Vigezo vya kumuengua mgombea wa CDM Igunga hivi hapa! 2

MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
999
815
Naomba wahakiki mnisaidie kupanga vizuri mada hii ili iwe na mtiriko mzuri, kwani natumia Cellphone na kuna Advert inanisumbua na kunikatisha, naomba niendelee na kigezo cha pili ambacho kitatumika kumuengua Mwl Kashindye, Kisha mwisho Kama hakutakuwa na interruption yoyote na kama charge itabakia, basi nitasuggest namna ya kupangua, lakini naamini kwa kuanika hadharani njama hizi, basi kutavunja nguvu sana utekelezaji wake.

Kipengele cha pili kitakachotumika kumuengua Mwl Kashindye ni hiki kifuatacho, kwenye form zake za kuwania ubunge alizokwenda kuzichukua kwa Mkurugenzi, kuna kipengele cha udhamini wa chama chake, mbali ya udhamini wa wapiga kura. Kipengele hiki kinatakiwa kujazwa na Katibu wa Wilaya wa chama chake ambacho ni CHADEMA, bila udhamini wa Katbu huyo form hizo zitakuwa hazija kamilika, mgombea ataenguliwa.

Sasa kwa Hali ilivyo CCM wilaya ya Igunga imegundua kuwa Katibu wa Wilaya wa CHADEMA, Bw Christopher, hakuchaguliwa kihalali kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, kwa hiyo watapinga uhalali wa yeye kuwa na mandate ya kumdhamini mgombea kwa niaba ya CHADEMA, kwa hiyo mgombea wa CHADEMA itabidi aenguliwe kwa kuwa atakuwa amekosa udhamini wa Afisa wa chama ngazi ya wilaya kama sheria inavyotaka.

Vipengele hivi viwili visipofanyiwa kazi (Wanasheria wanajua hivyo) hata kimojawapo tu kikipita kinatosha kuleta maafa na kilio, kulalamika na mikwara mingi baada ya mzinga kulia, havitasaidia. Kwa kuwa nachukia dhulma na kupenda haki itendeke, ingawa sina mamlaka yoyote ndani ya CDM, basi naomba tu wanasheria wa CDM waikague vizuri barua ya likizo ya Mgombea, kisha waiangalie zheria inayohusiana na utaratibu wa utoaji wa barua hiyo, kama vile, je, aliesaini barua hiyo Ana mamlaka hayo?

Maelezo na mihuri yake inakidhi? Chronological factors zimekaa sawa? Hakuna errors zozote (typing or otherwise) ambazo zinaweza kupotosha maana hivyo kutoa mwanya wa barua hiyo kupingwa uhalali wake? Pili, wahakikishe kuwa ni kweli kuwa katibu wa Wilaya wa CDM Bw Christopher hakuchaguliwa katika nafasi yake kwa mujibu wa katiba ya CDM, kama ndivyo, je ni utaratibu gani ulitumika wa kumuinstall, je document zilizomuhalalisha zipo na zipo valid hadi sasa?Kila ilivyo, wanasheria wazipuuze hata chembe ya factor yoyote inayoweza kutumiwa kumkwamisha mgombea, otherwise muda hautatosha kujitetea mahakamani kama ilivyokuwa kwa Wenje kule Mwanza, uchaguzi ule ulikuwa wa miezi mitatu lakini huu utakuwa wa wiki tatu tu, mahakama ikimaliza kusikiliza rufaa kabla haijatoa uamuzi uchaguzi utakuwa umekwisha, ngoma itabidi ije ianze upya!

MIBA YA MGUNGA HAIUCHOMI MGUNGA!
 
Naamini viongozi wa chadema watakua makini walio yapataga mbea wanayakumbuka
 
Bila shaka uongozi wa juu wa CDM hawatakubali yajirudie ya Mbeya vijijini kwa hiyo naamini watalifanyia kazi.
 
Hivi hizo microscope kali za NEC huwa ni kwa ajili ya fomu za wagombea wa CDM tu? Na by the way.... hivi makatibu wa CDM wa wilaya huwa wanachaguliwa au wanateuliwa -- yaani wa kuajiriwa -- kama vile kwa CCM? nauliza tu.
 
Mara nyingi muovu akishaona mbinu zake zinawekwa hadharani anaacha uovu, nadhani CCM kama wanazo hizo mbinu chafu na sisi tumeishazijua mapema wataamua kuachana nazo. Kama wana Igunga wameanza kuwa na msimamo basi hakuna wa kuizuia mvua. Ila binafsi siwaamini sana wanyamwezi, wao kwa CCM ni kama mbwa kwa chatu, huwa wanajipeleka tu...
 
Kweli CCM imefika pabaya -- Yaani yote haya ina maana kuwa CCM wangependa hasimu wao CDM waenguliwe ili wapete kiulaini? Watafanya mara ngapi hivyo?
 
Lakini kwa kuonbgezea tu hap juu, CCM wanaweza kumhonga mgombea wa CDM ili avurunde katika fomu zake kama vile kwa yule wa Mbeya Vijijini Shitambala. Au kama vile yule wa Bunda na kwa Mukono. Hii CCM wanaweza kufanya kutokana na nguvu za pesa.
 
Sasa kwa Hali ilivyo CCM wilaya ya Igunga imegundua kuwa Katibu wa Wilaya wa CHADEMA, Bw Christopher, hakuchaguliwa kihalali kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA,
Baseless claims nilifikiri unasema waliogundua ni wanaCDM kumbe ni wana CCM? unaweza kutuambia katibu wa CDM wa wilaya na si wa CCM anachaguliwa na nani? 'Utawapata tu wasiokufahamu' unaweza kuni quote hapo.
 
Back
Top Bottom