Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,129
- 18,740
Rais ana mamlaka ya kuteua jaji, hilo hakuna anaepinga. Lakini linalotia shaka ni vigezo vinavyotumika hadi Rais kuamua kuteua mtu fulani kuwa jaji. Sasa hili haliwezi kuwa jambo la ksiasa, au hisia tu za Rais kuhusu anampenda nani au hakimu gani kamfurahisha hadi aamue kumteua kuwa jaji. Rais anapaswa kufahamu wazi kwamba uteuzi wa mtu kuwa jaji haupaswi kufanywa bila kuzingatia vigezo vinavyostahili, au kuteua mtu kuwa jaji kama vile kumzawadia kwa jambo fulani alilofanya.
Kama vigezo hivyo havipo basi ni wakati muafaka wa kupigania viwepo ili kumwongoza Rais katika kufanya uteuzi wa majaji. Na kama vipo lakini Rais anavipuuza katika kuteua majaji basi tunapaswa kutafuta namna moja au nyingine kuzuia hili, ikiwezekana hata kada za sheria kuitisha mgomo dhidi ya majaji wanaoteuliwa kimazingaombwe.
Enzi za awamu ya kwanza jaji alikuwa ni mtu mwenye kuheshimika sana, akiwa nje na ndani ya mahakama. Nakumbuka tulivyokuwa tunawaheshimu majaji kama Korosso, Mapigano, Ruhumbika, Maina nk. Siku hizi baadhi ya majaji wanaonekana kama makanjanja tu, yeboyebo, watu walioteuliwa kwa vigezo vyenye kutilia shaka, au pengine hata kutokana na ushabiki wao wa kisiasa.
Tusipokuwa waangalifu na suala hili basi tutaishia kuwa na mfumo wa mahakama Tanzania ambao si tu utakuwa hautoi haki za kisheria bali pia utakuwa ni kichekesho cha ulimwengu. Tutakuwa na taasisi ya sheria ambayo itakuwa inawadharau baadhi ya majaji. Haya ni mambo ambayo wadau wa sheria nchini, pamoja na TLS, wanapaswa kuyapigania kwa kila namna, badala ya kuona gari la sheria nchini linaenda kutumbukia shimoni na kuamua kutofanya lolote kwa kuwa Rais Magufuli hapangiwi na mtu. Huo ni utumwa mamboleo wa kifikra. Magufuli ni Rais wa Tanzania, sio Tanzania ni ya Rais Magufuli. Kama haelewi hili anapaswa kueleweshwa kwa namna moja au nyingine.