Vigezo vitakavyotumika Kumuengua mgombea wa Igunga hivi hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigezo vitakavyotumika Kumuengua mgombea wa Igunga hivi hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MgungaMiba, Aug 31, 2011.

 1. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 890
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Kuna vigezo vitano ambavyo CCM wameviandaa kwa kushirikiana na Mrugenzi wa Halmashauri ya Igunga (DED) ambae ndie msimamizi mkuu wa uchaguzi huu na Idara ya Elimu ambayo ndiyo muajiri wagombea huyo Mwl Kashindye kwa ajili ya kumuengua katika kinyang'anyiro kijacho. Hapa vitatajwa vipengele viwili vya kwanza ambavyo ni dhahiri vitamuengua visipofanyiwa kazi mapema, vitatu vilivyobaki havitatajwa hapa kwa sababu havina nguvu kisheria na vimelenga kuwa Character Assasination kwa mgombea huyo ili hata akiteuliwa vitumike kama propaganda material kumuharibia mgombea huyo wakati wa campaign, hivyo si busara kuvitaja hapa kwani itakuwa ni kusaidia kueneza propaganda hiyo Unwittingly.

  1. Kigezo cha kwanza, ikumbukwe kuwa ili mtumishi yeyote wa serikali aweze kugombea ubunge, ni sharti apate kibali kutoka kwa mwajiri wake, ambaye ni serikali kupita idara husika, au achukue likizo ya bila malipo ili endapo akishindwa uchaguzi arejee kazini, au ajiuzulu kazi kabisa, ili akishindwa iwe imekula kwake. Mwl Kashindye baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CHADEMA alianza utaratibu wa kupata idhini ya mwajiri wake, lakini cha kushangaza ni kuwa aliwekewa ngumu kupita kiasi (sidhani kama Dr Kafumu nae kafanyiwa hivyo) ilifika mahali Mwl Kashindye kutaka kujiuzulu, lakini pia ikawa ni mtihani, kwani alitakiwa kutoa notice ya mwezi mzima, kitu ambacho hakingewezekana kutokana na muda uliopo, ikabidi maskini Mwalimu huyo aamue kujiuzulu kwa notice ya 24hrs na alipe mshahara wa mwezi mmoja, ilipofikia hapo, akaagizwa aende mkoani Tabora ili aweze kupata likizo ya bila malipo.

  Alikwenda Tabora na akapatiwa likizo hiyo na barua husika inayothibitisha hivyo. Mpaka hapo kila kitu kwa juujuu kinaonekana kuwa ni sawa, KOSA! Delays alizofanyiwa Mwl Kashindye zilikuwa ni za makusudi na very tactical, kwa maelekezo ya CCM, kwani under normal circumstances hakukuwa na sababu za kufanya hivyo. Wakati akizungushwa hivyo kumbe huku Maexpert wa kuchakachua walikuwa kazini wakidesign mtego utakaofyatuka wakati wa uteuzi ukifika, CCM kupitia mgombea wake itaweka pingamizi Mwl Kashindye asiteuliwe kwa kuwa ni mtumishi wa serkali, yeye atajitetea kuwa amefuata utaratibu wa kuchukua likizo bila malipo na barua yake ndio kielelezo chake, lakini haitasaidia kitu kwa kuwa barua hiyo, ambayo utayarishaji wake ulisimamiwa na wale Maexpert, itapingwa kuwa ina mapungufu mengi hivyo haikidhi haja, kwa hivyo Mwl Kashindye ataendelea kutambulika Kama mtumishi alie kazini bado kwa hiyo atapoteza sifa za kuwa mgombea!

  Kigezo cha pili ambacho kitatumika kumuengua Mwl Kashindye, Kisha mwisho Kama hakutakuwa na interruption yoyote na kama charge itabakia, basi nitasuggest namna ya kupangua, lakini naamini kwa kuanika hadharani njama hizi, basi kutavunja nguvu sana utekelezaji wake.

  2. Kipengele cha pili kitakachotumika kumuengua Mwl Kashindye ni hiki kifuatacho, kwenye form zake za kuwania ubunge alizokwenda kuzichukua kwa Mkurugenzi, kuna kipengele cha udhamini wa chama chake, mbali ya udhamini wa wapiga kura. Kipengele hiki kinatakiwa kujazwa na Katibu wa Wilaya wa chama chake ambacho ni CHADEMA, bila udhamini wa Katbu huyo form hizo zitakuwa hazija kamilika, mgombea ataenguliwa. Sasa kwa Hali ilivyo CCM wilaya ya Igunga imegundua kuwa Katibu wa Wilaya wa CHADEMA, Bw Christopher, hakuchaguliwa kihalali kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, kwa hiyo watapinga uhalali wa yeye kuwa na mandate ya kumdhamini mgombea kwa niaba ya CHADEMA, kwa hiyo mgombea wa CHADEMA itabidi aenguliwe kwa kuwa atakuwa amekosa udhamini wa Afisa wa chama ngazi ya wilaya kama sheria inavyotaka.

  Vipengele hivi viwili visipofanyiwa kazi (Wanasheria wanajua hivyo) hata kimojawapo tu kikipita kinatosha kuleta maafa na kilio, kulalamika na mikwara mingi baada ya mzinga kulia, havitasaidia. Kwa kuwa nachukia dhulma na kupenda haki itendeke, ingawa sina mamlaka yoyote ndani ya CDM, basi naomba tu wanasheria wa CDM waikague vizuri barua ya likizo ya Mgombea, kisha waiangalie zheria inayohusiana na utaratibu wa utoaji wa barua hiyo, kama vile, je, aliesaini barua hiyo Ana mamlaka hayo? Maelezo na mihuri yake inakidhi? Chronological factors zimekaa sawa? Hakuna errors zozote (typing or otherwise) ambazo zinaweza kupotosha maana hivyo kutoa mwanya wa barua hiyo kupingwa uhalali wake?

  Pili, wahakikishe kuwa ni kweli kuwa katibu wa Wilaya wa CDM Bw Christopher hakuchaguliwa katika nafasi yake kwa mujibu wa katiba ya CDM, kama ndivyo, je ni utaratibu gani ulitumika wa kumuinstall, je document zilizomuhalalisha zipo na zipo valid hadi sasa?Kila ilivyo, wanasheria wazipuuze hata chembe ya factor yoyote inayoweza kutumiwa kumkwamisha mgombea, otherwise muda hautatosha kujitetea mahakamani kama ilivyokuwa kwa Wenje kule Mwanza, uchaguzi ule ulikuwa wa miezi mitatu lakini huu utakuwa wa wiki tatu tu, mahakama ikimaliza kusikiliza rufaa kabla haijatoa uamuzi uchaguzi utakuwa umekwisha, ngoma itabidi ije ianze upya!

  MIBA YA MGUNGA HAIUCHOMI MGUNGA!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haya sasa si madogo; well siasa ni mikakati; we have said it others have said it before. Huwezi kuombea ushindi kwenye siasa, unautengeneza.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hilo lisikusumbue. CCM haiwezi kutaka mgombea wa CUF au CHADEMA atoke kwenye race kwa sababu uwepo wao ni fursa zaidi kwa CCM. Actually CCM inataka kuwe na wagombea zaidi wa upinzani.
  CCM ina kura zake fixed na inahitaji kudig kidogo kwa undecided voters ili ishinde. Tatizo ni kwamba undecided huwa wanalearn upinzani without specific party affiliation, kwahiyo kadri wapinzani wanavyoongezeka ndio ushindi wa CCM percentage wise unavyozidi kunona.

  Katika uchaguzi huu CCM itatumia taaluma za siasa na uchaguzi. Planning ya ufunguzi wa kampeni inaonyesha jinsi uchaguzi huu utakavyokuwa sophisticated. Kama Mkapa aliweza kumuweka sawa Seif Shariff Hamad, hawezi kushindwa kuwaweka sawa ring leaders wa Igunga.
   
 4. n

  njaaka Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zemarcopolo hujaeleweka. Mada ipo very open. Eleza ueleweke.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  hopefully concerns zako zitafanyiwa kazi. ila usitegemee ccm kuona aibu kwa sababu mbinu zao zimewekwa wazi, CCM HAINA AIBU! dhambi inaleta usugu!
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Aug 31, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli, CCM ni mashetani!
   
 7. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Likizo bila Malipo kwa mtumishi wa Umma hutolewa na Katibu Mkuu UTUMISHI, yeye tu ndiye mwenye madaraka hayo sasa kama hyo barua ilitolewa na maafisa wa serikali huko Tabora basi kuna makosa na ni vyema suala hili lifanyiwe kazi mapema.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  makatibu kwenye vyama nao wanachaguliwa? Hawa siyo watendaji ambao wanapaswa kuteuliwa na vikao husika?.......................just wondering aloud.................................sina katiba ya chadema kusoma haya majibu ya maswali elekezi............
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  well, sina hakika kama CDM itashinda.........uchaguzi wa igunga sio mgumu ila gamba CCM ndo tatizo pale.
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280

  nilelewavyo ni kuwa ukishajaza fomu ya kugombea uongozi kupitia chama chochoe moja kwa zote umepoteza ajira kwenye taasisis yoyote ya umma..............na kama hili ni kweli hizo hoja zote ulizozitoa hazina msingi.................kwa kuongezea tu ni kuwa ajira ni hiari huhitaji kibali cha mwajiri kuthibitisha kuwa wewe siyo mwajiriwa.................tarehe ile ambayo umwemwandikia barua ya kuwa siyo mtumishi wake ndiyo inatambuliwa kisheria ya kuwa utumishi wako umekoma......................................................hili ina uhakika nalo na hivyo kufanya hoja hii kukosa makalio...................achilia mbali mashiko......................
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  hoja hii sanasana yaweza kuchelewesha uchaguzi wa Igunga kwa vile ni mahakama tu ndicho chombo chenye mamlaka ya kutengua ajira ya huyo katibu si NEC au msajili wa vyama mwenye mamlaka hayo au kutafsiri kama ajira yake imezingatia sheria.....................kwa hiyo malalamiko ya ccm kama yapo yapaswa kupelekwa mahakamani......................na kama hili likifanyika inamaanisha uchaguzi kwanza yabidi uahirishwe...................who loses if the election is postponed? tough question.................................the winner is the major casualty................
   
 12. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Naona Chadema wameshaanza kujishuku!
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hiyo mbona sasa inakuwa kinyume cha katiba kwa nini serikali au muajiri mwingine yeyote ang'ang'anie kukuajiri wakati wewe hutaki??????
   
 14. D

  Derimto JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tafadhalini viongozi wa Chadema haya mambo yasipuuzwe hata kidogo yashughulikiwe haraka kwa ngazi ya kitaifa na mgombea apate muda wa kupumzika na kujipanga na kuwaandaa wapiga kura wake kwa ushindi mnono na siyo kuanza kukimbizana na barua za likizo .
   
 15. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Penye rangi, mbona soft copy ya Katiba nzima ipo kwenye website ya CHADEMA! Kiurahisi google "Katiba ya CHADEMA", then nenda kwenye uongozi wa wilaya.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa katiba ya chadema katibu wa wilaya anachaguliwa na mkutano mkuu wa wilaya, lakini pia anaweza kuteuliwa kutokana na mazingira ama sababu fulani.
   
 17. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Toa ma-propaganda yako ya kitoto hapa... vigezo na masharti vimezingatiwa mara fomu ya katibu ajaze katibu wilaya IMEJAZWA zen oh hajachaguliwa kwa mujibu wa katiba ya chadema so kachaguliwa kwa mujibu wa katiba ya magamba...
  pia we mzushi twenty four hour kuacha kazi ndio sheria ya kazi inavyosema mara umezusha likizo bila malipo wakati aliakuwa umesema karudisha mshahara ACHA PROPAGANDA ZISIZO NA MANTIKI MGOMBEA WETU KISHAPEWA NA HATI YA KUGOMBEA kula kona NGAMBA
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kama malaria sugu vile kuandika mengi pontless anyway utajivua sana magamba mpaka majina lakini wapi
   
 19. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndio tufauti ya chadema na CCM , sie chadema tunaomba nyie CCM mnatengeneza huo ushindi...
  Nguvu ya umma haitengenezwi.... vipi umeshawatengenezea huo mkakati hao magamba? mtaiba kura ngapi? malori mangapi na vituo hewa vingapi? TUNAKUJA IGUNGU KULINDA KULA kwa nguvu ya umma ulizia Mwanza, Ubungo na Kawe wanakuambia hao wenzio wanamkakati
   
 20. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mmmm kweli CDM washindwe kubaini hilo.Nakukumbusha sakata la kutunga la mbunge wa mwanza.Alienguliwa na jamaa akatangazwa anampinzani lakini haki ikapatikana mahakamani.Hoja zaifu saana
   
Loading...