Vigogo Dar wajiingiza orodha ya waathirika wa mafuriko... viwanja!

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,945
2,275
Vigogo wa jiji la Dar wamelazimisha majina yao kuingizwa kwenye list ya waathirika wa mafuriko ili wawemo kwenye mgao wa viwanja 2000 watakavyopatiwa wahanga hao. Hao ndio viongozi tulionao matatizo yetu kwao neema. source mtanzania la leo
 
Viongozi wa serikali wapo kwaajili ya matumbo yao na wala si kwaajili ya kutumikia wananchi, so kila dili lolote litakalo tokea lazima wao wawe wa kwanza kunufaika. Nawapongeza CDM misaada waliyotowa waliwapa waathirika moja kwa moja.
 
Ili kuwe na uwazi inabidi majina ya walioathirika na kugawiwa viwanja yawekwe hadharani. vinginevyo kweli tutakuta waathirika wa narudi jangwani na viwanja vya mabwe pande wanapewa vigogo. Tumeyaona haya kumbuka miaka ya 90 waathirika wa Jangwani waliambiwa wanapewa viwanja kinyerezi lakini waliovipata ni wachache vingine vikaenda kwa vigogo! Nchi hii bwana kila kitu deal!
 
Viongozi wa serikali wapo kwaajili ya matumbo yao na wala si kwaajili ya kutumikia wananchi, so kila dili lolote litakalo tokea lazima wao wawe wa kwanza kunufaika. Nawapongeza CDM misaada waliyotowa waliwapa waathirika moja kwa moja.

Ndugu zangu tutaishia kulalamika tu juu ya viongozi wetu,mbona hatuchukui hatua? Inayotakiwa kutumika kwa sasa ni nguvu na si siasa tena kwani ni wazi kuwa siasa zimeshindwa kutatua udhaifu wa viongozi wetu.
 
Kama kweli hili limefanyika hii ni kufuru na uchokozi dhidi ya amani (....) tuliyonayo. Fikiria kwamba waliokuwa wapangaji maeneo yaliyoathirika wameambiwa wajitafutie pa kupanga na kwamba serikali haishughuliki na wapangaji ila wenye nyumba!

Hebu fikiria bila wenye nyumba kuwa na nyumba hapo hao wapangaji wangeathirika vipi? ikizingatiwa kwamba zoezi zima kwa mpango fulani serikali inahusika kwa kutochukua hatua mapema na badala yake kujikita kwenye siasa badala hali halisi.
 
Naipenda sana serikali yangu ila kuna baadhi ya viongozi wananikatisha tamaa kwelikweli.
 
Nategemea wabunge wa Dsm wakiongozwa na CCM mkoa watawatetea kama ambavyo wamekuwa wanapiga kelele kuhusu kivuko cha Kigamboni!
 
Kama kweli hili limefanyika hii ni kufuru na uchokozi dhidi ya amani (....) tuliyonayo. Fikiria kwamba waliokuwa wapangaji maeneo yaliyoathirika wameambiwa wajitafutie pa kupanga na kwamba serikali haishughuliki na wapangaji ila wenye nyumba!

Hebu fikiria bila wenye nyumba kuwa na nyumba hapo hao wapangaji wangeathirika vipi? ikizingatiwa kwamba zoezi zima kwa mpango fulani serikali inahusika kwa kutochukua hatua mapema na badala yake kujikita kwenye siasa badala hali halisi.

Mimi hili la wapangaji nao kudai viwanja sili support ... Wapewe wenye nyumba tu ... Wapangaji wakatafute mahala pengine "sio bondeni kupanga "
 
Heri yako una nyumba tayari au hela ya kupanga Masaki.Ngoja tuhangaike tu tutapata hela nyingine ya kupanga Kigamboni/Mbagala...
 
Mimi hili la wapangaji nao kudai viwanja sili support ... Wapewe wenye nyumba tu ... Wapangaji wakatafute mahala pengine "sio bondeni kupanga "

Wewe kama sio dalali basi ni bepari mmojawapo mwenye nyumba nyingi hapa dar, hivyo unaogopa kukosa wapangaji. kwanini wasipewe viwanja? kwani wapangaji hawana haki ya kupata viwanja? wakirudi mabonddeni mtawalaumu?
 
Kama kweli hili limefanyika hii ni kufuru na uchokozi dhidi ya amani (....) tuliyonayo. Fikiria kwamba waliokuwa wapangaji maeneo yaliyoathirika wameambiwa wajitafutie pa kupanga na kwamba serikali haishughuliki na wapangaji ila wenye nyumba!

Hebu fikiria bila wenye nyumba kuwa na nyumba hapo hao wapangaji wangeathirika vipi? ikizingatiwa kwamba zoezi zima kwa mpango fulani serikali inahusika kwa kutochukua hatua mapema na badala yake kujikita kwenye siasa badala hali halisi.

"Eti wanaiuliza serikali waende wapi? kwani sisi ndio tuliwapeleka mabondeni?" mh.mkuu wa mkoa.
 
Nasikitika JF inapoteza credibility ma thread kibao, wachangiaji kibao, hoja hazina mshiko ni udaku...taja jina hapa kigogo fulani wa serikali ameingizwa kwenye orodha ya waathirika...otherwise unatupotezea muda wa kujadili mambo ya maana ya nchi
 
Gazeti la mtanzania ni gazeti majeruhi la Rostam Aziz na Hussein Bashe tuwe makini kulifanya chanzo chetu makini cha taarifa. magazeti majeruhi wakati mwingine yanaumba taarifa bandia ili kukidhi haja ya kuwasafisha majeruhi wa kisiasa au kututoa kwenye agenda za msingi za kujadili madhambi ya waliohujumu uchumi wetu na kutufikisha hapa tulipo.
 
hao vigogo wametajwa majina? je, hawana majina? kama hawajatajwa basi habari hii bado ni tetesi, umbea au kutaka kutuchanganya tu.
 
Back
Top Bottom