Vigezo vitakavyotupa Rais bora 2015 (Dini, Muungano, kipato, elimu, Katiba Mpya, wafadhili)

Hivi ndivyo kiongozi anavyotakiwa kuwa siyo kiongozi asiyeweza kutoa hata mawazo ya nini kifanyike na kwa mda gani kifanyike na sababu gani kifanyike.
 
Hehehehee,je kwa sasa ni nani anaweza kuthubutu kugombea uraisi,hasa kwa kigezo cha kuanzia jimboni kwake????
Je kuna mwanasiasa ambaye yupo tayari kuandika kitabu??-wengi wataandikiwa na maprofesa hawahawa,,,,
 
Hatuhitaji mgombea urasi ambae jk akibadili miwani au sauti naye anabadili ili wafanane, akipunguza nywele nae kaiga, hatuhitaji mgombea ambaye maneno anayoongea hayatoki rohoni, mgombea ambae ana jukumu la mahusianoya kimataifa, badala ya kuyaboresha anaomba talaka na kutaka uadui na majirani, je angekuwa rais jumuiya ya afrika mashariki ingekuwepo leo? Hizo gharama zilizopotea angezitoleaje maelezo, hapo tu ameshindwa kuhimili, akipewa pakubwa si ataomba talaka kila mahali
 
huwez msema membe kwa mabaya ni kati ya wawania urais anayekubalika siyo tu kitaifa bali hata kimataifa huyu ndo team uzalendo team tanzania tunayoitaka
 
Hili suala la kwenda vyuo vikuu haswaa ndio la muhimu sn,sio unatuambia kutunga vitabu! vya nn? nenda kaoneshe kwa watu uwezo wako wa kimaadili na thinking capacity."Akili ndogo kutawala akili kubwa"
 
Sidhani kama Tanzania inahitaji Raisi Mropokaji mithili ya Membe. Kauli alizowah kuzitoa Membe kuhusu mgogoro wa Malawi na ule wa EAC ni za kukurupuka. Hata akipata nafasi ya kuwa Mgombea hii nchi itafikia pabaya
 
Hehehehee,je kwa sasa ni nani anaweza kuthubutu kugombea uraisi,hasa kwa kigezo cha kuanzia jimboni kwake????
Je kuna mwanasiasa ambaye yupo tayari kuandika kitabu??-wengi wataandikiwa na maprofesa hawahawa,,,,

yupo aliyetayari kumlipa mtu amuandikie kitabu, halafu yeye anaki-kariri. Sema kwenye kujibu maswali ya wakufunzi na wana-vyuo itabidi atafute mbinu.
 
Watu wajitokeze na wabuni vigezo vigumu vya mtu kutaka kuliongoza Taifa. Kigezo hakiwezi kuwa kabila, wala fedha, wala marafiki, wala gender, wala hasira dhidi ya Serikali! Ofisi kuu ya nchi inataka watu mchanganyiko wakiwemo wasomi wakuombe ugombee na siyo kinyume chake.Urais siyo biashara. Urais sio kitu cha kukurupuka na kukimbilia! Mtu lazima uende kwenye kioo, jiangalie, jipime na jiulize; una sifa zipi unazowazidi Watanzania wenzako zinazokufanya udhani zinatosha kukufanya uwe Rais? Kama huzioni toka! Usipoteze muda na kudhani unaweza kupata urais kwa kudra. Pili kama Kafulila anavyosema lazima uandike kitabu cha namna utakavyolisaidia Taifa na (my emphasis) hasa mpango wako wa kupambana na rushwa na wa kuleta maendeleo. Vyuo vikuu visaidie kuwachuja waombaji kabla ya vyama husika kuchagua nani anafaa! Jamani msipofanya hivyo, Mtakuja kuchagua kinyozi wa nchi badala ya kiongozi wa nchi.
 
Membe azidi kumjibu Kafulila kuhusu urais wa 2015.Hii ni mwendelezo wa majibu yake kupitia group la Friends Of Hon.Membe la katika mtandao wa kijamii linaloongozwa na kijana Allan.
 
mkiikuuza hii picha mtakubaliana nami kuwa wakati ukifika wananchi hatutaki kuhutubiwa, tunahitaji kuwauliza maswali wanaotaka tuwaajiri top post.

ili wasituhonge mikutano tutaiandaa sisi wenyewe tuwaweke kikaangoni. maswali hayapatikani vyuoni pekee, hata vijijini maswali yapo.
 
Kama Membe anaweza kuwa rais, basi Tanzania itabidi kuomba sana maana miaka 5 itakuwa kama miaka 50.
We don't have leadership vaccum! Katika kipindi chake kama waziri wa Mambo ya Nje tumeshuhudia kwa mara ya kwanza mkuu wa diplomasia kutangaza vita na majirani wa Malawi badala ya kuwa mwanadiplomasia. Hili linaonyesha jinsi anavyokurupuka hata kwa yasiyo mhusu.
Kama mtu aliyefanya kazi ya ushushushu (intelligence) kukurupuka ni kati ya vigezo muhimu vya kumuondoa kwenye wadhifa alionao hata nyingine.
Mabalozi wa nchi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao wote kasoro mmoja tu wanamuona mbabaishaji, mtaka sifa na asiyejibu anachoulizwa.
Katika hili, namwomba Mola atuepushe naye vinginevyo atatusababishia matatizo mengi kuliko kutatua yaaliyopo.
 
Back
Top Bottom