Vigogo 60 serikalini kuhakikiwa mali zao, yumo Samuel Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo 60 serikalini kuhakikiwa mali zao, yumo Samuel Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 15, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TUME ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeanza mchakato wa kuhakiki mali za viongozi wa umma nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza itaanza na vigogo 60 akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Waziri Samia Suluhu Hassan wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano). Wengine ni wakuu wa mikoa na wilaya, Meya wa majiji, madiwani, wabunge na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za Serikali.

  Zoezi la uhakiki wa mali za viongozi hao litaanza Februari 20 hadi Machi mosi mwaka huu ambapo linafanyika baada ya kukamilika kwa zoezi la urejeshaji wa fomu za utajaji mali na madeni kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Serikali. Mbali na Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, wabunge wengine watakahakikiwa mali zao katika awamu hiyo ni John Mnyika(Ubungo), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Jerome Bwanansi (Lulindi), Faith Mitambo (Liwale) na Stella Manyanya (Viti Maalum).

  Katika orodha hiyo yumo pia Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovock Mwananzila, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Didas Masaburi na Meya wa Jiji la Tanga, Guledi Mohamed. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Charles Nyamrunda, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Placidus Luoga na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema kuwa uhakiki huo ni nguzo bora ya kuijenga jamii ya Watanzania, hasa viongozi wa umma katika kuishi kwa kufuata misingi ya uadilifu, iliyowekwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Alisema kwa kuwa idadi ya viongozi ni kubwa na kwamba tume hiyo itaanza na uhakiki wa viongozi 60 wenye nyadhifa mbalimbali.

  “Sisi tunachokiomba kutoka kwao ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wetu wakati wa zoezi zima la uhakiki wa mali zao,” alisema Kaganda. Alisema wananchi wanatakiwa kushirikiana na tume hiyo kutoa taarifa zitakazowasaidia kugundua mali zilizofichwa, ambazo zinadhaniwa kuwa ni za viongozi wa umma wanaoguswa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aliwataka viongozi wanaohakikiwa kutokuwa na hofu kwa kuwa zoezi hilo ni la kawaida.

  “Hawa hawana tuhuma zozote ni utaratibu wa kawaida tu,”alisema. Jaji mstaafu Kaganda aliliambia gazeti hili kuwa si kosa kwa kiongozi yoyote wa Serikali kuwa na mali na kwamba kosa ni mali hizo kupatikana kinyume na sheria. “Mbunge akiwa mfanyabiashara na biashara yenyewe inafuata sheria hilo sio tatizo ila tukigundua mali hizo au biashara inafanyika kinyume na sheria tunaweza kuwaeleza Takukuru" alisema Kaganda.

  Alisema kuwa kwa sasa uadilifu kwa viongozi wa umma umeshuka hivyo zoezi kama hilo kwa kiasi kikubwa linaweza kurudisha uadilifu huo. Katika hatua nyingine, Jaji Kaganda alisema anafanya utafiti wa sheria ya kutenganisha biashara na uongozi. “Nafanya utafiti kuhusu sheria hii ila kwa sasa ni mapema mno kueleza nilipofikia,” alisema Kaganda.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  What a waste of time and money katika zoezi lililokwisha feli kabla halijaanza!! Hiyo tume iliwahi kufanya wapi kazi zake kwa mujibu wa sheria na zikapata kuheshimika na wote bila maswali kujitokeza kwa wingi zaidi kuliko majibu???

  My foot; bure kabisa na wala hatutegemei chochote humo.
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Tangia miaka hiyo Watanzania tumenufaika nini na huu ******?? Na nani tangia enzi hizo kawajibishwa?
   
 4. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kazi hii, kama kweli ina dhamira nzuri na kuna nia ya dhati, basi ilitakiwa kufanywa kimya kimya! Yaani kwa msemo mwingine, "maneno kidogo, vitendo kwa wingi" na kisha isiishie kutoa ripoti tu, bali na hatua kwa vitendo zichukuliwe.
  Wahenga walisema "Simba mwenda pole ndio mla nyama".
   
 5. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sasa c wangeanza na jk, chenge, lowasa,karamagi au wanaanza na kazi nyepesi ndo ifate ngumu.....!
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hawa machali hawana kitu! wanaacha watu wenye mimali kibao wanakagua amabao bado hawajalimbikiza mali!
   
 7. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona nasikia huyo Placidius luoga amestaafu au hata wastaafu wanaakikiwa
   
 8. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ****** wa kuhakiki mali! Unahakiki mali za Mnyika badala ya kuhakiki mali za akina Blandina Nyoni wanaotuhumiwa
  wahakiki mali za :
  MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU, WAKUU WA IDARA ZA SERIKALI WOTE NA IDARA ZOTE, MAPOLISI HASA TRAFFIC, MAHAKIMU NA MAJAJI,

  Endelezeni orodha iwasaidie hawa TUME inaelekea hawajui wanahakiki kwa lengo gani - KUZUIA RUSHWA NA MENGINE
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  nanusa harufu ya kuwachafua kwa kuwabambikia mali feki watu flani..mnyika,sugu,sitta?
   
 10. D

  Dik JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wana jf kuna thread inajadiliwa hapa kuhusu kukaguliwa na kuhojiwa juu ya umiliki wao wa mali!najiuliza hiv J.mnyika na J.mbilinyi nao ni vigogo?kwani wao ni ccm?maana wamejumuishwa kwenye list ya vigogo 60 watakaochunguzwa mali zao!hiv jk,pinda,mkapa,rostam,EL,Chenge,...et al walishachunguzwa?mbona mali zao hazitangazwi?au maana ya kuchunguzwa ni nini?ina maana wote waliokwishachunguzwa wanamiliki mali kihalali!mbona hatujackia hata mmoja kutuhumiwa kumiliki mali visivyo?hebu 2shirikishane wana jf!
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  kigogo wa nini? hebu peleka maneno yako ya ccm huko
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,517
  Trophy Points: 280
  choko choko tu ccm utawaweza? wakawakague hadi kina kanumba kama vipi
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sijakuelewa hata kidogo!ngoja nipite tu
   
 14. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  bado natafakari..............
   
 15. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika nimeshitushwa sana na taarifa kuwa vogogo 60 watahakikiwa mali zao kuanzia Februari 20 hadi Machi mosi , takribani siku 9, jamani kweli inawezekana maana mali za hawa watu haziko sehemu moja zipo worldwide inawezekana vipi ukamaliza zoezi hili ndani ya muda mfupi, nionavyo mimi huu ni usanii ulio macho unless kama kuna hidden agenda.
   
 16. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,500
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Kamishina wa Maadili ni Jaji mstaafu Salome Kaganda!!!

  Hivi mbona hizo post zinakwenda kwa wastaafu tu!!!
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,077
  Likes Received: 6,539
  Trophy Points: 280
  Ni njia mojawapo ya kugawana keki ya taifa
  ili na wahakiki wale, kwani hamuwaoni hawa
  mafisadi waliobobea wanaojenga mapramidi
  huku bongo mnakwenda kuhangaika na akina
  samweli sitta, kuna viongozi wanakurupuka kama
  wametoka usingizini - kuhakiki nini kuhakiki.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Serikalini watu wako busy kutafuta posho aka per diem. Hakuna la maana wanalofanya hata wakihakiki mali hizo na kugundua kuna kasoro watakaa kimya maana wameshakula posho tayari.
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  ****** mtupu wanafanya,chenge mbona simuoni kwenye list,Anne makinda simuoni khaaaa
   
 20. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  “Hawa hawana tuhuma zozote ni utaratibu wa kawaida tu,”alisema. Jaji mstaafu Kaganda aliliambia gazeti hili kuwa si kosa kwa kiongozi yoyote wa Serikali kuwa na mali na kwamba kosa ni mali hizo kupatikana kinyume na sheria. “Mbunge akiwa mfanyabiashara na biashara yenyewe inafuata sheria hilo sio tatizo ila tukigundua mali hizo au biashara inafanyika kinyume na sheria tunaweza kuwaeleza Takukuru" alisema Kaganda.


  Ni kwa vipi wawe hao wachache kama hawana tuhuma au kuna ajenda nyingine nyuma ya pazia?!!!
   
Loading...