Elections 2010 Vigelegele wakati wa kupitisha bajeti ya serikali

Mzee Dogo

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
400
140
Kama mtanzania, ninapitia bajeti ya serikali yetu na ninaona ina mapungufu mengi na ya msingi, nashangaa kuona wabunge 81 tu ndio walioweza kuona mapungufu hayo na kuipinga, wabunge 234 wamepitisha mapungufu hayo tena kwa kupiga vigelegele na kuzomea wale walioipinga. Inasikitisha, lakini ndo viongozi tulionao!
 
wabunge wa ccm majority yao ni wachumia tumbo tu hawana lolote ni mzigo tu kwa walipa kodi
 
Kazi ya vigelegele bungeni ni kazi ya wabunge wa viti maalum ambao pia ni kikwazo kwetu. Mimi sidhani kama kuna mbunge wa kuchaguliwa ,mwenye akili timamu anayeweza kufanya upuuzi ule. kwani mbunge mwenye akili timamu hawezi shangilia hali ya kuwa anajua kuwa wananchi waliompeleka pale wakati yeye anashangilia wao wanalia kilio cha ukweli kuhusu wizi wanaojihalarishia kuwaibia wananchi. hakuna sentensi niliiona kama imetoka kinywani mwa mlevi kama ile ya kusema eti posho zenyewe huishia hapo nje, mbunge akitoka tu anakutana na wananchi wamekuja kuomba, hakika hii ni dharau kubwa kwa wananchi kuwa tumekuwa omba omba ndiyo maana anatetea wao waendelee kuchota posho ili tunapowaomba watupatie. jamani ivi haya ni maneno ya kutoka kinywani mwa msomi? kwa hili ndugu zetu wa dodoma wanatakiwa walipinge kwa nguvu kwa kwenda pale bungeni jamaa aliyetoa kashifa hiyo awataje wananchi waliokwisha mfata pale na kumuomba posho tuone kama milioni yote 5 amewagawia wangapi.haya ni matusi kwa wananchi wote na hasa wana dodoma, maana wabunge mi350 kila mbunge milion5 halafu huwa wanazigawa pale nje ya ukumbi basi wananchi wa dodoma wamesha kuwa matajiri sana. imefika ushabiki ktk isue zinazomuumiza mwananchi tuuache kwani siyo sawa. kama ni msomi ukawa unashabikia kisiasa mambo yanayomuumiza mtanzania wa chini basi unakuwa msomi mjinga.
 
Nafikia hatua ya kuamini kuwa hawa ccm walikuwepo kwa wingi bungeni ili wapitishe mambo ya wakubwa wao tu na si kumwangalia mwananchi aliye kule kwenye vitongoji
 
Mungu anapotaka kumuangamiza mtu au chama basi umnyima maono kwanza, majibu ya upofu huu wa ccm yatapatikana siku si nyingi kutoka sasa.
maana mimi mtaani kwangu sasa hivi wale waswahili ambao walizoea kuja kunipiga mizinga kulipia ada za watoto zao kwenye shule za kata nimeshawapiga stop, na nimewaeleza wazi kwamba Dr Slaa aliahidi elimu bure sasa nyinyi bado mnawapigia kura ccm!

Sasa hii njaa itakapozidi watanzania hawatohitaji tena kuhutubiwa, watachukuwa maamuzi bila hata kushawishiwa,...... mimi binafsi sasa naomba maisha yawe magumu mara 10 kuliko sasa, hiyo ndio njia pekee ya kuwasaidia watanzania kupata akili ya utambuzi.
 
Ndio maana sitachoka kusema kuwa kuitetea CCM kunahitaji ujasiri usio wa kawaida - ujasiri unaotawaliwa na ujinga, unafiki au ulafi. Yaani mtu unapiga vigegele kwa kupitisha bajeti itakayowaongezea maisha magumu wananchi unaowawakilisha. Shame, shame, shame wabunge wa CCM !
 
Mungu anapotaka kumuangamiza mtu au chama basi umnyima maono kwanza, majibu ya upofu huu wa ccm yatapatikana siku si nyingi kutoka sasa.
maana mimi mtaani kwangu sasa hivi wale waswahili ambao walizoea kuja kunipiga mizinga kulipia ada za watoto zao kwenye shule za kata nimeshawapiga stop, na nimewaeleza wazi kwamba Dr Slaa aliahidi elimu bure sasa nyinyi bado mnawapigia kura ccm!

Sasa hii njaa itakapozidi watanzania hawatohitaji tena kuhutubiwa, watachukuwa maamuzi bila hata kushawishiwa,...... mimi binafsi sasa naomba maisha yawe magumu mara 10 kuliko sasa, hiyo ndio njia pekee ya kuwasaidia watanzania kupata akili ya utambuzi.

Mkuu hapo ni sahihi kabisa. Lakini sina imani na waTZ wengi haswa wa vijijini; nahisi kadri wanavyopata shida wanakua mambumbumbu zaidi!!!

This goes up even kwa viongozi wetu haswa rais; ambao kadri nchi inavyopata shida, wenyewe wanafikiri wapi watapata misaada; badala ya kuumiza kichwa namna gani ya kutatua matatizo!!
 
Hao walioikataa jamani majina yanaruhusiwa kuwepo jamvini?wote waliokubali tunawaweka kama maadui wa tz,hasa walioshangilia bajeti kupita
 
jamani tutapataje majina ya waleo walio kuwa wakipiga vigelegele mule bungeni? Tunajua ni wa Viti Maalumu CCM bUT MAJINA YAO PLS WANO WEZA KUTUPATIA.
 
Natangaza rasmi kuwa wabunge wa ccm ni janga na msiba kwa taifa.
.
 
Mungu anapotaka kumuangamiza mtu au chama basi umnyima maono kwanza, majibu ya upofu huu wa ccm yatapatikana siku si nyingi kutoka sasa.maana mimi mtaani kwangu sasa hivi wale waswahili ambao walizoea kuja kunipiga mizinga kulipia ada za watoto zao kwenye shule za kata nimeshawapiga stop, na nimewaeleza wazi kwamba Dr Slaa aliahidi elimu bure sasa nyinyi bado mnawapigia kura ccm!Sasa hii njaa itakapozidi watanzania hawatohitaji tena kuhutubiwa, watachukuwa maamuzi bila hata kushawishiwa,...... mimi binafsi sasa naomba maisha yawe magumu mara 10 kuliko sasa, hiyo ndio njia pekee ya kuwasaidia watanzania kupata akili ya utambuzi.
waambie waende dodoma. Nasikia huko wabunge wanagawa posho kila wakitoka kwenye kikao
 
Ni tanzania tu ndo kuna bunge la kipashikuna watu wanapiga vigeleglee kusherehekea posho kutofutwa hakuna lolote wengi wana madeni waliyokopa wakati wa uchaguzi na kurudisha ni kupitia posho zisizostahili halafu utashangaa CCM kesho watakavyofanya maandamano kuunga mkono bajeti mawe si yapooooo jamani tuwapopoe tu popote watakapoandamana kuunga mkono ushuzi wa bajeti!!
 
Watanzania kazi tunayo kadri siku zinavyoenda ndo nchi inazidi kuporomoka.
 
Maajabu sasa wapipitisha kwa nguvu kubwa, baadae wakaanza kuipinga tena why Exemptions, kama unakumbuka
Mhesh Kange Lugola wa mwibara alilalamika kwamba hatuwezi kumlipia mzungu garama kuja kupanda Mlima K njaro
likewise kwenye Madini. SS Tundu lisu alikuwa amesema misamaha isipite wao wakawa wanashangili imeshakuwa sheria
ndio wanalalamika hii hali ya vigelegele wasubiri tu 2015 ndio mwisho wake.
 
Back
Top Bottom