Vigogo bodi ya kahawa moshi wachunguzwa kwa ufisadi

matengo

Member
Jun 1, 2011
30
4
[h=3]VIGOGO BODI YA KAHAWA MOSHI WACHUNGUZWA KWA UFISADI[/h]

JENGO LA MAKAO MAKUU YA BODI YA KAHAWA KAMA LINAVYOONEKANA.

Na Charles Ndagulla,Moshi.

VIGOGO watatu wa bodi ya kahawa nchini(TCB) yenye makao yake makuu mjini moshi akiwamo Mkurugenzi mwendeshaji wa bodi hiyo,Injinia Adolph Kumburu,wanachunguzwa na serikali wakituhumiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kufuja mamilioni ya fedha .

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa,Tume hiyo inawajumuisha maofisa kutoka Ikulu,Bodi ya zabuni ya taifa,Wizara ya Kilimo,chakula na ushirika pamoja na Tume ya utumishi wa umma .

Tume hiyo inachunguza mambo 11 ikiwamo utoaji wa zabuni bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma ambako mkurugenzi huyo na wasaidizi wake wanatuhumiwa kutoa zabuni kinyemela kwa baadhi ya makampuni bila kushindani makampuni mengine.

Tuhuma nyingine zinazomkabili mkurugenzi huyo na wasaidizi wake ni kutumia vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha dola 105,000 kwa ajili ya safari ya 'kutalii ' nchini Vietnam na China julai 12 hadi 31 mwaka jana ambako wajumbe wanane wa bodi hiyo na maofisa wawili walisafiri.

Inadaiwa kuwa, fedha hizo ziliidhinishwa na Mkurugenzi huyo na wasaidiazi wake bila kibali kutoka chombo kilicho juu ya bodi hiyo ambacho ni wizara ya Kilimo,chakula na Ushirika.

Tume hiyo ambayo ipo kwa zaidi ya siku tano sasa hapa mjini Moshi,tayari imeshawahoji Mkurugenzi anayeshughulikia ubora wa kahawa ndani ya bodi hiyo ,Primus Kimario,meneja wa fedha na ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa fedha(DF),Asteri Bitegeko na Mkurugenzi wao Injilia Adolph Kumburu.

Vigogo hao watatu ambao ndiyo waidhinishaji wakuu wa fedha(watia saini),wanatuhumiwa kutoa kandarasi ya kutathimini mali za bodi hiyo kwa kampuni moja ya mkoani Tabora yenye thamani ya sh,Milioni 60 bila kushindanisha makampuni mengine.

Pia wanatuhumiwa kuipa kandarasi kampuni moja ya Star Fish ya Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa taarifa za bei ya kahawa kwa wakulima kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu za kiganjani(SMS) kandarasi ya dola za kimarekani 15,000 kwa mwaka zaidi ya sh,Milioni 24 za Tanzania bila kushindanisha kampuni nyingine.

Hata hivyo pamoja na kukiri kuwepo na uchunguzi huo,Mkurugenzi wa bodi hiyo,Injinia Kumburu,amedai hiyo si tume bali ni kamati aliyodai ipo hapa mjini moshi kwa ajli ya ukaguzi wa kawaida japo hakuwa tayari kungia kwa undani ni mambo yapi kamati hiyo inachunguza.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jumanne wiki hii,Kumburu hakuwa tayari kujibu tuhuma dhidi yake ambazo ni miongoni mwa mambo yanayochunguzwa na tume hiyo kwa kile alichodai kufanya hivyo ni kuingilia kazi ya tume.

Tuhuma nyingine zinazochunguzwa na tume hiyo ni kuwepo na watumishi wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi mishahara ambayo ni nje ya ile iliyoidhinishwa na hazina huku bodi hiyo ikituhumiwa kuwa na vikao vingi vyenye lengo la kulipana posho vikao ambavyo vinadaiwa havina tija kwa bodi.

Inadaiwa kuwa,tangu januari mwaka huu hadi sasa bodi hiyo imeendesha vikao sita na kila kikao inadaiwa hutumia kiasi cha sh,Milioni 20 ambapo mwenyekiti wa bodi hulipwa sh,350,000 kwa kikao kimoja,mkurugenzi ambaye ni katibu wa bodi na wejumbe wengine hulipwa sh,300,000 kila mmoja.

Mkurugenzi huyo pia hakukiri wala kukanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake kuwa amekuwa akisafiri mara kwa mara hata safari ambazo hazina umhimu huku akidaiwa pia kuunda kanda nje ya kanunni za bodi hiyo za mwaka 2003.

Kwa mujibu wa habari za uchunguzi,mkurugenzi huyo ameanzisha kanda tatu za Tarime,Kigoma na Ruvuma nje ya kanuni za bodi huku akidaiwa kutenga Milioni 20 kila mwaka kwa kila kanda ingawa zipo taarifa kwamba fedha hizo huishia njiani.

MWISHO.

Sawa sawa hivi ndo tunataka, Hii tabia ipo hadi kwa wenyeviti wa vitongoji ya kujilia fedha zetu. Wananchi tunatakiwa kuhoji na kuwakaba koo mpaka pale watu watakapoacha kukimbilia uongozi kwa manufaa yao. Watu wanajimegea tenda wao kwa wao, which is a crazy game, tena mhandisi ndo kinara.
 
Hongera Serikali kwa kuchukua hatua. Pamoja na hayo ichunguzwe pia Kampuni inayofanya usafi Bodi ya kahawa kutoka Morogoro ina uhusihano na Mkurugenzi wa fedha aliyetokea Morogoro alikokuwa akifanya kazi NSSF. Hata hii Kampuni ya Tabora iliyopewa kazi ya kutathmini mali za shirika ana ndugu zake humo.
Kuhusu safari za wakurugenzi wa Bodi kupelekwa kutalii Vietnam na China hiyo ni mbinu ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa ya kutaka asihojiwe katika kufuja kwake fedha za umma. Fedha za umma anahakikisha hazitumii kulingana na bajeti iliyopitishwa na Serikali ili zibaki awe na pesa za kutosha kutumia mwenyewe au kuonga aendelee kuendesha shirika kama mali yake.
 
Hongera Serikali kwa kuchukua hatua. Pamoja na hayo ichunguzwe pia na Kampuni inayofanya ulinzi Bodi ya kahawa kutoka Morogoro ambayo inasemekana ina mahusihano na Mkurugenzi wa fedha (Bw. Astery Bitegeko) aliyetokea Morogoro alikokuwa akifanya kazi NSSF. Hata hii Kampuni ya Tabora iliyopewa kazi ya kutathmini mali za shirika ana ndugu zake humo. Kuhusu safari za Wajumbe wa Bodi kupelekwa kutalii Vietnam na China hiyo ni mbinu ya Injinia Kumburu kuwarubuni ma Boss wake hao wasimhoji kwa kuendesha Shirika la Umma bila ya kufuata sheria kanuni na taratibu na kufuja kwake fedha za umma. Fedha za umma anahakikisha anazibana zisitumike kulingana na bajeti iliyopitishwa na Serikali ili zibaki awe na pesa za kutosha kutumia kupitia njia ambazo zina maslahi kwake yeye binafsi, maswahiba wake au kuonga aendelee kuendesha shirika kama mali yake.
 
3.2.2 Hati Miliki ya Jengo la Kahawa House inashikiliwa na Exim Benki
Kahawa House ni Jengo la Bodi ya Kahawa Tanzania linalotumika kama makao
makuu ya bodi hiyo lililoko mjini Moshi. Ukaguzi umebaini kuwa hati ya jengo
hilo inashikiliwa na Exim Benki kama dhamana ya mkopo wenye shaka
uliosainiwa tarehe 6 Machi 2003.
Kwa taarifa ni kwamba, Mzabuni M/s Africa Consulting Group Ltd alishinda
zabuni ya kusambaza madawa ya kahawa mnamo mwaka 2003. Hata hivyo,
mzabuni huyo hakuwa na fedha kwa ajili ya kununua madawa na hivyo ili
mlazimu kwenda Exim Benk kutaka kukopa dola za Kimarekani millioni mia tatu
(300) kwa ajili ya biashara hiyo. Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa fedha
walitoa hati ya jengo kama dhamana. Hata hivyo, Bodi ilikataa kuidhinisha
dhamana hiyo. Mzabuni alishindwa kurejesha fedha hizo na Exim Benki
wameshikilia hati za jengo hilo na iko katika mchakato wa kuuza jengo hilo
ambalo lina thamani ya billioni nne (4) kw ajili ya kulipa deni hilo.
Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha kulazimisha kumdhamini
mzabuni mfanya biashara kinyume na maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi
kinaashiria rushwa na ufisadi wa hali ya juu endapo kama jengo husika kweli
litanadiwa.
http://nao.go.tz/?wpfb_dl=23

Vigogo kutoa ushahidi kesi ya Bodi ya Kahawa Send to a friend
Wednesday, 29 June 2011 21:04
digg
Mwandishi Wetu,Moshi
MASHAHIDI 26 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) watatoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa zamani wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).

Vigogo hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Leslie Omari na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha, Shaddy Kyambile ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorororo.

Miongoni mwa mashahidi hao ni Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa TCB, Adolf Kumburu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi hiyo wakati kosa hilo likitendeka,Profesa Husein Mongi.

Mashahidi wengine katika orodha hiyo ni Balozi Ernes Mulokozi ambaye naye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwanasheria Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk Audax Rutabanzibwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara, Geofrey Kirenga na waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi waliotajwa kuwa ni Edwin Mtey, Philip Mbogella na Michael Ngaleku Shirima.

Orodha hiyo ya mashahidi ilitolewa mahakamani mjini Moshi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Kilimanjaro, Simon Kobelo na wanasheria wawili wa Takukuru, Maghella Ndimbo na Jacopyo Richard.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali yaliyosomwa mahakamani,Takukuru ilifichua kuwa mshtakiwa wa kwanza, Omari pia alikuwa mwenye hisa nyingi katika kampuni binafsi ya African Consulting Group Limited.

Katika kipindi ambacho mshtakiwa huyo wa kwanza akiwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, hakuwahi kuiambia Bodi ya Wakurugenzi juu ya uhusiano wake na kampuni hiyo binafsi wala kutangaza kuwa na maslahi nayo.

Februari 8, 2003, bila kuwa na kibali cha bodi ya wakurugenzi ya TCB, washtakiwa waliingia mkataba na kampuni hiyo ili kuiwekea dhamana na kuiwezesha kukopa Sh330 milioni kutoka Benki ya Exim Bank(T) Ltd.

Fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kununulia pembejeo za kahawa na kukikopesha Chama Kikuu cha Ushirika cha Mbozi ingawa wakati huo TCB tayari ilikuwa imejiondoa katika usambazaji pembejeo tangu mwaka 1999.

Baadaye washtakiwa hao wakaweka kama dhamana hati ya umiliki wa kiwanja lilipo jengo la Makao Makuu ya TCB kwa ajili ya deni hilo la kampuni binafsi ambayo baadaye ilishindwa kulipa deni hilo.

Hali hiyo ilisababisha Benki ya Exim (T) Limited kutaka kuliuza jengo hilo baada ya deni na riba kufikia zaidi ya Sh700 milioni na imeilazimu TCB kutumia Sh50milioni kwa ajili ya kuzuia jengo hilo lisiuzwe kwa mnada.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Julai 4 mwaka huu na washtakiwa wanatetewa na Godwin Sandi anayemtetea mshtakiwa wa pili (Kyambile) na Eliakunda Kipoko anayemtetea mshtakiwa wa pili, (Omary) wapo nje kwa dhamana.
Vigogo kutoa ushahidi kesi ya Bodi ya Kahawa

[h=1]Mbunge CCM apinga uteuzi wa JK[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 13 June 2012

MBUNGE wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi amepinga uteuzi wa mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete.
Amepinga pia uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na kile alichoita "utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu."
Februari mwaka huu, rais alimteua Dk. Eve Hawa Sinare kuwa mwenyekiti wa TCB; hatua iliyofuatiwa na waziri wa kilimo (wakati huo Prof. Jumanne Maghembe) kuteua wajumbe wa bodi.
Hivi sasa Prof. Jumanne Maghembe ni waziri wa maji.
Katika barua ambayo Zambi amemwandikia Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza, ambayo MwanaHALISI imeona, mbunge huyo anachambua mjumbe mmoja baada ya mwingine na kusema hawakupatikana kwa uwiano wa kikanda.
Zambi anasema katika barua yake kwamba Dk. Sinare "hafai kuwa mwenyekiti wa bodi" kutokana na kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi.
"Naomba ieleweke kwamba, Dk. Eve Hawa Sinare, mwanasheria wa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys, ndiye alipewa kazi na Benki ya NMB kwa ajili ya kulipiga mnada jengo la Kahawa Moshi (ofisi kuu ya TCB). Hadi sasa jengo hilo lina mgogoro," anaeleza Zambi.
Anasema, "…inashangaza kumteua mtu ambaye amepewa kazi ya kulipiga mnada jengo hilo…kuwa mwenyekiti. Atakwepaje mgongano wa kimaslahi?"
Zambi anasema ana uhakika Rais Kikwete "amedanganywa" kuhusu mteuliwa wake. Anasema Dk. Sinare hawezi kutetea maendeleo ya Bodi kama mwenyekiti; na wakati huohuo kusimamia uuzwaji wa jengo ambamo ndipo zilipo ofisi kuu za TCB.
Anamshauri waziri Chiza amshauri rais kutengua uteuzi wa Dk. Sinare ili kuitendea haki bodi ya wakurugenzi; na menejimenti ya Bodi ya Kahawa iweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
Barua ya Zambi ya 4 Juni 2012, imenakiliwa kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Wajumbe wa bodi ambao kuteuliwa kwao kumepingwa na Zambi, ni pamoja na mhandisi mstaafu wa maji, Miraji Omari Msuya.
Zambi anasema uteuzi wa Msuya haukuzingatia sheria kwa sababu hajulikani anawakilisha kundi gani.
Mjumbe mwingine ni mwanasheria na mwenyekiti wa kampuni ya Lima anayosema inahusika na ununuzi wa kahawa, Eric Ng'maryo.
Anadai vyama ambavyo vinatambuliwa na vinaweza kuwakilishwa kwenye bodi ni Tanzania Coffee Association na Association of Coffee Growers, lakini siyo Lima anakotoka Ng'maryo.
Zambi ameituhumu pia Lima "kushawishi wakulima kuuza kahawa mbichi (mbivu) au red cherry kwa bei ndogo sana."
Kuhusu Prof. James Teri, ambaye ni mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kahawa (TaCRI), Zambi anasema "Taasisi yake siyo ya serikali na hivyo kumteua mtendaji wake mkuu kwenye bodi kama mwakilishi wa serikali, si sahihi hata kidogo…"
"Mheshimiwa waziri, sababu nyingine kubwa ya kupinga uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Kahawa ni kutozingatia uteuzi wa wajumbe kwa kuzingatia maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa nchini," anaandika Zambi katika barua ya kurasa nane.
Anataja kanda ya Kaskazini, yenye mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga; Mbinga (mkoani Ruvuma), Mbeya, Kagera, Kigoma na Tarime (mkoani Mara), kuwa ndiyo maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa.
Analalamika kuwa Mbeya ambako inalimwa kahawa nyingi, hawakupata mwakilishi kwenye bodi.
Anasema, "…inashangaza sana kuona kwamba kati ya wateuliwa wote kumi (10) kwenye Bodi, watano (5) wanatoka mkoa mmoja wa Kilimanjaro…"
Tuhuma za upendeleo kwa misingi ya ukanda, ziliwahi kutolewa mwaka jana wakati wa mkutano wa bajeti.
Zilikuwa zikilenga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo. Alikuwa akidaiwa kuwa chanzo cha watu kutoka sehemu moja kujazana idara ya wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Ezekiel Maige.
Kabla ya kwenda ikulu kuwa katibu mkuu kiongozi, Luhanjo alikuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Alihamia huko akitokea Wizara ya Maliasili na Utalii anakodaiwa alishawishi uteuzi wa watendaji kwa misingi ya ukabila katika Idara ya Wanyamapori.
Aidha, kanuni mpya za zao la kahawa ambazo Zambi anadai kupinga ni zile zilizojadiliwa kwenye mkutano wa wadau wa kahawa tarehe 24 na 25 Mei mwaka huu, mjini Morogoro.
Zambi anadai mkutano wa Morogoro uliambiwa kuwa kanuni mpya tayari zimesainiwa na waziri husika tangu 18 Aprili mwaka huu.
"Mheshimiwa waziri, napenda ufahamu kuwa kanuni hizo zimwetungwa kinyemela kwa sababu wadau wa kahawa hawakushirikishwa kabisa," anaeleza Zambi.
Anadai kuwa kikao cha TCB mjini Moshi mwaka 2011, ambacho inadaiwa ndiko zilitungiwa kanuni, hakikuwa na ajenda hiyo na kwamba yeye mwenyewe alikuwepo.
Anasema, hata hivyo, kikao hicho hakikuwa cha wadau kwani kilikuwa cha wajumbe 30 tu. Amemweleza waziri kuwa kikao cha wadau kina wajumbe zaidi ya 200.
Zambi anasema hajaona kanuni hizo lakini anadai "…zitakuwa kanuni mbaya. Kanuni ambazo hazina faida kwa mfanyabiashara."
Akiandika kwa niaba ya "Wanambeya (wakulina wa kahawa)," anasema wana imani na waziri.
"Tunatumaini masuala haya mawili mazito sana, moja uteuzi wa wajumbe wa bodi bila kufauta sheria na utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu, utayafanyia kazi kama ambavyo nimeshauri," anahitimisha barua yake.
Gazeti toleo lenye makala hii
WAFUATAO WANATAFUTIWA MAKOSA ILI WAFUKUZWE KAZI BODI YA KAHAWA.

Wafuatao wanatafutiwa au kuundiwa makosa ili wafukuzwe kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania yenye makao yake makuu Moshi.

1. Kilian Massawe - Huyu alishafukuzwa kazi mapema kabisa KOSA LAKE inasemekana lilikuwa kutokurudisha masurufu ya safari,2.Kuchakachua mishahara ya wafanya kazi wakati akiwa Mkurugenzi wa fedha. Kesi yake inaendelea mahakamani mjini Moshi.

2. Leopard Taso Mukebezi – KOSA LAKE – 1.Alihoji kwa nini fedha zinahamishwa toka kwenye matawi ya Tanga na Dar wakati matawi hayo yanajitegemea. 2. Kujihusisha na michezo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania halafu anaacha kufanya kazi za shirika.

4. Desdery Mboya – KOSA LA 1.Alimshauri Mkurugenzi Mkuu kuwa asitoe waraka wa kuuza kahawa za wakulima bila kujali reserve zao Mkurugenzi Mkuu akakataa akalazimisha ziuzwe matokeo yake zilipata bei ya chini sana na wakulima walikataa kuachia kahawa zao na ndipo ikabidi ziuzwe upya kwenye mnada uliofuata. Moto huo ulikuwa mkali sana kati ya wakulima na Bodi ya kahawa. Kumburu akapeleka swala hilo kwenye bodi ya wakurugenzi na Mwenyekiti ambaye ni Bw Pius Ngeze wa kikao hicho aliwaambia wakurugenzi kuwa makosa hayo yalifanywa na Muuzaji mkuu wa kahawa na kusababisha bw Kumburu kukatisha safari yake nchi za nje UK. Akaamuru aliyefanya makosa hayo Bw Mboya apewe barua ya onyo kali.Bw Mboya ambaye pia alikuwa kwenye kikao hicho akasimama na kuelezea wajumbe wa bodi kuwa huo ulikuwa uongo mtupu na kwamba Bw Kumburu hakuwepo safarini alikuwa ofisini na ndiye aliyeandika waraka huo. Mwenyekiti akaikaushia na kwenda kwenye hoja nyingine haraka. Kosa lake la 2. Ni kongea ukweli kwenye vikao kuhusu maswala yahusuyo masoko ya kahawa ndani na nje ya nchi pia alishawahi kukaimu mkurugenzi wa masoko kwa miaka kama nane hivi na kabla mkurugenzi mkuu Bw L.D.Omar Kusitaafu alikuwa anamwachia ofisi kukaimu kwa muda mrefu.Pia kwa sasa anaonekana kuwa tishio kwa mkurugenzi wa masoko wa sasa bw Primus Kimaryo ambaye ni swahiba mkubwa sana wa bw Kumburu kwa kuwa walitokea wote Kilicafe.Alisha jengewa mazingira ya kuitwa mwizi kutokana na mashine ya kukaanga kahawa iliyokuwa imeazimwa na kampuni ya kuuza kahawa ya DORMAN akituhumiwa kuwa alikuwa amewauzia kinyemela huku mashine hiyo ilikuwa imeazimwa kwa DORMA kwa kibali cha mkurugenzi mkuu wakati huo bw Omar. Cha kushangaza ni kwamba kwenye mafaili yote copy ya barua hiyo hakukutwa lakini kwa kuwa Mungu anajua kulinda watu wake Bw Mboya alikuwa na copy yake na ndicho kilichomsaidia.Sasa hivi anahusishwa na kutoa kahawa malipo yakaenda kwa kikundi kingine kimakosa ingawa waliopelekewa fedha hizo wameshakiri kimaandishi kuwa walipokea na wamekubali kuzirudisha.

4. Goodluck Sipira – Mwonekano wake (Personality), kwa umma na Elimu ya juu (M.Sc ukilinganisha na B.SC aliyo nayo Mkurugenzi Mkuu) inampa tabu sana pamoja na kumweleza ukweli bila kumwogopa ndio kunakomponza mpaka kufikia kutaka kumtimua. Alishamsingizia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kudai kuwa Sipira ndio kikwazo cha kukataa kutoa leseni za Cherry kumbe sio kweli ni yeye Kumburu ndio alimwambia asizitoe.

5. Kaberwa Rutachweka – KOSA LAKE LA 1.Huyu bwana alipogundua kuwa mshahara wake umechakachuliwa alipohoji ndio ikawa kosa lake ingawa alirudishiwa mshahara wake halali ulioidhinishwa na wizara kuanzia hapo ndio ikawa kosa lake. KOSA LAKE LINGINE NI Kuongea ukweli kwa mambo yanayoendelea bodi. Amekuwa akibadilishiwa vyeo ambavyo havieleweki ni msomi mzuri sana na masters 2 za kilimo.
Kosa ni kuandika barua ya kutaka kujua wadhifa na wajibu wake ndani ya Bodi baada ya kuhamishiwa Makao makuu akitokea Bukoba ambako alikuwa ameajiriwa kama Reginal Manager na kuteremshwa cheo kinyemela bila ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi Kosa la 3 ni kuulizia sababu za kubaguliwa kimaslahi kwa kulipwa posho ya mafuta tofauti na cheo kilichoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi.Baada ya Mkurugenzi mkuu kuona wanamnyima haki ndipo akarubuni Bodi ya Wakurugenzi wakaidhinisha hicho cheo kwa kuback date ili aendelee kumnyima haki Bw. Rutachweka.

6. Melikiadi Massawe - Mahusiano yake na wizara kutokana na kukahimu nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Kahawa kwa miaka 6 ndio kosa lake kubwa, na utumiaji wa gari nzuri ndio vilivyompelekea kutafutiwa visa ili amfukuze kazi. Bw kumburu alipoona hampati akaamua kumhamishia Tarime tawi ambalo kisheria na kikanuni halipo na ukizingatia uzalishaji wa kahawa kwenye wilaya hii ni mdogo sana kiasi cha tani 1200 kwa mwaka ili aache kazi mwenyewe.Sasa hivi amewekea mtu wa kumchunguza ambaye ni dereva wake na hivi sasa yuko hatiani kutiwa hatiani.

7. Alex Peter
Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye fukuzwa kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.

8. Edwin Hamaro
Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye mfukuza kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.

9. Rogatus Meela – KOSA LAKE LA KWANZA NI – Inasemakana ana Mahusiano na Kampuni kubwa ya ununuzi wa kahawa ya Rogers and Mann kampuni ambayo ilipeleka ushindani mkubwa wa kununua kahawa wilayani Tarime na kusababisha wakulima wa kahawa wilayani humo kufaidika sana mpaka hivi leo ndio iliyompelekea bwana huyu kutafutiwa visa vya kutaka kufukuzwa kazi kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa kwa muda mrefu ikituhumiwa na washindani waliokuwa wilayani huko kwa muda mrefu kudai kuwa kampuni hiyo inaharibu utaratibu wa ununuzi wa kahawa wilayani kitu ambacho sio cha kweli.. Pia kiongozi wa idara aliyokuwepo ya masoko Kimaryo alishawahi kusikika kua hataweza kuiiongoza idara hiyo kama huyu bw ataendelea kuwepo kwa kuwa hatawaliki Baada ya kusingiziwa vitu vya uongo vingi alihamishiwa idara ya Masoko na kupelekwa idara ya operation na hapohapo kuhamishiwa mkoani Kigoma na kupewa cheo cha Kukaimu afisa uendelezaji wa zao la kahawa mkoa wa Kigoma mkoa ambao uzalishaji wake wa kahawa kwa mwaka ni tani 1200 kama Tarime. Uhamisho wake mpaka leo haujaeleweka maana haukupitishwa kwenye menejiment ya shirika.Hayo yote ni ili aache kazi mwenyewe Inasemakana sasa bado anawindwa vibaya sana.

10. Elia Mkwawa
Uzoefu kazini unampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve inabidi amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi.Kama ni makosa hata Mkurgenzi anatakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.

11. Elias Temu
Uzoefu kazini pamoja na kuwa kiongozi wa wafanyakazi ambapo amekuwa akimwambia Bw. Kumburu ukweli ndivyo vinampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve huyu bwana alionekana kuongelea swala hilo kwa kuhoji inabidi naye amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani na wao wakashindwa kuona hii hitilafu yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi. Hata hivyo hatua zilichukuliwa kurekebisha hitilafu hii Idara ya fedha ikazembea kuchukua hatua. Kama ni makosa ya uwajibikaji hata Bw. Kumburu naye pia angetakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.Usemaji ukweli wake ndio unaomponza kwa kuwaeleza ukweli wawapo vikaoni ila inasemakana hatima yake iko karibusana

12. Frank Mrema
Alituhumiwa kwa kosa la kuambiwa na kukubali kumpa mkubwa wake wa kazi bwana Daudi Kiangi LPO ili aijaze ( Bw. Kiangi ni mjumbe wa Menejimenti na ndiye alikuwa na details za hiyo LPO). Huyu naye alikuwa karibu na Mkurugenzi wa fedha aliyemfukuza.Na pia kwenda kudai malipo ya jingo toka CRDB Bank ya Dola takribani 75,000 sasa sijui ilitakiwa akachukue mwenyewe Kumburu au sijui alitaka kitu gani.

13. Esther Mlay.
Alituhumiwa kwa kosa la kuwalipa wajumbe wa Bodi kwenye hati ambayo wachapaji hawakuandika jina. Hata hivyo malipo yenyewe hakulipa yeye binafsi. Kinachomponza ni kuvuja kwa taarifa za uchakachuaji wa pesa za shirika anatuhumiwa kwamba yeye ndiye anayezivujisha.Hivi sasa yuko hatarini kufukuzwa kazi saa yoyote

Kumekuwa na matukio mengi katika bodi ya wafanyakazi kunyayaswa na kuonewa pale utakapoonekana unaufahamu wa kazi au jambo lolote lile.

Wafanyakazi hata wakifanya kosa kidogo yeye hajui taratibu anachojua yeye ni kufukuza na alishasikika akisema hata wakienda mahakamani mpaka hizo kesi ziishe yeye atakuwa ameshaondoka kwenye Bodi hiyo.

Ila anachotaka hasa nikuhakikisha watu aliowakuta bila kujali familia zao au muda wa mtu aliokaa kazini anataka kuwafukuza na kuwaharibia maisha yao bila kujali.(inawezekana sio mwanadamu ni mnyama fulani hivi)

Alipopata cheo hicho wale aliyokuwa akifanya nao kazi huko MCCCo LTD NA Kilicafe walianza kuwaeleza wafanyakazi wa bodi kuwa mmekwisha huku wao wakisherekea kuondoka kwake huko kilicafe

Mara kwa mara ameshasikika akisema yeye haogopi mtu hata waziri kwake hamjali kwa kuwa waziri na yeye wote ni wateuliwa na Raisi.

Akishirikiana na Mwenyekiti walimpa Waziri wa kilimo taarifa za uongo kwenye mkutano wa wadau wa kahawa uliofanyika Mkoani Morogoro mwezi May 2011 na waziri kujikuta akitoa hutuba ambayo baadae ilibidi isitangazwe kwenye vyombo vya habari vyote kwa kuwa ingeweza kumuharibia kazi,na hayo waliyafanya kwa manufaa yao wenyewe na manufaa ya Kilicafe na Techno serve.

Alishawahi kukaa kwenye kikao cha wafanya kazi akasikika akimwambia Mwenye kiti Bw Piusi Ngeze hawa hata siku moja hawaninyimi usingizi analala kwa raha kabisa hata kwa ni wajinga mno.

Kutokana na aliyomfanyia waziri sasa hivi anahaha kutafuta utaratibu wa watu kumwombea msamaha kwa waziri na hivi sasa akijua kuna kikao ambacho waziri atakuwepo anajishauri jinsi kwenda kwenye kikao hicho kule kwenye mkutano Bukoba hakwenda kwa kuwa kulikuwa na maofisa wa wizarani akamtuma DCDO mkutano huo.
SASA UKITENDA SI LAZIMA UTENDWE?

Kama hujawahi kukutana na mtu muongo kwenye maisha toka uzaliwe karibiana na huyu mtu utatapika au utakimbia

Barua alizoandikiwa toka wizarani tunaomba waziri zifanyie kazi vizuri maana zitakuwa na uongo mwingi sana usiamini alichokujibu .
Na pia tunaomba kujua je Mwenyekiti wa bodi Bw Pius Ngeze ni mtendaji mkuu au ni mwenyekiti wa vikao,maana tunashangaa wakati wote yuko Moshi na ofisi amepewa ghorofa ya pili na awapo Moshi hulipwa per diem zake kama kawaida.

Tunamuomba Waziri wa Kilimo, chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe aingilie kati na kurudisha morali ya wafanyakazi wa bodi vinginevyo wafanyakazi wataingia katika mgomo baridi ambao utaathiri sekta ya kahawa nchini.

https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/157578-kulikoni-bodi-ya-kahawa-moshi.html
Chizza atwishwa hatima ya Mkurugenzi Bodi ya Kahawa

na Charles Ndagulla, Moshi

amka2.gif
HATIMA ya ajira ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Injinia Adolph Kumburu ipo mikononi mwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia Christopher Chizza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini hapa, Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TBC, Dk. Eve Hawa Sinare, alisema suala la mkurugenzi huyo sasa litaamuliwa na waziri, huku akiishutumu bodi iliyopita kwa kuleta mgawanyiko mkubwa ambao ulidhoofisha ufanisi wa mamlaka hiyo.
Bodi hiyo iliagiza kurejeshwa kazini mara moja kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji na Maendeleo ya Kahawa, Goodluck Sipira ambaye alisimamishwa kazi tangu Agosti mwaka jana.
Dk. Sinare alisema kuwa kulingana na tathimini iliyofanywa na bodi yake walibaini kuwa taratibu na kanuni za kazi hazikufuatwa katika kumsimamisha kazi Sipira.
Aidha, alisema kuwa, bodi imeagiza kurejeshwa makao makuu mjini hapa Ofisa Maendeleo ya Kahawa, Logath Meela ambaye bodi ya zamani ilimhamishia mkoani Kigoma.
Aliongeza kuwa, Meela ni mtaalamu wa kuonja kahawa na kwamba anarudishwa Moshi kuendelea na kazi yake hiyo.
[h=2]Tuesday, November 8, 2011[/h][h=3]SERIKALI YAPOTEZA ZAIDI YA MILIONI 100 ZA KODI YA KAHAWA MBEYA[/h]

JENGO LA BODI YA KAHAWA TANZANIA LILILOPO MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

VIONGOZI WA BODI YA KAHAWA

* Ni makusudi ya bodi ya kahawa, kuzuia kampuni
* Kampuni 20 zakwepa kodi Mbeya
* Zajiita vikundi ili zisidaiwe

SERIKALI imepoteza mapato zaidi ya Shilingi Milioni 100 kutoka kampuni za ununuzi wa Kahawa mbichi mkoani Mbeya kutokana na bodi ya kuhawa nchini (TCB)kuzuia kwa makusudi baadhi ya makampuni kununua zao hilo, Imebainika.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa baadhi ya vigogo wa wa bodi hiyo akiwemo Mkurugenzi mkuu Adolph Kumburu kwa kushirikiana na Halmashauri zinazolima zao hilo mkoani Mbeya waliamua kuyasimamisha baadhi ya makampuni ikiwemo kampuni ya Lima Limited na kuruhusu kampuni 20 zisizolipa kodi kununua kahawa hiyo mbichi (Chery).

Kusimamishwa kwa makampuni yanayolipa kodi kulifanyika kwa kipindi cha msimu wa mwaka huu 2011 msimu ulioanza April mwaka huu ambapo Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika iliposhitukia mkakati huo hatari ka uchumi wan chi na kuiamuru bodi hiyo kutoa leseni June mwaka huu.

Imebainika kuwa kampuni 20 ambazo ziliruhusiwa kununua kahawa hiyo mbichi zipo wilayani Mbozi ambazo zilinunua kahawa hiyo katika wilaya za Mbozi, Ileje na Mbeya Vijijini.

Kampuni hizo zimejipachika kivuli cha vikundi vya wakulima ambavyo havilipi kodi ingawa vinapata faida na mikopo Benki na kufanya kazi kama za kampuni zinazolipa kodi kisheria.

Kampuni hizo na majina ya viongozi wake kwenye mabano ni Ikonga Farmers Group (Fredy Mgalla), Amne Family Farmer Group (Amos Mwamlima), Peoples Group + GDM Company(Gilbert Mwangoka), Mpito Coffee Group (Adam Kalonge),Uporoto CPU Cofee (Japhet Ganda), Lungwa Coffee Growers(Richard Mwashitete) na Mbozi Highland Coffee Farmers(Kandona Chisunga/Kollin Mahenge.

Zingine ni Ifumbo Coffee Group (Burton Sinyenga),Igunda Mboreshaji miche ya Kahawa(Anthon Mtambo), Umoja wa wakulima Itaka(kasimbilo),Uhuru Coffee Farmers Group(Mwashambwa Kenard), Wailolela Coffee Group Clement Mkondya), Vilisyala Coffee Group(Shula Sande) na Shilenama Coffee Group (Mishack Mpogolo).

Kampuni zingine sita zinazojiita vikundi ni hegi(Aswile Mwashala), Igamba Mpya(Lute Mkisi), Zelezeta Farmers Group(Lyanda Hezron Mwamukinga), Cjamila Group(Shukrani Mtete, Kivuli Coffee Group (Mussa Msyete) na Man Company inayoongozwa na Manfred Kapusi.

Kwa mujibu wa taarifa, ni kwamba msingi wa bodi ya kahawa kukubali kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na zao hilo ni kuwawezesha wakulima kukusanyiwa kahawa zao ili kupeleka kwenye makampuni yanayonunua zao hilo lakini badala ya kufanya hivyo makampuni hayo yasiyo na usajili ili kukwepa kodi yananunua kahawa mbichi na kavu na kuipeleka katika soko la ndani Mjini Moshi.

Ili kuhalalisha mfumo huo wa ukwepaji kodi, wamilii na vigogo wa makampuni hayo (Vikundi), wameunda mtandao wa vikundi vya vya wakulima wilayani Mbozi unaojulikana kama MVIKAMBO unaoongozwa na Fredy Mgalla kwa lengo la kuwa na sauti ya pamoja na kuendelea kukwepa kulipa kodi Serikalini kupitia mwamvuli huo kuwa ni wakulima na wala si wafanyabiashara.

Kwa upande wake bodi ya kahawa kwa makusudi ama kwa bahati mbaya ili kuhalalisha ukwepaji kodi huo na kuikosesha Serikali mapato, iliipiga marufuku kampuni ya Lima inayolipa kodi kutokana na manunuzi ya kahawa hiyo zaidi ya Shilingi M,ilioni 20 kwa mwaka.

Baadhi ya barua na nyaraka zingine zilizopatikana na Mtanzania Jumapili kuzinasa, zinaonesha kuwa kampuni hiyo haikupaswa kununua kahawa katika wilaya za Ileje, Mbozi, Mbinga, Mbeya Vijijini na Rungwe jibu lililopatikana mwezi Juni mwaka huu wakati kampuni husika iliomba leseni hiyo mwezi wa tano baada ya kuona inazuiliwa na Halmashauri husika wakati tangu mwaka 2003 ilikuwa ikinunua.

Barua moja wapo iliyonaswa ni ile iliyokuwa imeandikwa na bodi hiyo Juni 3 mwaka huu ambayo inaeleza kuwa haina mamlaka ya kutoa leseni za kununua kahawa hiyo mbichi na kupelekwa nakala yake kwa katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Katibu tawala wa mkoa wa Mbeya, Katibu tawala mkoa wa Ruvuma.

Baada ya barua hiyo kuwafikia viongozi hao, imeelezwa kuwa Wizara ikagundua udhaifu uliokuwepo katika ukiritimba wa bodi hiyo na kuona jinsi Serikali itakavyopoteza mapato yake, ndipo ikaiamuru bodi hiyo kufuta barua yake ya awali ambapo bodi hiyo kupitia Mkurugenzi Mkuu Adolph Kumburu.

Kumburu aliifuta barua yake ya kwanza yenye kumbukumbu namba OP-PCB/LIMA 3'd June,2011 kwa kuandika barua ya Juni 4 mwaka huu yenye kumbukumbu No. OP-PGB/LIMA 4[SUP]th[/SUP] June, 2011.

Kwa aibu bodi hiyo ikaamua kutoa leseni tano kwa kampuni ya Lima Limited tarehe hiyo hiyo Juni 4 mwaka huu ambazo zitaishia April 30, 2012 leseni ambazo zilisainiwa June 6 mwaka huu.

Leseni hizo ni zenye namba TCB/CB/11/002 inayoruhusu kununua kahawa michi na kavu wilayani Rungwe, TCB/CB/001 Wilayani Ileje, TCB/CB/11/003 Wilayani Mbozi, TCB/CB/11/004 Wilayani Mbeya Vijijini na leseni No. TCB/CB/11/005 inayoruhusu kununua kahawa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati tayari msimu ukiwa umebakia miezi miwili tu.

Meneja wa Kampuni ya Lima Tinson Nzunda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni alisema kuwa kampuni yake imeingia hasara pamoja na kutoweza kufikia malengo ya kulipa kodi Serikalini hivyo itafanya kila iwezalo ili kuwafikisha wale wote kwenye vyombo vya Sheria ili waweze kufidia hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 110.

Nzunda alisema kampuni hiyo yenye wafanyakazi zaidi ya 104 na vibarua zaidi ya 1000 inatarajia kupunguza wafanyakazi hao na vibarua hao wamekosa ajira ambazo walikuwa wakitegemea kwa muda wote huo.

Aidha hivi karibuni yaliwahi kujitokeza malumbano juu ya suala hilo la ununuzi wa kahawa hiyo mbichi wilayani Mbozi mbele ya Naibu Waziri wa kilimo Chakula na Ushirika Injinia Christopher Chiza ambaye hata hivyo hakuweza kutoa maamuzi baada ya kubaini kuwa kila upande wa wafanyabiashara hao yaani Mvikambo na kampuni ya Lima kila mmoja kuvutia maslahi kwake.

3.2.2 Hati Miliki ya Jengo la Kahawa House inashikiliwa na Exim Benki
Kahawa House ni Jengo la Bodi ya Kahawa Tanzania linalotumika kama makao
makuu ya bodi hiyo lililoko mjini Moshi. Ukaguzi umebaini kuwa hati ya jengo
hilo inashikiliwa na Exim Benki kama dhamana ya mkopo wenye shaka
uliosainiwa tarehe 6 Machi 2003.
Kwa taarifa ni kwamba, Mzabuni M/s Africa Consulting Group Ltd alishinda
zabuni ya kusambaza madawa ya kahawa mnamo mwaka 2003. Hata hivyo,
mzabuni huyo hakuwa na fedha kwa ajili ya kununua madawa na hivyo ili
mlazimu kwenda Exim Benk kutaka kukopa dola za Kimarekani millioni mia tatu
(300) kwa ajili ya biashara hiyo. Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa fedha
walitoa hati ya jengo kama dhamana. Hata hivyo, Bodi ilikataa kuidhinisha
dhamana hiyo. Mzabuni alishindwa kurejesha fedha hizo na Exim Benki
wameshikilia hati za jengo hilo na iko katika mchakato wa kuuza jengo hilo
ambalo lina thamani ya billioni nne (4) kw ajili ya kulipa deni hilo.
Kitendo cha Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha kulazimisha kumdhamini
mzabuni mfanya biashara kinyume na maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi
kinaashiria rushwa na ufisadi wa hali ya juu endapo kama jengo husika kweli
litanadiwa.
http://nao.go.tz/?wpfb_dl=23

Vigogo kutoa ushahidi kesi ya Bodi ya Kahawa Send to a friend
Wednesday, 29 June 2011 21:04
digg
Mwandishi Wetu,Moshi
MASHAHIDI 26 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) watatoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa zamani wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).

Vigogo hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Leslie Omari na aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha, Shaddy Kyambile ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorororo.

Miongoni mwa mashahidi hao ni Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa TCB, Adolf Kumburu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi hiyo wakati kosa hilo likitendeka,Profesa Husein Mongi.

Mashahidi wengine katika orodha hiyo ni Balozi Ernes Mulokozi ambaye naye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwanasheria Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk Audax Rutabanzibwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara, Geofrey Kirenga na waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi waliotajwa kuwa ni Edwin Mtey, Philip Mbogella na Michael Ngaleku Shirima.

Orodha hiyo ya mashahidi ilitolewa mahakamani mjini Moshi jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Kilimanjaro, Simon Kobelo na wanasheria wawili wa Takukuru, Maghella Ndimbo na Jacopyo Richard.

Kwa mujibu wa maelezo ya awali yaliyosomwa mahakamani,Takukuru ilifichua kuwa mshtakiwa wa kwanza, Omari pia alikuwa mwenye hisa nyingi katika kampuni binafsi ya African Consulting Group Limited.

Katika kipindi ambacho mshtakiwa huyo wa kwanza akiwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, hakuwahi kuiambia Bodi ya Wakurugenzi juu ya uhusiano wake na kampuni hiyo binafsi wala kutangaza kuwa na maslahi nayo.

Februari 8, 2003, bila kuwa na kibali cha bodi ya wakurugenzi ya TCB, washtakiwa waliingia mkataba na kampuni hiyo ili kuiwekea dhamana na kuiwezesha kukopa Sh330 milioni kutoka Benki ya Exim Bank(T) Ltd.

Fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kununulia pembejeo za kahawa na kukikopesha Chama Kikuu cha Ushirika cha Mbozi ingawa wakati huo TCB tayari ilikuwa imejiondoa katika usambazaji pembejeo tangu mwaka 1999.

Baadaye washtakiwa hao wakaweka kama dhamana hati ya umiliki wa kiwanja lilipo jengo la Makao Makuu ya TCB kwa ajili ya deni hilo la kampuni binafsi ambayo baadaye ilishindwa kulipa deni hilo.

Hali hiyo ilisababisha Benki ya Exim (T) Limited kutaka kuliuza jengo hilo baada ya deni na riba kufikia zaidi ya Sh700 milioni na imeilazimu TCB kutumia Sh50milioni kwa ajili ya kuzuia jengo hilo lisiuzwe kwa mnada.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Julai 4 mwaka huu na washtakiwa wanatetewa na Godwin Sandi anayemtetea mshtakiwa wa pili (Kyambile) na Eliakunda Kipoko anayemtetea mshtakiwa wa pili, (Omary) wapo nje kwa dhamana.
Vigogo kutoa ushahidi kesi ya Bodi ya Kahawa

[h=1]Mbunge CCM apinga uteuzi wa JK[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 13 June 2012

MBUNGE wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi amepinga uteuzi wa mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete.
Amepinga pia uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na kile alichoita “utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu.”
Februari mwaka huu, rais alimteua Dk. Eve Hawa Sinare kuwa mwenyekiti wa TCB; hatua iliyofuatiwa na waziri wa kilimo (wakati huo Prof. Jumanne Maghembe) kuteua wajumbe wa bodi.
Hivi sasa Prof. Jumanne Maghembe ni waziri wa maji.
Katika barua ambayo Zambi amemwandikia Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza, ambayo MwanaHALISI imeona, mbunge huyo anachambua mjumbe mmoja baada ya mwingine na kusema hawakupatikana kwa uwiano wa kikanda.
Zambi anasema katika barua yake kwamba Dk. Sinare “hafai kuwa mwenyekiti wa bodi” kutokana na kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi.
“Naomba ieleweke kwamba, Dk. Eve Hawa Sinare, mwanasheria wa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys, ndiye alipewa kazi na Benki ya NMB kwa ajili ya kulipiga mnada jengo la Kahawa Moshi (ofisi kuu ya TCB). Hadi sasa jengo hilo lina mgogoro,” anaeleza Zambi.
Anasema, “…inashangaza kumteua mtu ambaye amepewa kazi ya kulipiga mnada jengo hilo…kuwa mwenyekiti. Atakwepaje mgongano wa kimaslahi?”
Zambi anasema ana uhakika Rais Kikwete “amedanganywa” kuhusu mteuliwa wake. Anasema Dk. Sinare hawezi kutetea maendeleo ya Bodi kama mwenyekiti; na wakati huohuo kusimamia uuzwaji wa jengo ambamo ndipo zilipo ofisi kuu za TCB.
Anamshauri waziri Chiza amshauri rais kutengua uteuzi wa Dk. Sinare ili kuitendea haki bodi ya wakurugenzi; na menejimenti ya Bodi ya Kahawa iweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.
Barua ya Zambi ya 4 Juni 2012, imenakiliwa kwa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Wajumbe wa bodi ambao kuteuliwa kwao kumepingwa na Zambi, ni pamoja na mhandisi mstaafu wa maji, Miraji Omari Msuya.
Zambi anasema uteuzi wa Msuya haukuzingatia sheria kwa sababu hajulikani anawakilisha kundi gani.
Mjumbe mwingine ni mwanasheria na mwenyekiti wa kampuni ya Lima anayosema inahusika na ununuzi wa kahawa, Eric Ng’maryo.
Anadai vyama ambavyo vinatambuliwa na vinaweza kuwakilishwa kwenye bodi ni Tanzania Coffee Association na Association of Coffee Growers, lakini siyo Lima anakotoka Ng’maryo.
Zambi ameituhumu pia Lima “kushawishi wakulima kuuza kahawa mbichi (mbivu) au red cherry kwa bei ndogo sana.”
Kuhusu Prof. James Teri, ambaye ni mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kahawa (TaCRI), Zambi anasema “Taasisi yake siyo ya serikali na hivyo kumteua mtendaji wake mkuu kwenye bodi kama mwakilishi wa serikali, si sahihi hata kidogo…”
“Mheshimiwa waziri, sababu nyingine kubwa ya kupinga uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Kahawa ni kutozingatia uteuzi wa wajumbe kwa kuzingatia maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa nchini,” anaandika Zambi katika barua ya kurasa nane.
Anataja kanda ya Kaskazini, yenye mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga; Mbinga (mkoani Ruvuma), Mbeya, Kagera, Kigoma na Tarime (mkoani Mara), kuwa ndiyo maeneo makubwa ya uzalishaji kahawa.
Analalamika kuwa Mbeya ambako inalimwa kahawa nyingi, hawakupata mwakilishi kwenye bodi.
Anasema, “…inashangaza sana kuona kwamba kati ya wateuliwa wote kumi (10) kwenye Bodi, watano (5) wanatoka mkoa mmoja wa Kilimanjaro…”
Tuhuma za upendeleo kwa misingi ya ukanda, ziliwahi kutolewa mwaka jana wakati wa mkutano wa bajeti.
Zilikuwa zikilenga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo. Alikuwa akidaiwa kuwa chanzo cha watu kutoka sehemu moja kujazana idara ya wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Ezekiel Maige.
Kabla ya kwenda ikulu kuwa katibu mkuu kiongozi, Luhanjo alikuwa Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Alihamia huko akitokea Wizara ya Maliasili na Utalii anakodaiwa alishawishi uteuzi wa watendaji kwa misingi ya ukabila katika Idara ya Wanyamapori.
Aidha, kanuni mpya za zao la kahawa ambazo Zambi anadai kupinga ni zile zilizojadiliwa kwenye mkutano wa wadau wa kahawa tarehe 24 na 25 Mei mwaka huu, mjini Morogoro.
Zambi anadai mkutano wa Morogoro uliambiwa kuwa kanuni mpya tayari zimesainiwa na waziri husika tangu 18 Aprili mwaka huu.
“Mheshimiwa waziri, napenda ufahamu kuwa kanuni hizo zimwetungwa kinyemela kwa sababu wadau wa kahawa hawakushirikishwa kabisa,” anaeleza Zambi.
Anadai kuwa kikao cha TCB mjini Moshi mwaka 2011, ambacho inadaiwa ndiko zilitungiwa kanuni, hakikuwa na ajenda hiyo na kwamba yeye mwenyewe alikuwepo.
Anasema, hata hivyo, kikao hicho hakikuwa cha wadau kwani kilikuwa cha wajumbe 30 tu. Amemweleza waziri kuwa kikao cha wadau kina wajumbe zaidi ya 200.
Zambi anasema hajaona kanuni hizo lakini anadai “…zitakuwa kanuni mbaya. Kanuni ambazo hazina faida kwa mfanyabiashara.”
Akiandika kwa niaba ya “Wanambeya (wakulina wa kahawa),” anasema wana imani na waziri.
“Tunatumaini masuala haya mawili mazito sana, moja uteuzi wa wajumbe wa bodi bila kufauta sheria na utungwaji kanuni za zao la kahawa bila kufuata taratibu, utayafanyia kazi kama ambavyo nimeshauri,” anahitimisha barua yake.
Gazeti toleo lenye makala hii
WAFUATAO WANATAFUTIWA MAKOSA ILI WAFUKUZWE KAZI BODI YA KAHAWA.

Wafuatao wanatafutiwa au kuundiwa makosa ili wafukuzwe kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania yenye makao yake makuu Moshi.

1. Kilian Massawe - Huyu alishafukuzwa kazi mapema kabisa KOSA LAKE inasemekana lilikuwa kutokurudisha masurufu ya safari,2.Kuchakachua mishahara ya wafanya kazi wakati akiwa Mkurugenzi wa fedha. Kesi yake inaendelea mahakamani mjini Moshi.

2. Leopard Taso Mukebezi – KOSA LAKE – 1.Alihoji kwa nini fedha zinahamishwa toka kwenye matawi ya Tanga na Dar wakati matawi hayo yanajitegemea. 2. Kujihusisha na michezo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania halafu anaacha kufanya kazi za shirika.

4. Desdery Mboya – KOSA LA 1.Alimshauri Mkurugenzi Mkuu kuwa asitoe waraka wa kuuza kahawa za wakulima bila kujali reserve zao Mkurugenzi Mkuu akakataa akalazimisha ziuzwe matokeo yake zilipata bei ya chini sana na wakulima walikataa kuachia kahawa zao na ndipo ikabidi ziuzwe upya kwenye mnada uliofuata. Moto huo ulikuwa mkali sana kati ya wakulima na Bodi ya kahawa. Kumburu akapeleka swala hilo kwenye bodi ya wakurugenzi na Mwenyekiti ambaye ni Bw Pius Ngeze wa kikao hicho aliwaambia wakurugenzi kuwa makosa hayo yalifanywa na Muuzaji mkuu wa kahawa na kusababisha bw Kumburu kukatisha safari yake nchi za nje UK. Akaamuru aliyefanya makosa hayo Bw Mboya apewe barua ya onyo kali.Bw Mboya ambaye pia alikuwa kwenye kikao hicho akasimama na kuelezea wajumbe wa bodi kuwa huo ulikuwa uongo mtupu na kwamba Bw Kumburu hakuwepo safarini alikuwa ofisini na ndiye aliyeandika waraka huo. Mwenyekiti akaikaushia na kwenda kwenye hoja nyingine haraka. Kosa lake la 2. Ni kongea ukweli kwenye vikao kuhusu maswala yahusuyo masoko ya kahawa ndani na nje ya nchi pia alishawahi kukaimu mkurugenzi wa masoko kwa miaka kama nane hivi na kabla mkurugenzi mkuu Bw L.D.Omar Kusitaafu alikuwa anamwachia ofisi kukaimu kwa muda mrefu.Pia kwa sasa anaonekana kuwa tishio kwa mkurugenzi wa masoko wa sasa bw Primus Kimaryo ambaye ni swahiba mkubwa sana wa bw Kumburu kwa kuwa walitokea wote Kilicafe.Alisha jengewa mazingira ya kuitwa mwizi kutokana na mashine ya kukaanga kahawa iliyokuwa imeazimwa na kampuni ya kuuza kahawa ya DORMAN akituhumiwa kuwa alikuwa amewauzia kinyemela huku mashine hiyo ilikuwa imeazimwa kwa DORMA kwa kibali cha mkurugenzi mkuu wakati huo bw Omar. Cha kushangaza ni kwamba kwenye mafaili yote copy ya barua hiyo hakukutwa lakini kwa kuwa Mungu anajua kulinda watu wake Bw Mboya alikuwa na copy yake na ndicho kilichomsaidia.Sasa hivi anahusishwa na kutoa kahawa malipo yakaenda kwa kikundi kingine kimakosa ingawa waliopelekewa fedha hizo wameshakiri kimaandishi kuwa walipokea na wamekubali kuzirudisha.

4. Goodluck Sipira – Mwonekano wake (Personality), kwa umma na Elimu ya juu (M.Sc ukilinganisha na B.SC aliyo nayo Mkurugenzi Mkuu) inampa tabu sana pamoja na kumweleza ukweli bila kumwogopa ndio kunakomponza mpaka kufikia kutaka kumtimua. Alishamsingizia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kudai kuwa Sipira ndio kikwazo cha kukataa kutoa leseni za Cherry kumbe sio kweli ni yeye Kumburu ndio alimwambia asizitoe.

5. Kaberwa Rutachweka – KOSA LAKE LA 1.Huyu bwana alipogundua kuwa mshahara wake umechakachuliwa alipohoji ndio ikawa kosa lake ingawa alirudishiwa mshahara wake halali ulioidhinishwa na wizara kuanzia hapo ndio ikawa kosa lake. KOSA LAKE LINGINE NI Kuongea ukweli kwa mambo yanayoendelea bodi. Amekuwa akibadilishiwa vyeo ambavyo havieleweki ni msomi mzuri sana na masters 2 za kilimo.
Kosa ni kuandika barua ya kutaka kujua wadhifa na wajibu wake ndani ya Bodi baada ya kuhamishiwa Makao makuu akitokea Bukoba ambako alikuwa ameajiriwa kama Reginal Manager na kuteremshwa cheo kinyemela bila ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi Kosa la 3 ni kuulizia sababu za kubaguliwa kimaslahi kwa kulipwa posho ya mafuta tofauti na cheo kilichoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi.Baada ya Mkurugenzi mkuu kuona wanamnyima haki ndipo akarubuni Bodi ya Wakurugenzi wakaidhinisha hicho cheo kwa kuback date ili aendelee kumnyima haki Bw. Rutachweka.

6. Melikiadi Massawe - Mahusiano yake na wizara kutokana na kukahimu nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Kahawa kwa miaka 6 ndio kosa lake kubwa, na utumiaji wa gari nzuri ndio vilivyompelekea kutafutiwa visa ili amfukuze kazi. Bw kumburu alipoona hampati akaamua kumhamishia Tarime tawi ambalo kisheria na kikanuni halipo na ukizingatia uzalishaji wa kahawa kwenye wilaya hii ni mdogo sana kiasi cha tani 1200 kwa mwaka ili aache kazi mwenyewe.Sasa hivi amewekea mtu wa kumchunguza ambaye ni dereva wake na hivi sasa yuko hatiani kutiwa hatiani.

7. Alex Peter
Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye fukuzwa kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.

8. Edwin Hamaro
Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye mfukuza kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.

9. Rogatus Meela – KOSA LAKE LA KWANZA NI – Inasemakana ana Mahusiano na Kampuni kubwa ya ununuzi wa kahawa ya Rogers and Mann kampuni ambayo ilipeleka ushindani mkubwa wa kununua kahawa wilayani Tarime na kusababisha wakulima wa kahawa wilayani humo kufaidika sana mpaka hivi leo ndio iliyompelekea bwana huyu kutafutiwa visa vya kutaka kufukuzwa kazi kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa kwa muda mrefu ikituhumiwa na washindani waliokuwa wilayani huko kwa muda mrefu kudai kuwa kampuni hiyo inaharibu utaratibu wa ununuzi wa kahawa wilayani kitu ambacho sio cha kweli.. Pia kiongozi wa idara aliyokuwepo ya masoko Kimaryo alishawahi kusikika kua hataweza kuiiongoza idara hiyo kama huyu bw ataendelea kuwepo kwa kuwa hatawaliki Baada ya kusingiziwa vitu vya uongo vingi alihamishiwa idara ya Masoko na kupelekwa idara ya operation na hapohapo kuhamishiwa mkoani Kigoma na kupewa cheo cha Kukaimu afisa uendelezaji wa zao la kahawa mkoa wa Kigoma mkoa ambao uzalishaji wake wa kahawa kwa mwaka ni tani 1200 kama Tarime. Uhamisho wake mpaka leo haujaeleweka maana haukupitishwa kwenye menejiment ya shirika.Hayo yote ni ili aache kazi mwenyewe Inasemakana sasa bado anawindwa vibaya sana.

10. Elia Mkwawa
Uzoefu kazini unampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve inabidi amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi.Kama ni makosa hata Mkurgenzi anatakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.

11. Elias Temu
Uzoefu kazini pamoja na kuwa kiongozi wa wafanyakazi ambapo amekuwa akimwambia Bw. Kumburu ukweli ndivyo vinampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve huyu bwana alionekana kuongelea swala hilo kwa kuhoji inabidi naye amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani na wao wakashindwa kuona hii hitilafu yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi. Hata hivyo hatua zilichukuliwa kurekebisha hitilafu hii Idara ya fedha ikazembea kuchukua hatua. Kama ni makosa ya uwajibikaji hata Bw. Kumburu naye pia angetakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.Usemaji ukweli wake ndio unaomponza kwa kuwaeleza ukweli wawapo vikaoni ila inasemakana hatima yake iko karibusana

12. Frank Mrema
Alituhumiwa kwa kosa la kuambiwa na kukubali kumpa mkubwa wake wa kazi bwana Daudi Kiangi LPO ili aijaze ( Bw. Kiangi ni mjumbe wa Menejimenti na ndiye alikuwa na details za hiyo LPO). Huyu naye alikuwa karibu na Mkurugenzi wa fedha aliyemfukuza.Na pia kwenda kudai malipo ya jingo toka CRDB Bank ya Dola takribani 75,000 sasa sijui ilitakiwa akachukue mwenyewe Kumburu au sijui alitaka kitu gani.

13. Esther Mlay.
Alituhumiwa kwa kosa la kuwalipa wajumbe wa Bodi kwenye hati ambayo wachapaji hawakuandika jina. Hata hivyo malipo yenyewe hakulipa yeye binafsi. Kinachomponza ni kuvuja kwa taarifa za uchakachuaji wa pesa za shirika anatuhumiwa kwamba yeye ndiye anayezivujisha.Hivi sasa yuko hatarini kufukuzwa kazi saa yoyote

Kumekuwa na matukio mengi katika bodi ya wafanyakazi kunyayaswa na kuonewa pale utakapoonekana unaufahamu wa kazi au jambo lolote lile.

Wafanyakazi hata wakifanya kosa kidogo yeye hajui taratibu anachojua yeye ni kufukuza na alishasikika akisema hata wakienda mahakamani mpaka hizo kesi ziishe yeye atakuwa ameshaondoka kwenye Bodi hiyo.

Ila anachotaka hasa nikuhakikisha watu aliowakuta bila kujali familia zao au muda wa mtu aliokaa kazini anataka kuwafukuza na kuwaharibia maisha yao bila kujali.(inawezekana sio mwanadamu ni mnyama fulani hivi)

Alipopata cheo hicho wale aliyokuwa akifanya nao kazi huko MCCCo LTD NA Kilicafe walianza kuwaeleza wafanyakazi wa bodi kuwa mmekwisha huku wao wakisherekea kuondoka kwake huko kilicafe

Mara kwa mara ameshasikika akisema yeye haogopi mtu hata waziri kwake hamjali kwa kuwa waziri na yeye wote ni wateuliwa na Raisi.

Akishirikiana na Mwenyekiti walimpa Waziri wa kilimo taarifa za uongo kwenye mkutano wa wadau wa kahawa uliofanyika Mkoani Morogoro mwezi May 2011 na waziri kujikuta akitoa hutuba ambayo baadae ilibidi isitangazwe kwenye vyombo vya habari vyote kwa kuwa ingeweza kumuharibia kazi,na hayo waliyafanya kwa manufaa yao wenyewe na manufaa ya Kilicafe na Techno serve.

Alishawahi kukaa kwenye kikao cha wafanya kazi akasikika akimwambia Mwenye kiti Bw Piusi Ngeze hawa hata siku moja hawaninyimi usingizi analala kwa raha kabisa hata kwa ni wajinga mno.

Kutokana na aliyomfanyia waziri sasa hivi anahaha kutafuta utaratibu wa watu kumwombea msamaha kwa waziri na hivi sasa akijua kuna kikao ambacho waziri atakuwepo anajishauri jinsi kwenda kwenye kikao hicho kule kwenye mkutano Bukoba hakwenda kwa kuwa kulikuwa na maofisa wa wizarani akamtuma DCDO mkutano huo.
SASA UKITENDA SI LAZIMA UTENDWE?

Kama hujawahi kukutana na mtu muongo kwenye maisha toka uzaliwe karibiana na huyu mtu utatapika au utakimbia

Barua alizoandikiwa toka wizarani tunaomba waziri zifanyie kazi vizuri maana zitakuwa na uongo mwingi sana usiamini alichokujibu .
Na pia tunaomba kujua je Mwenyekiti wa bodi Bw Pius Ngeze ni mtendaji mkuu au ni mwenyekiti wa vikao,maana tunashangaa wakati wote yuko Moshi na ofisi amepewa ghorofa ya pili na awapo Moshi hulipwa per diem zake kama kawaida.

Tunamuomba Waziri wa Kilimo, chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe aingilie kati na kurudisha morali ya wafanyakazi wa bodi vinginevyo wafanyakazi wataingia katika mgomo baridi ambao utaathiri sekta ya kahawa nchini.

https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/157578-kulikoni-bodi-ya-kahawa-moshi.html
Chizza atwishwa hatima ya Mkurugenzi Bodi ya Kahawa

na Charles Ndagulla, Moshi

amka2.gif
HATIMA ya ajira ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Injinia Adolph Kumburu ipo mikononi mwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia Christopher Chizza.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini hapa, Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TBC, Dk. Eve Hawa Sinare, alisema suala la mkurugenzi huyo sasa litaamuliwa na waziri, huku akiishutumu bodi iliyopita kwa kuleta mgawanyiko mkubwa ambao ulidhoofisha ufanisi wa mamlaka hiyo.
Bodi hiyo iliagiza kurejeshwa kazini mara moja kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji na Maendeleo ya Kahawa, Goodluck Sipira ambaye alisimamishwa kazi tangu Agosti mwaka jana.
Dk. Sinare alisema kuwa kulingana na tathimini iliyofanywa na bodi yake walibaini kuwa taratibu na kanuni za kazi hazikufuatwa katika kumsimamisha kazi Sipira.
Aidha, alisema kuwa, bodi imeagiza kurejeshwa makao makuu mjini hapa Ofisa Maendeleo ya Kahawa, Logath Meela ambaye bodi ya zamani ilimhamishia mkoani Kigoma.
Aliongeza kuwa, Meela ni mtaalamu wa kuonja kahawa na kwamba anarudishwa Moshi kuendelea na kazi yake hiyo.
[h=2]Tuesday, November 8, 2011[/h][h=3]SERIKALI YAPOTEZA ZAIDI YA MILIONI 100 ZA KODI YA KAHAWA MBEYA[/h]

JENGO LA BODI YA KAHAWA TANZANIA LILILOPO MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

VIONGOZI WA BODI YA KAHAWA

* Ni makusudi ya bodi ya kahawa, kuzuia kampuni
* Kampuni 20 zakwepa kodi Mbeya
* Zajiita vikundi ili zisidaiwe

SERIKALI imepoteza mapato zaidi ya Shilingi Milioni 100 kutoka kampuni za ununuzi wa Kahawa mbichi mkoani Mbeya kutokana na bodi ya kuhawa nchini (TCB)kuzuia kwa makusudi baadhi ya makampuni kununua zao hilo, Imebainika.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa baadhi ya vigogo wa wa bodi hiyo akiwemo Mkurugenzi mkuu Adolph Kumburu kwa kushirikiana na Halmashauri zinazolima zao hilo mkoani Mbeya waliamua kuyasimamisha baadhi ya makampuni ikiwemo kampuni ya Lima Limited na kuruhusu kampuni 20 zisizolipa kodi kununua kahawa hiyo mbichi (Chery).

Kusimamishwa kwa makampuni yanayolipa kodi kulifanyika kwa kipindi cha msimu wa mwaka huu 2011 msimu ulioanza April mwaka huu ambapo Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika iliposhitukia mkakati huo hatari ka uchumi wan chi na kuiamuru bodi hiyo kutoa leseni June mwaka huu.

Imebainika kuwa kampuni 20 ambazo ziliruhusiwa kununua kahawa hiyo mbichi zipo wilayani Mbozi ambazo zilinunua kahawa hiyo katika wilaya za Mbozi, Ileje na Mbeya Vijijini.

Kampuni hizo zimejipachika kivuli cha vikundi vya wakulima ambavyo havilipi kodi ingawa vinapata faida na mikopo Benki na kufanya kazi kama za kampuni zinazolipa kodi kisheria.

Kampuni hizo na majina ya viongozi wake kwenye mabano ni Ikonga Farmers Group (Fredy Mgalla), Amne Family Farmer Group (Amos Mwamlima), Peoples Group + GDM Company(Gilbert Mwangoka), Mpito Coffee Group (Adam Kalonge),Uporoto CPU Cofee (Japhet Ganda), Lungwa Coffee Growers(Richard Mwashitete) na Mbozi Highland Coffee Farmers(Kandona Chisunga/Kollin Mahenge.

Zingine ni Ifumbo Coffee Group (Burton Sinyenga),Igunda Mboreshaji miche ya Kahawa(Anthon Mtambo), Umoja wa wakulima Itaka(kasimbilo),Uhuru Coffee Farmers Group(Mwashambwa Kenard), Wailolela Coffee Group Clement Mkondya), Vilisyala Coffee Group(Shula Sande) na Shilenama Coffee Group (Mishack Mpogolo).

Kampuni zingine sita zinazojiita vikundi ni hegi(Aswile Mwashala), Igamba Mpya(Lute Mkisi), Zelezeta Farmers Group(Lyanda Hezron Mwamukinga), Cjamila Group(Shukrani Mtete, Kivuli Coffee Group (Mussa Msyete) na Man Company inayoongozwa na Manfred Kapusi.

Kwa mujibu wa taarifa, ni kwamba msingi wa bodi ya kahawa kukubali kuwepo kwa vikundi vinavyojihusisha na zao hilo ni kuwawezesha wakulima kukusanyiwa kahawa zao ili kupeleka kwenye makampuni yanayonunua zao hilo lakini badala ya kufanya hivyo makampuni hayo yasiyo na usajili ili kukwepa kodi yananunua kahawa mbichi na kavu na kuipeleka katika soko la ndani Mjini Moshi.

Ili kuhalalisha mfumo huo wa ukwepaji kodi, wamilii na vigogo wa makampuni hayo (Vikundi), wameunda mtandao wa vikundi vya vya wakulima wilayani Mbozi unaojulikana kama MVIKAMBO unaoongozwa na Fredy Mgalla kwa lengo la kuwa na sauti ya pamoja na kuendelea kukwepa kulipa kodi Serikalini kupitia mwamvuli huo kuwa ni wakulima na wala si wafanyabiashara.

Kwa upande wake bodi ya kahawa kwa makusudi ama kwa bahati mbaya ili kuhalalisha ukwepaji kodi huo na kuikosesha Serikali mapato, iliipiga marufuku kampuni ya Lima inayolipa kodi kutokana na manunuzi ya kahawa hiyo zaidi ya Shilingi M,ilioni 20 kwa mwaka.

Baadhi ya barua na nyaraka zingine zilizopatikana na Mtanzania Jumapili kuzinasa, zinaonesha kuwa kampuni hiyo haikupaswa kununua kahawa katika wilaya za Ileje, Mbozi, Mbinga, Mbeya Vijijini na Rungwe jibu lililopatikana mwezi Juni mwaka huu wakati kampuni husika iliomba leseni hiyo mwezi wa tano baada ya kuona inazuiliwa na Halmashauri husika wakati tangu mwaka 2003 ilikuwa ikinunua.

Barua moja wapo iliyonaswa ni ile iliyokuwa imeandikwa na bodi hiyo Juni 3 mwaka huu ambayo inaeleza kuwa haina mamlaka ya kutoa leseni za kununua kahawa hiyo mbichi na kupelekwa nakala yake kwa katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Katibu tawala wa mkoa wa Mbeya, Katibu tawala mkoa wa Ruvuma.

Baada ya barua hiyo kuwafikia viongozi hao, imeelezwa kuwa Wizara ikagundua udhaifu uliokuwepo katika ukiritimba wa bodi hiyo na kuona jinsi Serikali itakavyopoteza mapato yake, ndipo ikaiamuru bodi hiyo kufuta barua yake ya awali ambapo bodi hiyo kupitia Mkurugenzi Mkuu Adolph Kumburu.

Kumburu aliifuta barua yake ya kwanza yenye kumbukumbu namba OP-PCB/LIMA 3’d June,2011 kwa kuandika barua ya Juni 4 mwaka huu yenye kumbukumbu No. OP-PGB/LIMA 4[SUP]th[/SUP] June, 2011.

Kwa aibu bodi hiyo ikaamua kutoa leseni tano kwa kampuni ya Lima Limited tarehe hiyo hiyo Juni 4 mwaka huu ambazo zitaishia April 30, 2012 leseni ambazo zilisainiwa June 6 mwaka huu.

Leseni hizo ni zenye namba TCB/CB/11/002 inayoruhusu kununua kahawa michi na kavu wilayani Rungwe, TCB/CB/001 Wilayani Ileje, TCB/CB/11/003 Wilayani Mbozi, TCB/CB/11/004 Wilayani Mbeya Vijijini na leseni No. TCB/CB/11/005 inayoruhusu kununua kahawa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati tayari msimu ukiwa umebakia miezi miwili tu.

Meneja wa Kampuni ya Lima Tinson Nzunda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni alisema kuwa kampuni yake imeingia hasara pamoja na kutoweza kufikia malengo ya kulipa kodi Serikalini hivyo itafanya kila iwezalo ili kuwafikisha wale wote kwenye vyombo vya Sheria ili waweze kufidia hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 110.

Nzunda alisema kampuni hiyo yenye wafanyakazi zaidi ya 104 na vibarua zaidi ya 1000 inatarajia kupunguza wafanyakazi hao na vibarua hao wamekosa ajira ambazo walikuwa wakitegemea kwa muda wote huo.

Aidha hivi karibuni yaliwahi kujitokeza malumbano juu ya suala hilo la ununuzi wa kahawa hiyo mbichi wilayani Mbozi mbele ya Naibu Waziri wa kilimo Chakula na Ushirika Injinia Christopher Chiza ambaye hata hivyo hakuweza kutoa maamuzi baada ya kubaini kuwa kila upande wa wafanyabiashara hao yaani Mvikambo na kampuni ya Lima kila mmoja kuvutia maslahi kwake.

Uchunguzi umeisha makelele ya Zambi juu ya Mwenyekiti wa Bodi nayo yameisha sasa hali inaendelea kama kawaida
 
hyo bodi ya kahawa wanaionea sana yule aliyetoka kwa tuuma za rushwa bwana kiambile bado kesi yake aijatolewa hukumu alafu yanaibuka haya tena jamani tunaibiwa na watanzania ambao siyo waaminifu, wa hukumiwe
 
VIGOGO BODI YA KAHAWA MOSHI WACHUNGUZWA KWA UFISADI

JENGO LA MAKAO MAKUU YA BODI YA KAHAWA KAMA LINAVYOONEKANA.

Na Charles Ndagulla,Moshi.

VIGOGO watatu wa bodi ya kahawa nchini(TCB) yenye makao yake makuu mjini moshi akiwamo Mkurugenzi mwendeshaji wa bodi hiyo,Injinia Adolph Kumburu,wanachunguzwa na serikali wakituhumiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kufuja mamilioni ya fedha .

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa,Tume hiyo inawajumuisha maofisa kutoka Ikulu,Bodi ya zabuni ya taifa,Wizara ya Kilimo,chakula na ushirika pamoja na Tume ya utumishi wa umma .

Tume hiyo inachunguza mambo 11 ikiwamo utoaji wa zabuni bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma ambako mkurugenzi huyo na wasaidizi wake wanatuhumiwa kutoa zabuni kinyemela kwa baadhi ya makampuni bila kushindani makampuni mengine.

Tuhuma nyingine zinazomkabili mkurugenzi huyo na wasaidizi wake ni kutumia vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha dola 105,000 kwa ajili ya safari ya 'kutalii ' nchini Vietnam na China julai 12 hadi 31 mwaka jana ambako wajumbe wanane wa bodi hiyo na maofisa wawili walisafiri.

Inadaiwa kuwa, fedha hizo ziliidhinishwa na Mkurugenzi huyo na wasaidiazi wake bila kibali kutoka chombo kilicho juu ya bodi hiyo ambacho ni wizara ya Kilimo,chakula na Ushirika.

Tume hiyo ambayo ipo kwa zaidi ya siku tano sasa hapa mjini Moshi,tayari imeshawahoji Mkurugenzi anayeshughulikia ubora wa kahawa ndani ya bodi hiyo ,Primus Kimario,meneja wa fedha na ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa fedha(DF),Asteri Bitegeko na Mkurugenzi wao Injilia Adolph Kumburu.

Vigogo hao watatu ambao ndiyo waidhinishaji wakuu wa fedha(watia saini),wanatuhumiwa kutoa kandarasi ya kutathimini mali za bodi hiyo kwa kampuni moja ya mkoani Tabora yenye thamani ya sh,Milioni 60 bila kushindanisha makampuni mengine.

Pia wanatuhumiwa kuipa kandarasi kampuni moja ya Star Fish ya Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa taarifa za bei ya kahawa kwa wakulima kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu za kiganjani(SMS) kandarasi ya dola za kimarekani 15,000 kwa mwaka zaidi ya sh,Milioni 24 za Tanzania bila kushindanisha kampuni nyingine.

Hata hivyo pamoja na kukiri kuwepo na uchunguzi huo,Mkurugenzi wa bodi hiyo,Injinia Kumburu,amedai hiyo si tume bali ni kamati aliyodai ipo hapa mjini moshi kwa ajli ya ukaguzi wa kawaida japo hakuwa tayari kungia kwa undani ni mambo yapi kamati hiyo inachunguza.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jumanne wiki hii,Kumburu hakuwa tayari kujibu tuhuma dhidi yake ambazo ni miongoni mwa mambo yanayochunguzwa na tume hiyo kwa kile alichodai kufanya hivyo ni kuingilia kazi ya tume.

Tuhuma nyingine zinazochunguzwa na tume hiyo ni kuwepo na watumishi wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi mishahara ambayo ni nje ya ile iliyoidhinishwa na hazina huku bodi hiyo ikituhumiwa kuwa na vikao vingi vyenye lengo la kulipana posho vikao ambavyo vinadaiwa havina tija kwa bodi.

Inadaiwa kuwa,tangu januari mwaka huu hadi sasa bodi hiyo imeendesha vikao sita na kila kikao inadaiwa hutumia kiasi cha sh,Milioni 20 ambapo mwenyekiti wa bodi hulipwa sh,350,000 kwa kikao kimoja,mkurugenzi ambaye ni katibu wa bodi na wejumbe wengine hulipwa sh,300,000 kila mmoja.

Mkurugenzi huyo pia hakukiri wala kukanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake kuwa amekuwa akisafiri mara kwa mara hata safari ambazo hazina umhimu huku akidaiwa pia kuunda kanda nje ya kanunni za bodi hiyo za mwaka 2003.

Kwa mujibu wa habari za uchunguzi,mkurugenzi huyo ameanzisha kanda tatu za Tarime,Kigoma na Ruvuma nje ya kanuni za bodi huku akidaiwa kutenga Milioni 20 kila mwaka kwa kila kanda ingawa zipo taarifa kwamba fedha hizo huishia njiani.

MWISHO.

Nimesoma kwenye magazeti ambapo Katibu Mwenezi wa CCM Moses NNauye akiwataja Mawaziri wa Kilimo kuwa wanatakiwa kujieleza kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao. Katika mambo wanayotakiwa kuyatolea maelezo pia ni pamoja na matokeo ya hii tume ambayo mapendekezo yake wameyakalia. Je nini kimewashawishi kuyakalia?.

Back
Top Bottom