Vigezo vitakavyotupa Rais bora 2015 (Dini, Muungano, kipato, elimu, Katiba Mpya, wafadhili) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigezo vitakavyotupa Rais bora 2015 (Dini, Muungano, kipato, elimu, Katiba Mpya, wafadhili)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by busar, Mar 21, 2012.

 1. b

  busar JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Sio habari tena kwamba mbio zauraisi 2015 zilianza 2004 na labda nyuma ya hapo. Kwa tuliopiga kura yakumchagua rais wa 2005/10/2010/15 huenda pia tuliamua juu ya rais wa2015/2020.

  Leo hii vigezo vitakavyoamua rais ajaye huenda vimeimarika zaidi na kutoa changamoto kubwa zaidi kwa nchi, wagombea, wapiga kura na majirani zetu. Sehemu hii ya kwanza nitajadili machache.

  Sehemu ya pili, tatu na nne nitakamilisha.


  Dini
  Pamoja na kuwa Katiba yetuinatupa uhuru wa kuabudu na kuamini mungu umtakaye maadamu haiingilii uhuru wa mtu mwingine lakini nguvu ya dini hizi mbili, yaani Uislamu na Ukristu si ya kubeza. Leo hii ni dhahiri kwamba kuna udini Tanzania (dini kama mojawapo yavigezo vinavyompa sifa mtu na haki ya kupata vile ambayo asiye wa dini husika hapati, iwe kwa uwazi au kwa kificho).

  Hali hii imejitokeza na inaimarika katika mfumo rasmi (wa kisheria na kitaratibu kama katika elimu, biashara na ajira) na katika mfumo usio rasmi (mashindano ya kidini, katika michezo, vijiwe na maongezi ya mtu na mtu). Katika mfumo usio rasmi ni sifa kwa muislamu na jambo la kujivunia kuwa na kiongozi au mkuu wa kitengo Fulani muislamu, halikadharika kwa mkristo ni sifa na jambo la kujivunia kuwa na mkristo kiongozi au mkuu wa kitengo Fulani mkristu.

  Na kinyume chake ni jambo baya kuongozwa na mtu wa dini isiyo yako. Wasomi na viongozi kadhaa wa umma kwa unafiki wamelibeza hili mbele ya umma kwa muda mrefu sasa. Ni Mh. Rais Kikwete tu aliyelieleza hili kwa ujasiri mbele ya umma katika hotuba yake kwa wabunge wa bunge la JMT, lakini pia alibezwa na wengi, hata viongozi wa dini ambao kwa siri wanaliona lakini kwa unafiki wao wanashindwa kulisemea.
  Raisi wa kwanza wa nchi yetu alilaumiwa, na anaendelea kulaumiwa sana na jamii ya kiislamu kwa kuukandamiza uislamu Tanzania na kuujenga na kuuimarisha ukristu (ukatoliki?). Waislamu wana sababu wanazozitoa.

  Nitatoa mifano michache katika hili, tumeshuhudia sana wakati wa mazimisho ya miaka 50 ya uhuru kuwa wapigania uhuru wengi na hasa waislamu hawakuenziwa na utawala wa mwalimu Nyerere (je tatizo ni dini yao?), pia kuundwa kwa BAKWATA kuwa haikuwa ridhaa ya waislamu bali malengo ya Mwalimu kuunda chombo cha kugandamiza uislamu na harakati za uislamu kujitanua, nafasi za ajira na uongozi. Katika elimu pia, fuatilia madajiliano baada ya matakeo ya kidato cha nne yaliyopita na sakata la Ndanda Sekondari kwa uchache kwa siku za jirani.

  Rais Mwinyi naye katika utawala wake alilaumiwa sana na wakristu kwa kujenga uislamu Tanzania. Maaskofu na hasa wakatoliki (TEC) walijitokeza wazi kuvutana na serikali katika mambo kadhaa. Wakristo waliona kuna kitu kinapungua kwa kuwa na Rais muislamu, na hasa wavaa kanzu wengi kuonekana wakitembelea Ikulu na shamrashamra za kiislamu kuwa na mh. Rais mara nyingi. Hamu ikawa ni kuwa na mabadiliko katika uchaguzi wa mwaka 1995.

  Tunatambua kwa hakika harakati kadhaa za mihadhara ya uislamu na ukristu ilivyoshamiri katika awamu hii.
  Kelele za lawama kutoka kwa maaskofu zilipungua sana katika wakati wa Mkapa na nyingi zikitokea katika uislamu. Lakini bado alihusishwa sana na ukristu, katika teuzi zake kwa wakuu wa idara nyeti za umma kama Mahakama, TISS, na Jeshi. Wakristo waliona ile kuwa na rais asiye muislamu ni jambo jema kwao bila ya hasa nini anakifanya.

  Baada ya enzi ya Mkapa, kaingia Kikwete, kwa mbwembwe na sifa nyingi kutoka pande zote za dini hizi. Waislamu wakiona ni wakati sasa wakukamilisha ajenda zao nyingi kama kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi na kuongeza idadi ya wateule waislam. Mambo ambayo waislamu wengi wanaona leo bado hayajatimia na wangependa yasimamiwe na awamu ijayo ya 2015/20.

  Na wakristu nao wakaona Kikwete aliyesoma shule za kikristu na mwenye msimamo usiojulikana juu ya u-islamu atafaa kwa sasa kwani ndio chaguo lilokuwepo na namna pekee ilikuwani kumuunganisha na Mungu wa wakristu kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu.

  Katika miakahii 7 tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia mivutano na minyukano mikali ya u-dini. Ndani ya mfumo wa elimu na hasa makao makuu, ofisi ya utumishi, TISS, wizara ya fedha, mashirika ya umma, wakala za serikali, mifuko ya hifadhi yajamii, uafisa katika idara nyingi za halmashauri.

  Ni vigumu kuamini mambo haya, lakini pia panahitajika vigezo gani ili kuyaamini haya?
  Sasa tunapoelekea uchaguzi wa 2015 kigezo (variable) cha dini kitakuwa na nguvu kubwa. Wakristo watapenda rais ajaye awe mkristo kama sifa kuu ya kumuunga mkono (tunatambua nguvu ya maaskofu wa makanisa mbalimbali ndani ya Tanzania).

  Huyu mkristo atakabidhiwa (ameshakabidhiwa) jukumu la kusimamia nchi isiyo na mahangaiko ya udini (kuachana na mahakama ya kadhi), kurudisha taasisi za kikristu mikononi mwa wenyewe, kuteua wakristu katika taasi muhimu za umma na kurekebisha na ama kuzima kabisa hisia za udini katika makao makuu ya Wizara nyingi hasa Elimu, fedha na ofisi ya Makamu wa Rais na Utumishi Makao Makuu. Rais mkristo atatakiwa kusukuma mbele ajenda ya kufadhili taasisi za kikristu kwa mlango wa ruzuku.

  Mfumo huu ni vigumu kwa waislamu kupambana nao kwani taasisi nyingi za afya na elimu ni za kikristu.
  Mgombea u-Rais mkristu ndio litakuwa pia chaguo la nchi za magharibi ambazo harakati dhidi ya u-islam ni kati ya ajenda kuu ya kiuchumi na kijamii. Hili litaongezwa nguvu na mapambano ya ugaidi kwa sasa, mambo ambayo Mkapa aliyasimamia kwa nguvu na misingi yake kushindwa kuvunjwa na Kikwete.

  Ufadhili wa nchi za magharibi kwa TISS ulijikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi. Pamoja na kutokuwa na uhakika wa takwimu zetu lakini ukiachia ukanda wa pwani (Dar, Lindi, Mtwara, Tanga) nabaadhia maeneo machache ya bara (kama Tabora, Kigoma na sehemu chache za mkoa wa Kagera na Iringa) sehemu zinazosalia kwa Tanzania Bara ni ama Wakristu, kwa uchache sana waislamu na/au wenye dini nyingine (lakini si uislamu).

  Pia ndani ya ukanda wa Pwani ukristu umeenea sana na idadi ya wakristu kuongezeka. Pia wana ushawishi mkubwa wa kitamaduni (umagharibi) kuliko uarabu (tazama miji ya dar, tanga),. Wakristu hawa ni wapinzani wa uislamu kwani kwa mtazamo wao u-islamu ni si dini sahihina (wenye mtazamo mkali uislamu=ushetani). Kundi hili la wakristu watakuwatayari kumpigia kura rais yeyote asiye mu-islamu kwani kufanya hivyo ni sehemuya kuimarisha uinjilishaji.

  Hapa kigezo cha usafi kitashindwa dhidi ya umoja. Ajenda ya ufisadi haitakuwa na nguvu tena.
  Mgombea u-Rais muislamu asiye na msimamo mkali na ambaye hajulikani vizuri huku bara anaweza kupewa nafasi kiasi ndani ya jumuia ya kikristu lakini ni wakristu wachache wataziba masikio yao wakati wa kampeni kama kauli hii itatumika ‘” waislamu kuongoza nchi kwa awamu mbili, yaani miaka 20”’’ . kwa hakika ataungwa mkono kwa nguvu zote na waislamu hata kama hana sifa, sifa kuu ya kuwa mu-islamu itakuwa kigezo kikuu. Huyu ndiye atakayebeba jukumu la kukamilisha uwepo wa mahakama ya kadhi na vipaumbele kadhaa kwa waislamu.

  Waislamu watapata nafasi ya kutafakari upya ndoto ya kuanzisha mahakama ya kadhi. Karata ya waislamu wa Tanzania kumpata raisi muislamu awamu ya tano itawabidi kuungana na wazanzibari kupigana kupata Rais wa Muungano mzanzibari. Kwani hilo litawahakikishia rais muislamu (hata kama ni mzanzibari).

  Kama hili likifanyika (limeanza kufanyika?) changamoto kuu ni namna ya kumuuza kwa wabara, ambao ni wapiga kura wengi na ambao kwa hakika bado hawaoni mzanzibari anayefaa kwa sasa kuwaongoza. Hili la changamoto za kumnadi mgombea uraisi mzanzibari nitalieleza vizuri katika sehemu zijazo.


  Hivyo basi vyama vya siasa, wagombea urais na wapambe wao wanalazimika kukiangalia vizuri kigezo hiki chadini na kuchagua maneno mazuri sana ya kutumia kuwauza watu wao. Ni wakati muafaka wa ‘think tanks’ za watu hawa kufanya kazi hasa juu ya hili ikiwemo kupata ushauri wa wataalmu (Consultants) wenye weledi.

  Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx tuonane maranyingine xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
   
 2. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na malumbano marefu ya kuanza kupiga ramli nani atakuwa rais wetu mwaka 2015. Katika malumbano hayo watu wanaongelea majina ya watu. Mimi nafikiri tuongelee sifa za kiongozi atakayetufaa na baada ya sifa hizo tuangalie nani anazo bila kuangalia chama anachotoka, kabila lake, rangi yake wala dini yake.

  Mimi naanza kuhorodhesha na naomba wengine muendeleze.


  1. Awe ni mtanzania mwenye akili timamu;
  2. Mwenye angalau shahada ya kwanza;
  3. Awe mkweli na muadilifu na fitina kwake mwiko;
  4. Anayechukia rushwa kwa nguvu zake zote na ukimtazama sura yake uone hivyo;
  5. Asiwe mbaguzi wa dini au kabila;
  6. Asiwe na historia ya kufanya au kuhusishwa na scandal yeyote ya wizi au ya ufisadi;
  7. Awe mzalendo, mbunifu na mpenda maendeleo;
  8. Awe mtu anayeamini kwamba Tanzania ina rasilimali za kutosha kinachotakiwa ni namna ya kuzitumia zinufaishe jamii yote;
  9. wengine muendelee....

  Na kama mtu hana sifa hizo asipewe kabisa hiyo nafasi
   
 3. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Awe tayari kutetea rasimali za nchi yetu kwa kuwadhbiti wezi wahusika bila kujali ukubwa majina na vyeo vyao au kuhatarisha maisha yake.
  Awe na uzoefu kiasi wa miaka isiyopungua 10 ktk uongozi. Japo hili linajadilika.
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Asiwe mnafiki, ndumilakuwili, bali awe ni msema kweli na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengi.
   
 5. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Awe tayari kufa kwa ajili ya kutetea siyo tu Taifa na watu wake ila hata katiba ya nchi yake.
   
 6. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Awe maskni au tajiri, lakini akiwa tajiri kusiwe na shaka yeyote jinsi alivyoupata. yaani awe na utajiri unaoelezeka kwa maana ya utajiri wa kurithi au wa biashara na awe mlipa kodi mzuri
   
 7. M

  MWASAMAJENDA Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atambue na kuamini kuwa Tanzania si maskini, na hivyo kutokuwa ombaomba.
   
 8. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Awe mkali sana na mwenye kukemea maovu kwa viongozi wake na alinde mipaka ya nchi kwagharama yoyote
   
 9. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Asiwe opportunist.
   
 10. dabo kliki

  dabo kliki Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Kumbuka tunaweza kuishi bila RAIS ila ni vigumu RAIS kuishi bila WANANCHI hivyo aseme bila kutoa ahadi 79 kuwa ataifanyia nini TZ na siyo TZ itamfanyia nini!

  2. Rais na mawaziri wake wafunge mikanda na siyo sisi walalahoi

  3. Awekewe gavana ya kuthibiti safari za nje na siyo 4:3 yaani siku 4 TZ siku 3 ng'ambo kutembea juu kwa kamba na burudani ya farasi

  4. Awe na walau kahistoria fulani ka kukemea na kuhadhibu wezi nk.
   
 11. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tuendelee kuchangia sifa za mgombea atakayetufaa. Tukiongelea majina hakika tutapata taabu sana kupata rais kwani yapo mengi ambayo yameshaanza kutajwa na hadi kufikia 2015 yatakuwa zaidi ya 50 lakini wana JF tukiongelea wasifu wa rais tunayemtaka hakika majina yatakuwa machache sana na itakuwa rahisi ku-pick moja ambaye atakuwa na sifa hizo. naendelea
  Awe mcha Mungu anayekereka na umaskini wa Watanzania
   
 12. s

  suli Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  awe jasir wa kuchukua maamuzi magumu hata kama mabepar hawatapendezwa nayo
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  awe bikra na hajawahi kabisaa kuliwa au kula
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Sikilizeni kwa makini, nchi hii tunatakiwa kuwa makini sana kwenye kuchaguwa madiwani ili tupate Halmashauri thabiti, Tanzania hata bila Rais mambo yanakwenda tu. kwa sasa Urais ni cheo ceremonial tu ndio maana hata vichaa wanatangaza kugombea Urais. hakuna kazi yoyote wala haitajiki msomi kuwa Rais wa nchi hii.

  [​IMG]
   
 15. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kaka hapa tunamzugumzia mbowe au
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Kwa nini usiulize Manji?
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa anazo zote
   
 18. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Watanzania changamkieni kutoa ushauri kwenye rasimu ya katiba mpya ili iwe yenye faida kwa wote isinufaishe kikundi Fulani kama ya hivi sasa inavyowanufaisha chama tawala cha CCM.

  Katiba mpya iendane na malekebisho makubwa katika taasisi ya urais, bila kufanya marekebisho katika taasisi hii basi hata katiba mpya itakuwa ni bure kabisa kwa maana haitakuwa na uwezo wa kuboresha mastakabali (future) wa taifa letu.

  Mstakabali wa watoto wetu na wajukuu zetu unategemea jinsi tutavyojipanga kuchagua rais atakae toa maamuzi ambayo yatawalinda mbeleni, tusijiangalie sisi tu, ndio maana wanzetu nchi za inje kama Marekani, China au Japan wanatushinda kila nyanja kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa hata kijeshi kwa sababu wanaangalia mbele miaka mia moja au hata miaka mia mbili, sisi hatuna utamaduni huo ambao sasa inabidi au inatulazimu tuanze.


  Kwa mstakabali mzuri wa taifa letu rais ajae awe na sifa nyingi , mbili kati ya hizo ni:_


  1. Rais ajae awe na sifa ya ujasili wa kuvunja mkataba wa kuuza TANESCO umeme iliowekwa na makampuni ya Richmund. Dowans na IPTL. Mkataba huu ukiachwa uendelee huko mbeleni utasababisha maafa makubwa sana kwa sababu gharama za umeme mpaka sasa ni kubwa sana na tunaambiwa bado shirika linaendeshwa kihasara, kikubwa zinatakiwa fedha nyingi kuwalipa hawa jamaa wanaouzia umeme Tanesco.

  MADHARA YAKE SASA. Gharama kubwa za nishati ya umeme zinasababisha jamii ijikite katiak utumiaji wa mkaa wa mimea au miti, wanajamii ngazi zote mahala popote wanatumia mkaa kupikia ili hali wajiko ya umeme wanayo lakini wameyaweka uvunguni kukwepa gharama, watumishi wa serikali waalimu, polisi, wanasiasa wanatumia mkaa kupikia. Wanasiasa wabunge,wakuu wa mikoa na wilaya wanatumia mkaa kupikia katika familia zao, wafanyabiashara wahindi, waarabu, wasomali sehemu za kariakoo , kisutu wote wanatumia mkaa kupikia kukwepa gharama kubwa za nishati za umeme, pia sisi walala hoi tunatumia kuni au mkaa kupikia suala la umeme hatuliwaziii kabisa.

  Gharama za umeme zingekuwa chini wakundi mengine yote niliyoyataja hapo juu yangetumia nishati ya umeme, ni sisi walala hoi tu tungeendelea kutumia mkaa na kuni

  Sasa hebu jiulize hali hii ikiendelea miaka 30 ijayo itakuwaje kimazingira ? milima , vyanzo vya maji vitasalimika kweli? Je kutakuwa na mvua ya kutosha itayowezesha sera ya kilimo kwanza. Ni wazi kabisa hali ya mikataba kama huu wa dowans ukiendelea miaka 50 ijayo taifa la Tanzania litapotea katika uso wa dunia.

  NINI KIFANYIKE. Tunahitaji rais ambae atalinusuru taifa kwa kuliwezesha kutumia umeme utaofuliwa na gesi yetu ambao ni nyingi sana, gesi hii itumike kufua umeme tuachane na umeme wa kununua wa IPTL na DOWANS ili gharama za umeme zipunguwe makundi mengine yatumie umeme watuachie sisi walala hoi tutumie mkaa na kuni. Watu wa Mtwara wanahitaji elimu ya uraia tu wataelewa wanashindwa kuelewa kwa sababu viongozi wanaoenda kuwahabarisha hawana maadili.  1. Sifa kuu ya pili ya rais ajae awe na uwezo wa kuvunja mkataba wa Mtoto wa mfalme wa Saudia wa kukodisha kipande cha ardhi ya loliondo na kutumia kuwindia kwa miaka 30. Makataba huu ni mbovu na unatia aibu ni sawa mtu anakuwa na ubia na mke wako nay eye anakuwa na haki ya kulala nae , mikataba kama hii wajukuu hawataweza kutuelewa, ni sawa na ule mkataba wa kikoloni uliowekwa mwaka 1928 eti nchi za maziwa makuu zilinyimwa ruhusa kutumia maji ya ziwa Victoria ruksa hiyo ikapewa Misri pekee kutumia maji hayo kupita mto Nile si mnaona wenyewe akina Lowasa walivyoushitukia mkataba huu pale walipoanza project ya kupeleka maji Shinyanga?
  Kwa hiyo Lowassa ,sijui Membe,Wasira hawana sifa hizi, watanzania anzeni kutafuta rais ataewasaidia nyie watoto wenu na wajukuu zenu.

  Ebaeban
  Tel.Aviv
   
 19. alteza

  alteza JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2013
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kafulira amesema kweli. Kila mgombea lazima awe na kitu kinaitwa "platform." Yaani anataka agombee Urais ili afanye nini? Na anasifa zipi za kuwazidi watanzania wengine mpaka atake kwenda Ikulu? Amefanya nini jimboni kwake kama ni mbunge kuonyesha kuwa anatenda na amewazidi wenzake! Kwa hiyo kuandika kitabu ni lazima! Lakini la pili lazima waombaji waitwe vyuo vikuu wakatoe lecturer na wajibu maswali ya waalimu na wanachuo ili wananchi waweze kuchagua mchele na siyo pumba.

  MEMBE RAIS AJAE T2015BM

  Kuna umuhimu mkubwa sana kwa mgombea urais ambae ni makini andike kitabu kuhusu nchi namna anavoijua na majibu ya matatizo ya wananchi.itasaidia sana kupima mawazo na kujua hata misimamo ya viongozi hawa kuhusu maswala mbalimbali kuliko kufanya issue ya kugombea kama jambo la mipasho na mapambano ya umbea..nimuhimu tujue mawazo na fikra zao kuhusu mambo mengi ya nchi yetu. Nasema hiv kwasababu kuna watu wanagombea sio kwasababu wana mawazo bali kwasababu muda wa uchaguzi umefika.
   
 20. M

  Mr. Mpevu Senior Member

  #20
  Nov 16, 2013
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 111
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  Hapo umenena mkuu. Tunahutaji daktari anayejua maradhi yetu na dawa ya kutibu maradhi hayo. Kina mamvi kazi kwenu.
   
Loading...