Vigogo bodi ya kahawa Tanzania waibua njia mpya za ulaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo bodi ya kahawa Tanzania waibua njia mpya za ulaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by matengo, Dec 26, 2011.

 1. m

  matengo Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika jitihada za kujinasua na tuhuma mbali mbali zinazomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu sasa kupitia mtandao amefanikiwa kujisajili mtandao wa Recruitment Africa kuhudhulia Africa India Pertnership summit iliyofanyika Mauritius tarehe 14 Desemba ili apewe zawadi bandia ya kumuonyesha kuwa ni kiongozi bora. Vigezo vinavyotumika ni kuandika maneno yasiyozidi 2500 pamoja na viambatanisho, maelezo ya Taasisi n.k.

  Kwa kutumia pesa za umma akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha walienda Mauritius na kupokea hiyo zawadi ya utawala bora ambayo haitokani na utendaji halisi bali utaalamu wa kupangilia maneno aliyoyaandika mwenyewe au kuandikiwa. Picha inayomuonyesha akipokea hiyo zawadi ameibandika katika website ya Bodi ya kahawa.

  Wanajamii forum wenzangu ebu angalia viongozi wabovu wanavyotumia kila njia kurubuni serikali ili isiwachukulie hatua hata baada ya ushahidi wa Tume iliyotumwa Bodi ya kahawa kuwachunguza kudhibitisha kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa matumizi mabaya ya madaraka unaendelea ndani ya Bodi ya kahawa.
   
Loading...