2010.

Unless huko damu damu inatakiwa utupe siri iliyopelekea kufikia maamuzi makubwa kiasi hiki
 
Unless huko damu damu inatakiwa utupe siri iliyopelekea kufikia maamuzi makubwa kiasi hiki

Ndio maana mimi nikamuomba ufafanuzi maana sioni kwanini JK apewe kura pamoja na kuwa tangu aingie madarakani hadi sasa amevurunda vibaya sana. Kati ya sasa mpaka 2010 kuna kipindi kirefu anaweza kurudisha credibility yake hivyo Watanzania kumwamini tena na hivyo kumpa 'KULA' nyingine.
 
Ndio maana mimi nikamuomba ufafanuzi maana sioni kwanini JK apewe kura pamoja na kuwa tangu aingie madarakani hadi sasa amevurunda vibaya sana. Kati ya sasa mpaka 2010 kuna kipindi kirefu anaweza kurudisha credibility yake hivyo Watanzania kumwamini tena na hivyo kumpa 'KULA' nyingine.

Watanzania tunatakiwa kusimama kidete siyo lazima RAIS akae miaka kumi. baada ya kukaa miaka mitano tunayo haki ya kuhakikisha harudi tena nafikiri JK tumeisha elewa strength yake. Tunahitaji watu wa kutuvusha alipo tufikisha.

Sina uhakika kama kweli anahitaji kipindi kingine nafikiri hata yeye mpaka 2010 atakuwa amechoka sana ataitaji kusaidiwa.
 
JK anakwepa maswali magumu, what a bus****. Hizo safari ni muhimu kuliko kuwaambia waliomchagua uso kwa uso.

Kwanini anaona haya na kutumia vibaraka wake? Je, huko anakokwenda nani analipia safari yake? kweli tumepata mkwere.

Upo wapi ule ujasiri jamani...ujasiri wa watanzania...watu walioandamana maelfu ya kilometa na hadi wengine kupoteza maisha..katika kuunga mkono misimamo ya sirikali..na pia chama tawala..enzi hizo za hayati BABA wa TAIFA..? Ina maana leo tuseme inakuwa ngumu watanzania kutumia ujasiri huu huu kuandamana na kushinikiza mafisadi washghulikiwe ipasavyo..? Ni sisi tunaolipa kodi ndio tunaotoa ridhaa ya hao akina JAaa KAaaYAaaa na wenziwe kuingia ikulu, kutumiapato la nchi tukiwa na lengo la kupata maendeleo, sasa inakuwaje kama wanakiuka makubaliano tusiwachukulie hatua muafaka..haswa nyakati za uchaguzi...?
Jee, mei mosi ikitambulika kama siku ya wavuja jasho, na wachangiaji wa kiasi kikubwa wa shughuli za kiuchumi katika sekta mbali mbali nchini... ni mojawapo ya matukio muhimu nchini yanayoelekea kupoteza umuhimu wake?..mie simo..
 
Naam hakuna popote palipoandikwa kwamba Rais wa Tanzania ni lazima akae madarakani miaka 10. Kama miaka yake mitano ya kwanza kazi imemshinda basi Watanzania wanastahili kabisa kupata Rais mpya.
 
Naam hakuna popote palipoandikwa kwamba Rais wa Tanzania ni lazima akae madarakani miaka 10. Kama miaka yake mitano ya kwanza kazi imemshinda basi Watanzania wanastahili kabisa kupata Rais mpya.

na hata hiyo mitano yenyewe sio lazima, kama mtu unaakili timamu na unayaona haya yanayotokea hapa nchini kwa sasa basi unatakiwa kujiuzuru tu.
ila kwa heshima ya viongozi dizaini hii kama atawin 2010 basi unaweza kusikia 2015 anataka katiba irekebishwe ili aendelee...
 
Naam hakuna popote palipoandikwa kwamba Rais wa Tanzania ni lazima akae madarakani miaka 10. Kama miaka yake mitano ya kwanza kazi imemshinda basi Watanzania wanastahili kabisa kupata Rais mpya.

Bubu,
Ndio maana ya kuwa na chaguzi kila miaka mitano, ili wananchi wachague viongozi wengine kama waliopo hawakuwatimizia matakwa yao.

Bahati mbaya tu ni kwamba wananchi hawapewi nafasi na elimu ya kutosha kuonyesha kuwa hawa viongozi hawakutimiza waliyotumwa. Matokeo ya kukosa elimu hii muhimu, ni kuwarudisha viongozi wale wale.
 
Ndio maana mimi nikamuomba ufafanuzi maana sioni kwanini JK apewe kura pamoja na kuwa tangu aingie madarakani hadi sasa amevurunda vibaya sana. Kati ya sasa mpaka 2010 kuna kipindi kirefu anaweza kurudisha credibility yake hivyo Watanzania kumwamini tena na hivyo kumpa 'KULA' nyingine.

huko ni kupoteza muda, kama mtu ulimwamini akaamua kukusaliti unatakiwa umweke mbali zaidi na wewe la sivyo atakufanyia usaliti mbaya zaidi ambao hutaweza ku-recover. Kikwete alimwamini Chenge na alipounda baraza lingine ( pamoja na kulalamikiwa sana na wananchi) alimpa second chance, look what shame has he coursed him!!!!!!!!!!
 
kutokana na ahadi nyingi sana alizozitoa JK na kushindwa kutimiza hata thumuni ya hizo, huyu mtu tayari ameonyesha kushindwa kuwaondoa mafisadi na ufisadi wao.

sio kama hataki, lakini labda hana uwezo wa kiakili, au kibidii, au kimoyo wa kukaa mbali na mafisadi.

kwa hivi kashfa zinavyoibuka siku hadi siku, basi hata yeye mwenyewe kikwete anaweza kugutuka kuwa hana cha kuwaeleza wananchi mwaka 2010, na akajitoa.
 
Lakini jamani, JK amechanganyikiwa,wale waliomsuport sasa wamemsaliti, sijui afanye nini ili kujinusuru na balaa hili linaloandama uongozi wake
 
Hivi mapambano haya ni ya JK au ni wananchi. Ni mapema mno kumhusisha JK ktk hili kabla hajawafikisha watuhumiwa mahakamani
 
Back
Top Bottom