Vigogo halmashauri ya Siha wadaiwa “kutafuna “mil 140 ,wadaiwa kuigeuza halmashuri shamba la Bibi.

Nashukuru Mungu Sijaona Mchaga hata mmoja lakini utasikia kuna matackle matacle wanaosema sijui Wachaga ni Wezi sijui wapigaji na wakati wote nawaona ni watu wa Kanda nyonyo waliowekwa na Mtakatifu Mwendazake

By the way niko hapa njia panda nmetokea Daslam na Familia napata KITIMOTO na Masanga nikazikusanye Tena hizi ngonjera za Kibaguzi Tupa Kule
Chamecha meku
 
Mwandishi kashindwa kueleza kiundani hizo milioni 140 zimetoka wapi? Yaani hiyo jumla kaipataje?

Hizo POS huwa zinazingua kama ilivyo mifumo mingine ya kompyuta. Sasa kusema tu kwamba walisingizia mashine mbovu wakati uhalisia ni kwamba kuna wakati POS huzingua, siyo sawa.

Halafu haingii akilini kusema hela zimepigwa bila kutaja na kueleza kwa kina zimepigwa katika chanzo kipi maana Halmashauri huwa na vyanzo vingi na kila chanzo kina makisio/ lengo la makusanyo kwa siku, mwezi, na mwaka.

Sasa hiyo milioni 140 ilikuwa makusanyo ya wapi na siku ngapi? Na wakusanya ushuru ni wangapi? Na yupi pesa yake ilichotwa na kivipi? Kazi ya IT ilikuwaje na alihisikaje?

Halafu ni kawaida sana wakusanya ushuru kusainishwa mikataba, na pia ni kawaida sana kwa wakusanya ushuru kukusanya mapato na kuyakabidhi kwa mhasibu na kisha mhasibu kuzipeleka benki. Sijaona kosa hapo japo Halmashauri nyingine wakusanya ushuru hupeleka pesa benki moja kwa moja.

Hii habari imekaa kiumbea umbea sana
Wewe ni mke wa mmoja wao hao wezi?
 
Vigogo halmashauri ya Siha wadaiwa kuchota milioni 140 fedha za makusanyo ya ndani.

*Wadaiwa kuigeuza halmashauri “shamba la bibi “

*Yumo mwanasheria,mhasibu,mkaguzi wa fedha za ndani pamoja na mtaalamu wa mfumo wa mashine za kukusanya mapato .

Na,Mwandishi Maalumu

SIRI mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi zinazoiandama halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro zimezidi kuwekwa hadharani ambapo aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Ndaki Muhuli ametajwa kuchota zaidi ya kiasi cha sh,140 million.

Ndaki ambaye alihamishwa na kupelekwa halmashauri ya Kakonko mkoani Kigoma katika mabadaliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ametajwa kuchota fedha hizo kati ya mwezi Agosti mwaka jana fedha ambazo zimetajwa zilikuwa ni za makusanyo ya ndani.

Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa muda mfupi baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Valerian Juwal pamoja na aliyekuwa mweka hazina,Frank Maleto aliletwa Ndaki ambapo alianza kusuka mipango ya ulaji wa fedha hizo kwa kushirikiana na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo,Onesmo Buswelu aliyehamishiwa wilaya mpya ya Tanganyika .

Vyanzo vya uhakika vimeeleza kwamba Ndaki aliandaa mikataba mbalimbali kwa wakusanya mapato wanaotumia mfumo wa POSS ambapo inaelezwa fedha zote za mapato zilizokuwa zikikusanywa zilikabidhiwa kwa Mhasibu aliyetambulika kwa jina moja la Mudi.

“Ndaki alimpanga mhasibu aitwae Mudi kusimamia mapato na akaandaa mikataba kwa wakusanya mapato wamkabidhi yeye fedha zote taslimu badala ya kuzipeleka benki “kilisema chanzo cha habari

Taarifa hizo zilienda mbali zaidi na kueleza kuwa cha ajabu hata mikataba iliyoandaliwa kwa wakusanya mapato haikuwahi kuwasilishwa kwa wakuu wa idara (CMT) wala mbele ya kamati ya fedha bali iliandaliwa na mwanasheria aliyetajwa kwa jina moja la SASSI.

“Fedha nyingi zilichotwa ndani ya mwezi Agosti mwaka jana na hata kabla ya Ndaki kuhamishiwa Kakonko alikomba hela nyingi tu alafu akawaelekeza wakusanya mapato waripoti kwamba mashine ni mbovu “kilifafanua chanzo cha habari

Taarifa za ndani zinadai tayari mhasibu (Mudi)amekiri baada ya kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya uchunguzi kuwa Ndaki alichota fedha hizo kwa kushirikiana na katibu tawala (Mabiti) sanjari na Buswelu ambapo amefichua kuwa fedha nyingi ilipelekwa kuwekezwa kwenye kilimo cha ngano na shamba la miti la West Kilimanjaro.

Baadhi waliotajwa kushiriki kunufaika na uchotaji huo wa fedha ni pamoja na mtaalamu wa mifumo ya mashine za mapato aitwae JOEL sanjari na aliyekuwa kaimu mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo ,Frank Mbaga.

“ndugu mwandishi hawa watu watatu Buswelu,Ndaki na Mabiti waliunda utatu mtakatifu kwa kuwa wote wanatokea sehemu moja hivyo walikuwa wakijichotea wanavyotaka na kiufupi waliigeuza hii halmashauri kama shamba la bibi “kilisema chanzo cha habari

Baadhi ya watuhumiwa katika kashfa hiyo wametafutwa kwa nyakati tofauti ili kujibu tuhuma hizo lakini hawajawa tayari kujibu lolote juhudi za
kundelea kuwatafuta bado zinaendelea.

Itaendelea..........

Pichani chini ni viongozi waliodaiwa kuunda utatu mtakatifu halmashauri ya Siha,wa kwanza ni aliyekuwa mkurugenzi (Ndaki Muhuli),aliiyekuwa Mkuu wa wilaya (Onesmo Buswelu) pamoja na katibu tawala (Joseph Mabiiti)

View attachment 2054210

View attachment 2054211

View attachment 2054212
Sukuma gang again
 
Mwendazake aliipanga safu ya wasukuma kila sehemu...hivi mnadhani kwa ukabila aliokuwa nao mwendazake wale wahanga wa ajira msiokuwa wasukuma mnahisi mungetoboa??,,...sidhani ngoma ya suma lee😁😁
 
waziri2020 unawaitaje wenzako mafisadi huku unasema tuache vyombo vya Usalama vifanye kazi? Unajua kabisa usemacho hakina ukweli siyo?

Acheni kuwachafua maafisa wa Serikali kwa ghiliba.
 
Nashukuru Mungu Sijaona Mchaga hata mmoja lakini utasikia kuna matackle matacle wanaosema sijui Wachaga ni Wezi sijui wapigaji na wakati wote nawaona ni watu wa Kanda nyonyo waliowekwa na Mtakatifu Mwendazake

By the way niko hapa njia panda nmetokea Daslam na Familia napata KITIMOTO na Masanga nikazikusanye Tena hizi ngonjera za Kibaguzi Tupa Kule
Wape salamu hapo kwa mromboo.....
 
Umekaa upande gani hapa njia panda😅😅
 
Mwandishi kashindwa kueleza kiundani hizo milioni 140 zimetoka wapi? Yaani hiyo jumla kaipataje?

Hizo POS huwa zinazingua kama ilivyo mifumo mingine ya kompyuta. Sasa kusema tu kwamba walisingizia mashine mbovu wakati uhalisia ni kwamba kuna wakati POS huzingua, siyo sawa.

Halafu haingii akilini kusema hela zimepigwa bila kutaja na kueleza kwa kina zimepigwa katika chanzo kipi maana Halmashauri huwa na vyanzo vingi na kila chanzo kina makisio/ lengo la makusanyo kwa siku, mwezi, na mwaka.

Sasa hiyo milioni 140 ilikuwa makusanyo ya wapi na siku ngapi? Na wakusanya ushuru ni wangapi? Na yupi pesa yake ilichotwa na kivipi? Kazi ya IT ilikuwaje na alihisikaje?

Halafu ni kawaida sana wakusanya ushuru kusainishwa mikataba, na pia ni kawaida sana kwa wakusanya ushuru kukusanya mapato na kuyakabidhi kwa mhasibu na kisha mhasibu kuzipeleka benki. Sijaona kosa hapo japo Halmashauri nyingine wakusanya ushuru hupeleka pesa benki moja kwa moja.

Hii habari imekaa kiumbea umbea sana
Yawezekana nawe pia ni mnufaika
 
TUKISEMA TUWE NA KATIBA MPYA YENYE KANUNI MPYA ZA UTUMISHI WA UMMA, KUSHUGHULIKA NA WAHUJUMU UCHUMI, NK.
UNAONA TATIZO NI GAIDI MBOWE NA CHADEMA SIO?
 
Back
Top Bottom