Vigezo vya TRA kufanya makadirio ya juu zaidi ya gharama halisi za magari yanayoingizwa nchini

Me niligiza bmw x3 specification zikionesha ni Wagon kikokotozi kikasema kodi ni 11.7m

Gari imefika nimelia hela naenda kutoa wanakataa kuwa walikosea ile ni SUV SPORT ivyo kodi inaenda mpk 23m nilichoka akili

Serikali isipoangalia TRA wanaweka uzio sana kwenye uingizaji wa magari nchini
Maana hapa nawaza kuagiza gari nyingine ya gharama but na wasiwasi na hawa jamaa
 
Mkuu ukitaka kushangaa angalia Audi na VW magari ya kuanzia 2009 ushuru wake utakimbia hadi unajiuliza hivi hawa jamaa hawataki watu waendeshe magari ya ulaya au vipi nahisi wengi wao ni watu waluotoka vijijini sana wanaona VW au Audi ni magari ya anasa sana
 
Kwa kawaida mitandao ya wauza magari duniani(hasa Japan), haiaminiki. Hivyo gari ya aina moja na umri mmoja inaweza kuuzwa bei tofauti tofauti.
Pia wateja wanaweza kula njama na wauzaji ili 'CIF value' iwe ndogo. Hivyo TRA ilichofanya ni kufanya utafiti na kujiwekea 'CIF value' waliyoifanyia kazi kwa magari mbalimbali ili wasije 'kupigwa' na wafanyabiashara.
Kinachokera ni pale wanapo-'uplift' tena hizi tarakimu baada ya gari kufika Bandarini na taratibu za malipo ya ushuru kuanza.
Hii inaleta wasiwasi kuwa hata kikokotoo chao wenyewe hawakiamini..
Mkuu naona hauelewi kinachoongelewa hapa ni CIF iliyowekwa na TRA maswala ya ku uplift hayahusiki mfano ukiangalia beforward BMW 320 ya kuanzia 2005-2010 CIF ya Japan inaanzia $2200-4500 ila gari hio hio kwenye CIF ya TRA ile ya kwenye kikokotoo ni around $2500-2900 swali linakuja inakuaje hio Exiga wameivalue kwa $11,000 kama CIF ya TRA ya kikokotoo wameipata wapi hio bei?
 
Kweli mpo sahihi hawa TRA Motor Vehicle system hawapo sahihi kabisa hii Model ya Exiga wameiweka kundi la SUV na wanaipiga zaidi ya 20M
labda kwa vile wapo kweny viti tu hawayajui magari yote, wauzaji/ waagizaji na watumiaji wangewahabarisha wabadili hicho kipenele
Hizo valuation haziwezi kufanyiwa marekebisho kwasasa. Nenda ofisi yoyote ya tra waulize kwann makadirio ya ushuru yapo juu kuliko bei halisi? Wakikupa majibu ya uhakika, najiondoa jf. 90% ya wafanyakazi wa tra hawajui kwann ushuru unakuwa x2_x3 ya bei halisi. Wanapata pesa ndefu kuliko wauzaji.

Halafu mimi nafikiri imefika wakati ambao teknolojia inatakiwa itumike kimkakati. Wafanye utaratibu ukitaka kuagiza gari, pesa ya kodi inakatwa juu kwa juu. Bandarini unalipia tozo zao tu.
 
Kwa kawaida mitandao ya wauza magari duniani(hasa Japan), haiaminiki. Hivyo gari ya aina moja na umri mmoja inaweza kuuzwa bei tofauti tofauti.
Pia wateja wanaweza kula njama na wauzaji ili 'CIF value' iwe ndogo. Hivyo TRA ilichofanya ni kufanya utafiti na kujiwekea 'CIF value' waliyoifanyia kazi kwa magari mbalimbali ili wasije 'kupigwa' na wafanyabiashara.
Kinachokera ni pale wanapo-'uplift' tena hizi tarakimu baada ya gari kufika Bandarini na taratibu za malipo ya ushuru kuanza.
Hii inaleta wasiwasi kuwa hata kikokotoo chao wenyewe hawakiamini..
Wao walipaswa kukadiria bei reasonable, na inayolipika. Watu wangelipa. Lakini wanakadiria bei kubwa mno isiyolipika. Hii inashawishi watu kukwepa kabisa. Kutokulipa hata hiyo kidogo hawaipati.

Unanunua gari mpaka hapa dar. Inafika kwa shs Mil 4.5. Wao wanataka Kodi mil 5. Hivi mnachangia au ?? Kodi ni asilimia ya fedha unayonunulia. Wao wanaweka Kodi zaidi ya mtaji ?
 
Kweli mkuu, VW Passat ni kama Toyota Corolla tu Ila ushuru wake sio wa kawaida mpaka nashangaa. Nilicheck hata Vauxhall insignia ina ushuru mkubwa kuliko hata Passat nikaona hawa tra ni washamba kabisa.
Mkuu ukitaka kushangaa angalia Audi na VW magari ya kuanzia 2009 ushuru wake utakimbia hadi unajiuliza hivi hawa jamaa hawataki watu waendeshe magari ya ulaya au vipi nahisi wengi wao ni watu waluotoka vijijini sana wanaona VW au Audi ni magari ya anasa sana
 
Kweli mkuu, VW Passat ni kama Toyota Corolla tu Ila ushuru wake sio wa kawaida mpaka nashangaa. Nilicheck hata Vauxhall insignia ina ushuru mkubwa kuliko hata Passat nikaona hawa tra ni washamba kabisa.
Mkuu ukitaka uchoke kabisa kuna gari inatwa Lexus IS250 hio ni muendelezo wa Altezza yani gari ya kuanzia 2006 na kuendelea ushuru wake ni mkubwa balaa unaweza hata ukazimia
 
Hapa ndipo nilipowaheshimu TRA
Screenshot_20190906-114137_Chrome.jpeg
Screenshot_20190906-114143_Chrome.jpeg
 
Hili swala la kodi la magari jamaa wanakosea sana,
Na ni dhambi kubwa sana na ndiyo maana viongozi wao wengi wamepata matatizo ukute ni laana za mangung’uniko ya watu kama Haya ya magari!

Unakuta mtu amekopa saccos, ameona kwenye mtandao trade car view gari dogo bei USD 2,000/- ameshajipanga na kiasi cha ushuru wa kulipa kwa kuzingatia gharama alonunulia,

Sasa akifika TRA CUstoms wanamwambia hii gari thamani yake ni USD 5,000 imagine

Badala ya kulipia ushuru kwenye bei halisi ya usd 2,000 analipia ile ya TRA usd 5,000/-

Hii kitu imekuwa ikiumiza wananchi kwa kiasi kikubwa sana!

Kwa hiyo mwananchi inabidi ashindwe kulipia ushuru gari iende mnadani au akakope tena aje kulipa ushuru wa forodha.

Tumuogope Mungu
 
Me niligiza bmw x3 specification zikionesha ni Wagon kikokotozi kikasema kodi ni 11.7m
Gari imefika nimelia hela naenda kutoa wanakataa kuwa walikosea ile ni SUV SPORT ivyo kodi inaenda mpk 23m nilichoka akili
Serikali isipoangalia TRA wanaweka uzio sana kwenye uingizaji wa magari nchini
Maana hapa nawaza kuagiza gari nyingine ya gharama but na wasiwasi na hawa jamaa

Daah, hawa jamaa ni wadhalimu sana aisee,kwa staili hii nchi yetu ktk sekta ya usafirishaji itadumaa sana kukua
 
Unaweza kuwa na gari unataka umtumie mtu zawadi, umlipie mpaka kulisafirisha, alitoe mwenyewe huko.

Ukiangalia ushuru unagahairi.

Maana unakuta ushuru ni mkubwa kuliko bei na gharama za kusafirisha gari.

Unaweza kumpa mtu zawadi, halafu zawadi ikawa adhabu.
 
Huu ni wizi mchana kweupe, kama tungepata wanasheria makini, tungefungua kesi dhidi ya serikali.

Hakuna sababu ya msingi ushuru kuwa mkubwa kiasi hiki, tena gari ya miaka kumi nyuma.

Chama cha walaji wanaangalia bei ya mchele na maharage tu, SMH !!
 
Back
Top Bottom