Vigogo Dodoma wanaswa kwa tuhuma za ufisadi ................................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Vigogo Dodoma wanaswa kwa tuhuma za ufisadi Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 21:19 0diggsdigg

Habel Chidawali, Dodoma
JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, akiwemo mwenyekiti aliyemaliza muda wake, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mwenyekiti huyo ni Godwin Mkanwa ambaye anashikiliwa pamoja na mhandisi wa wilaya, Slyvester Kayunga pamoja na mkurugenzi wa wilaya hiyo, Robert Kitimbo ambaye alihojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Zelothe Stephen alikiri taarifa za kukamatwa kwa watu hao, lakini akasema kuwa suala hilo bado ni la ndani na hivyo asingeweza kulizungumzia kwa kuwa upepelezi wa kina bado unaendelea na unaweza kuhusisha na watu zaidi.

Sababu za kukamatwa kwa watu hao zimeelezwa kuwa ni kutokana na upotevu wa mamilioni ya fedha ambayo yalitokana na manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa Daraja la Godegode lililo wilayani Mpwapwa ambalo ujenzi wake unaonekana kuwa wa kiwango cha chini.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa sakata hilo lilianza tangu Jumamosi iliyopita wakati mhandisi huyo pamoja na maafisa wengine walitiwa mbaroni na kuhojiwa na baadaye mwenyekiti kukamatwa juzi.
"Ni kweli suala hilo lipo na tunawashikilia watu kadhaa ambao ni viongozi, lakini siwezi kusema kwa kuwa bado tunafanya uchunguzi wa kina zaidi... nitawaambia wala msiwe na shaka ndugu zangu maana mambo kama haya ukianza kusema kuna nini au nini kinaendelea unaweza kukuta umevujisha siri kubwa,"alisema Zelothe.

Habari zaidi zinadai kuwa kwa pamoja viongozi hao walishiriki katika kupitisha tenda ya ujenzi wa daraja hilo ambalo lilipangwa kujengwa kwa Sh500 milioni.

Mei 19 mwaka huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa walifika kwenye daraja hilo lililo katikati ya Kijiji cha Godegode na Kimagai na ambalo linaunganaisha Jimbo la Kibakwe na wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, kwa lengo la kujionea hali halisi ya ujenzi wake.
Akiwa katika eneo hilo, Waziri Pinda alisema ujenzi wa daraja hilo ulipaswa kusimaiwa na wakandarasi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na akataka ujenzi wake ukamilike ndani ya miezi miwili huku akiahidi kurejea eneo hilo.

Hata hivyo, Pinda alionyesha wasiwasi wake kwa mhandisi tangu siku hiyo baada ya kujikanyaga katika maelezo yake ya mbinu atakazotumia katika kufanikisha ujenzi huo.
"Wewe mhandisi mbona una wasiwasi au hujiamini katika kazi yako... wewe kweli ni mhandisi," Pinda alimuuliza mhandisi huyo.
"Lakini hili daraja msipoangalia, litawatokea puani maana hatuna mchezo katika fedha za walipa kodi."
Kauli ya Pinda siku hiyo ilipozwa na Dk Kawambwa ambaye alionekana kumtetea mhandisi huyo na kumsaidia katika kutoa ufafanuzi juu ya namna watakavyojenga daraja hilo.
"Hawa jamaa wametafuna fedha nyingi sana... sakata hili lilianza mara baada ya mhandisi kutoka Jeshi la Wananchi kufika katika eneo hili kulikagua na kubaini kuwa daraja hili ni hatari sana kwa kuwa limejengwa chini ya kiwango," alisema mtoaji habari wetu.

Kwa mujibu wa mmoja wa maafisa wa polisi mkoani hapa ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwa madai si msemaji, kilichowaponza viongozi hao ni kitendo cha kupitisha zabuni bila ya kufuata taratibu za manunuzi pamoja na kumtumia mkandarasi ambaye hakuwa na sifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom