Vigezo gani niangalie kupata mwanamke wa maisha?

jameszejie

Member
Jun 26, 2016
17
3
Hello wana JF,

Natumaini mko poa na tunaendelea kusapotiana kwenye mambo ya msingi, naombeni ushauri.Nilishakuwa na girlfriend mmoja ambaye nilitumaini anaweza kuja kuwa mke wangu kwa maana nilimpenda sana kutokana na ukarimu na upendo alionionyesha kwa muda huo ingawa kwa upande wangu sikuwa najali sana kwa kuwa nilikuwa bado na mawazo ya kitoto japo nilimzidi girlfriend wangu huyo kwa mwaka mmoja.

Ilifika kipindi akabadilika na mwishowe tukaachana lakini kwa sasa nimekaa na kufikiria kama nitaweza kupata girlfriend ambaye anaweza kuwa na tabia chanya kama za yule wa mwanzo. Wote naona hatuendani kwa kila kitu japo wananipenda na mara nyingi nakumbuka vitendo na hata tabia za yule wa mwanzo ila nashindwa kumrudia kwa sababu kwao ni mbali pia ameshakua na mahusiano mengine

Sasa naomba ushauri niangalie vigezo gani muhimu ili nisijeumizwa kwenye mahusiano kwa sababu napenda nianze mahusiano sasa ili yanifikishe kwenye ndoa.

Msaada wenu please!
 
Tabia hujenga, na ukijaribu kumtafuta tena utajiumiza buree, maana yeye ameshasahau na atokuwa na mapenzi ya kweli kama mwanzo, endelea kumtafuta mpya, natumai wapo wengi wanaofaa.
 
Wakati ukitafuta usitafute kwa kufananisha na yule Wa mwanzo itakuathiri.

Tafuta mtu smart tuu mcha Mungu Wa kweli, mnyenyekevu , muelewa, msikivu....mengineyo unaweza kumbadilisha the way you want to her be.....

N.b asiwe mpenda miamala ya pesa
 
Search for your standard, the one who fits u is the better one
 
Wanawake ni kama nyanya za sokoni unainunua kwa kuiona nzuri ukifika nyumbani imesha toa maji,jaribu kubahatisha kwa kuangalia tabia kama unapenda umbo na sura ongezea hapo lakini msome mapema maana viumbe hawa hawaeleweki wanahitaji akili na uvumilivu vinginevyo utabadili mpaka utachoka
 
Cha msingi ni kuingia kwanza kwenye mapenzi na kufahamu tabia zao utakao kuwa nao.

Ni ngumu sana kumjua mtu na tabia zake ukiwa nje ya mahusiano naye, ila ukishaingia tu ndani unakuta hola.

Kama umri bado unaruhusu we endelea kuwa na wengi, one day utabahatisha mmoja mzuri.
 
Hello wana JF,

Natumaini mko poa na tunaendelea kusapotiana kwenye mambo ya msingi, naombeni ushauri.Nilishakuwa na girlfriend mmoja ambaye nilitumaini anaweza kuja kuwa mke wangu kwa maana nilimpenda sana kutokana na ukarimu na upendo alionionyesha kwa muda huo ingawa kwa upande wangu sikuwa najali sana kwa kuwa nilikuwa bado na mawazo ya kitoto japo nilimzidi girlfriend wangu huyo kwa mwaka mmoja.

Ilifika kipindi akabadilika na mwishowe tukaachana lakini kwa sasa nimekaa na kufikiria kama nitaweza kupata girlfriend ambaye anaweza kuwa na tabia chanya kama za yule wa mwanzo. Wote naona hatuendani kwa kila kitu japo wananipenda na mara nyingi nakumbuka vitendo na hata tabia za yule wa mwanzo ila nashindwa kumrudia kwa sababu kwao ni mbali pia ameshakua na mahusiano mengine

Sasa naomba ushauri niangalie vigezo gani muhimu ili nisijeumizwa kwenye mahusiano kwa sababu napenda nianze mahusiano sasa ili yanifikishe kwenye ndoa.

Msaada wenu please!

sali sana na kumuomba Mungu then ombi lako litajibiwa
 
Ewe mwanaume ukioa mwanamke:

Mrefu, jua kwamba utaoa mwanamke mpenda maendeleo, mchapa kazi na mkarimu ila hawajui mapenzi na ni wavivu kujiweka safi kimazingira.

Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaoa mwanamke mchangamfu na mpenda elimu sana ila tu wanapenda mnongono na hawaridhiki.

Mfupi kabisa.Jua ya kwamba utaoa mwanamke msikivu na mcha Mungu ila ni waroho kwa kula na wabishi sana.
Ewe mwanamke ukiolewa na mwanaume:

Mrefu, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye upendo, utu na ubinadamu ila ni wabahili mno na hawapendi kupendeza.

Mfupi kiasi, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwenye fikra na akili timamu za maendeleo, mbunifu, mcheshi na fundi wa mahaba ila ni wapenda ushirikina sana, wana wivu na wambea sana na mara nyingi hupenda kupiga chabo kwa watu wanaofanya mapenzi.

Mfupi kabisa, jua ya kwamba utaolewa na mwanaume mwaminifu, msikivu, mnyenyekevu ila huwa wepesi wa kujiua, kukata tamaa upesi, wanawivu sana na hawapendi kuoga.
Nawatakieni kila la kheri wale wenye wapenzi na ambao mnajiandaa kuoa au kuoelewa ila zingatia sana tabia hizo hapo juu za huyo unayetegemea kufunga nae pingu za maisha ili usije kutusumbua baadae. Chukueni tahadhari!
Hello wana JF,

Natumaini mko poa na tunaendelea kusapotiana kwenye mambo ya msingi, naombeni ushauri.Nilishakuwa na girlfriend mmoja ambaye nilitumaini anaweza kuja kuwa mke wangu kwa maana nilimpenda sana kutokana na ukarimu na upendo alionionyesha kwa muda huo ingawa kwa upande wangu sikuwa najali sana kwa kuwa nilikuwa bado na mawazo ya kitoto japo nilimzidi girlfriend wangu huyo kwa mwaka mmoja.

Ilifika kipindi akabadilika na mwishowe tukaachana lakini kwa sasa nimekaa na kufikiria kama nitaweza kupata girlfriend ambaye anaweza kuwa na tabia chanya kama za yule wa mwanzo. Wote naona hatuendani kwa kila kitu japo wananipenda na mara nyingi nakumbuka vitendo na hata tabia za yule wa mwanzo ila nashindwa kumrudia kwa sababu kwao ni mbali pia ameshakua na mahusiano mengine

Sasa naomba ushauri niangalie vigezo gani muhimu ili nisijeumizwa kwenye mahusiano kwa sababu napenda nianze mahusiano sasa ili yanifikishe kwenye ndoa.

Msaada wenu please!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom