Vigezo vinavyotumika kubainisha viashiria vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Athari ya vitendo vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu ni pamoja na upotevu wa fedha za umma, wananchi kutokuwa na imani na serikali yao, kukosekana kwa utawala bora, uvurugaji wa bei ya soko kwa bidhaa mbalimbali na kupelekea wananchi kukosa huduma bora za kijamii.

Katika Uchambuzi wa ripoti za CAG, yapo maeneo ambayo huonesha uwepo wa viashiria vya Rushwa, Udanganyifu na Ubadhirifu ikiwemo Mapato kutopelekwa Benki.

Pia, Kukosekana kwa Hati za Malipo, kutumia Hundi ya malipo iliyoghushiwa, kwenda kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu za manunuzi na ulipaji Fedha za Umma, na kupokea huduma au bidhaa kwa udhibitisho wa uongo.

Malipo kwa Watumishi hewa, Matumizi mabaya ya nafasi au Cheo katika kufanya maamuzi ya ya makusanyo na matumizi ya Fedha za Umma pamoja na Malipo ya huduma au bishaa ambazo hazijatolewa au hazijapokelewa.
 
Back
Top Bottom