Vigezo vya TRA kufanya makadirio ya juu zaidi ya gharama halisi za magari yanayoingizwa nchini

Hiyo ngoma ya umeme mkuu ina battery haina engine ya mafuta wala gesi.

Kibongo bongo itabidi uchaji kwa umeme wa Tanesco. Huu huu wa single phase 220v ila ndio inabidi uweke circuit breaker kubwa zaidi ya 32amps. Betri itajaa ndani ya masaa 12 na utaweza kutembea 500km. Inachaji kwa 7kW so ndani ya masaa 12 itakuwa imetumia 84kWh yani unit 84 za umeme ambao kwa rate tunayonunua bongo ni kama umeme wa 30,000/= hivi

Yaani Tsh 30,000 unatembea 500km, Dar Dodoma hiyo. Tesla sio gari ya mchezo.

Ukitaka gari ijae haraka unafunga umeme wa three phase 400v hiyo mzigo unakuwa unachaji kwa 11kW ndani ya masaa 8 gari imejaa. So unit zinatumika zaidi kidogo 88kWh ila unakuwa umeokoa muda.

Usiulize service. Hizi gari hazina oil mkuu hazina oil filter hazina spark plugs, ATF na madude mengine. Motor yake ni sealed hamna cha kuservice. So labda uongezee maji ya wiper mkuu

Gari hizi zina regenerative braking ambapo ukitoa mguu kwny pedal ya "mafuta" gari inageuza direction ya motor na kutumia momentum iliyobaki kwenye gari kulipunguza spidi huku at the same time umeme unaovunwa hapo unawekwa kwny betri. Kwahyo brake pad huzitumii sana kama kwny gari za engine.

Yani ukiwa unashuka mlima au ukiachia mafuta, tairi zinageuzwa dynamo kurudisha umeme kwny betri ya gari! Na kifanya hvyo ndo inakuwq kama breki ya gari yani. Chukulia mfano vile vitaa vya baiskeli vya kwny tairi ya mbele, kama unakumbuka ilikuwa ukiiconnect kwny tairi inawaka unavyoendesha ila baiskeli inakuwa nzito zaidi.

Vitu vya kutengeneza kwny hii gari labda mabushing na mashock up

Tatizo bei za hizi ndinga SIO MCHEZO.
Ila ukiipata unasahau shida.
Umeme wa 30k kwa 500km,mbona kama ni cheap sana ku operate hii gari mzee...Sema bei imesimama sana.
Hivi Mo Dewji si anamiliki Tesla mkuu?
 
Umeme wa 30k kwa 500km,mbona kama ni cheap sana ku operate hii gari mzee...Sema bei imesimama sana.
Hivi Mo Dewji si anamiliki Tesla mkuu?
Yeah kuoperate hii gari ni cheap sana. Bei imesimama yes hii ni brand new from Japan bado hujailipia kodi hapa. $88k USD kama 200M hivi

Mo alisema ananunua sijajua kama anayo actually
 

Attachments

  • Screenshot_20191203-133523_Chrome.jpg
    Screenshot_20191203-133523_Chrome.jpg
    110.3 KB · Views: 1
Mkuu ukitaka uchoke kabisa kuna gari inatwa Lexus IS250 hio ni muendelezo wa Altezza yani gari ya kuanzia 2006 na kuendelea ushuru wake ni mkubwa balaa unaweza hata ukazimia
Kuna kitu inaitwa jeep compass la 2005-2009 , Japan CIF ni $ 4500 hadi $ 5000....sitaki kuongea mengi nendeni wenyewe mjionee kwenye kikokoteo chao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bil
Nawaambia mara nyingi hapa kwamba TRA ni kikwazo Tanzania. Lakini majinga majinga yanakuja hapa oooh...! Mnakwepa kodi. Ole wako yakukute. TRA wameirudisha nyuma sana hii nchi kwa kodi zao za ajabu ajabu. Siku hizi watu wanaoenda kuagiza mizigo nje wamepungua mno,sababu ya makadirio ya ovyo ya hawa njemba. TRA ni majanga
Bila TRA wengi tungemiliki mikoko.Na wale ambao tayari wanayo wangemiliki ya maana zaidi
 
Nd
Ikisikia wizi ndio huu, gari inauzwa 21m ,ushuru ni mara tatu ya garama ya kununua
Ndiyo maana hakuna mpango wa kujenga kiwanda hata Cha kuassembly magari tu maana biashara ya kukusanya Kodi inalipa kuliko kuwa na kiwanda
 
Salam wana jukwaa.

Kodi ilivyokadiriwa kwenye gari aina ya Subaru Exiga ya mwaka 2008, ambapo ushuru wa garii hii unasomeka kama Tsh 21,000,000 wakati Valuation iliyotumika kwenye kupata ushuru huo ni Dola 8000+

Uhalisia wa gharama za gari hii yaani CIF ni dola kati ya 2000 mpaka 5000+ kama ambavyo ntaambatanisha kwenye picha hapa chini. Kwa kweli kodi iliyokadiriwa ni kubwa mno kwa gari hii ukilinganisha na CIF halisi tunayoishuhudia kwenye mitandao ya wauzaji wa magari huko Japan ambayo ni kati ya CIF dola 1900 mpaka CIF dola 5000.

Subaru Exiga ya 2009 imethaminishwa kwa CIF dola 11,000 na Ushuru wake ni 22,000,000+ wakati ukiingia mitandao halisi ya wauza magari huko nje unakuta CIF dola 2000 mpaka 6000 ambayo ni chini sana tofauti na wanayotumia wao kwenye hesabu zao.

Ombi kwa mamlaka husika wajaribu kulipitia upya jambo hili au kama kuna vigezo maalum wanatumia kwa baadhi ya magari basi vizuri wakaweka utaratibu wa kutoa elimu juu ya vigezo hivyo ili watanzania wapate kufahamu.

Kama ni makosa ya kibinadamu pia wafanye marekebisho maana watanzania wengi wanataka kutumia gari hizi ila Ushuru mkubwa ni kikwazo.

Karibuni wadau kwa maoni zaidi ili Mamlaka ipate kuona uzito katika jambo hili na kwa aina nyingine za magari.

0746267740...Waagizaji wa Magari kutoka nje ya Nchi

View attachment 1266524View attachment 1266525
Kabla ya huu uzi niliwai kuandika kuhusu hii Subaru Exiga. Habari njema ni kuwa TRA wameshusha kodi ya Exiga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom