Vifurushi vya internet 'visivyo rasmi' kwa makampuni ya simu

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,421
2,000
Hii ni thread ya vifurushi ambavyo sio rasmi kama vya chuo au vifurushi maalum ambavyo vinatoa kiasi kikubwa cha internet, nitalist vifurushi ninavyovifahamu kama kuna wanaojua vyengine watasaidia

Tigo
Kwa Tigo bonyeza *147*00# kisha chagua size yako, unaweza kupata vifurushi vizuri, Ila njia hii sio reliable kwani vifurushi hivyo hubadilika kila Mara.

Vodacom
Vodacom angalia kwenye ya kwako tu, piga *149*03# kuangalia ofa.

Airtel
[
Halotel
-Royal bundles pengine kifurushi kizuri zaidi kwa Sasa kinakupa dakika takriban 200 na Internet unlimited kwa 0.5mbps kwa mwezi mzima. Ni vyema kwenda ofisi za Halotel na kununua line ya Royal bundle, pia unaweza kukuunga kwa kubonyeza menu yao ya *148*66#

-Mega bundle kwa shilingi 10,000 Unapata GB 15 ambazo unatumia mb 500 kila siku kwa mwezi, kujiunga ni *150*88#, unakiunga na salio la halopesa.

-Kifurushi Cha usiku kwa 1000 unapata Internet unlimited, kizuri kwa ajili ya kudownload files kubwa Kama games na movies. Kujiunga *148*66# kisha vifurushi maalum (ya kwako tu)

vifurushi vya 4G kuendana na line zao mpya za 4G,
1000 unapata GB 1 kwa siku
5000 unapata GB 7 kwa wiki
10,000 unapata GB 10 kwa mwezi.

TTCL
-bandika bandua ni vifurushi vizuri kwa matumizi makubwa Kama kuangalia Netflix, zipo option Kama
-1000 GB 4 kwa siku (Mb 500 mchana 3.5GB usiku)
-2500 GB 10 kwa siku
-5000 GB 8 kwa wiki (3gb mchana na 5GB usiku)
Uzuri wake ni kwamba GB za usiku zinaanza saa 2 usiku muda mzuri ambao watu wanaangalia movies baada ya kutoka makazini.

-Toboa Night navyo ni vifurushi vizuri vya usiku in case Halotel kwako inasumbua ama Haina speed, kwa 500 unapata GB 2 na 1000 unapata GB 10.

Vyote toboa na bandika bandua unajiunga kwa kubonyeza *148*30# kisha TTCL bundles.

-Ofa maalum, pia TTCL Wana ofa mbalimbali Kama vile za sabasaba, nanenane etc ambazo wanazieka kwenye option ya vifurushi maalum,

Remote[/B][/B][/B]
 
Masterkratos

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
550
1,000
Ukitoa TTCL sidhani Kama Kuna kwenye vifurushi vizuri vya chuo. Wote wamepunguza.

Hivi kuna mtandao unaotoa true unlimited kama nchi nyingine ambapo unatumia utakavyo ukilipia kiasi flani. Kwasababu naona hii mitandao inatufanya watanzania wajinga, unakuta kuna vifurushi vya mwezi hadi vya 100000 lakini unakuta GB 40 . Wakati nchi nyingine watu wanalipa 50000 kwa mwezi anapata unlimited @ 6Mbps. Halafu eti wanatuambia Tanzania ni nchi yenye bei nafuu data.
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,421
2,000
Hivi kuna mtandao unaotoa true unlimited kama nchi nyingine ambapo unatumia utakavyo ukilipia kiasi flani. Kwasababu naona hii mitandao inatufanya watanzania wajinga, unakuta kuna vifurushi vya mwezi hadi vya 100000 lakini unakuta GB 40 . Wakati nchi nyingine watu wanalipa 50000 kwa mwezi anapata unlimited @ 6Mbps. Halafu eti wanatuambia Tanzania ni nchi yenye bei nafuu data.
Mkuu kwenye mobile data Hata huko duniani throttling ipo,

Ukitaka true unlimited ipo kwenye broadband ambayo hupatikana Sana mjini, around 70K unapata 10mbps kwa Tanzania.

TTCL Wana nduki ambayo hupatikana Hata maeneo yasiyo katikati ya jiji sema Bei na speed haviendani.
 
Arien

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
10,052

Ni unlimited?!
 
Bujoro

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,898
2,000
Njoo halotel ni unlimited aisee kuna vifurushi vya Royal unajiunga kwa 10k mwzi mzima dakika za mitandao yote na halotel , sms kama zote na internet bila kipimo wala kikomo mwezi mzima. Unaingia kila mtandao wa kijamii bila kulimitiwa sjui youtube unawezxa hata shida youtu.be unastream mamuvi na udaku insta ni wewe tu acha kujitesa wote voda tushaikimbia mda. Voda kwangu ipo hewani kwa ajili ya kuokea wanaopiga tu sio niweke salio no narudia tena noooo.
Hivi kuna mtandao unaotoa true unlimited kama nchi nyingine ambapo unatumia utakavyo ukilipia kiasi flani. Kwasababu naona hii mitandao inatufanya watanzania wajinga, unakuta kuna vifurushi vya mwezi hadi vya 100000 lakini unakuta GB 40 . Wakati nchi nyingine watu wanalipa 50000 kwa mwezi anapata unlimited @ 6Mbps. Halafu eti wanatuambia Tanzania ni nchi yenye bei nafuu data.
 
Arien

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
10,052
2,000
Njoo halotel ni unlimited aisee kuna vifurushi vya Royal unajiunga kwa 10k mwzi mzima dakika za mitandao yote na halotel , sms kama zote na internet bila kipimo wala kikomo mwezi mzima. Unaingia kila mtandao wa kijamii bila kulimitiwa sjui youtube unawezxa hata shida youtu.be unastream mamuvi na udaku insta ni wewe tu acha kujitesa wote voda tushaikimbia mda. Voda kwangu ipo hewani kwa ajili ya kuokea wanaopiga tu sio niweke salio no narudia tena noooo.
Hivi hizo Royal bundle ni unlimited kweli?
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,421
2,000
JIBU NI HAPANA UO JAMAA ANAPOTOSHA AKITAKA KUONA KUA SIO UNLIMITE AJARIBU KUINGIA TORRENT KU DOWNLOAD MIZIGO
Na huu ndio wasiwasi wangu
Ni unlimited nakitumia muda mrefu (nipo mwezi wa tatu Sasa), sema speed ni around 60KBps ukimaliza GB zako, ambayo ni Kama 0.5mbps.

Kwa matumizi ya simu kuingia FB, YouTube, WhatsApp, kubrowse JF kinafaa.

Au Kama unatumia kudownload tafuta computer isio na kazi muda wote maana hizo movies na magame vinachukua masaa Kama sio siku kadhaa, kwa masaa 24 unaweza shusha movie Kama 3 za HD.

Au Kama una simu unastream tumia website zenye movie za low quality Kama 240p.
 
Alaa kumbe! Kimenikumbusha kile cha voda unlimited kipindi kile.. Series nzima una download wiki nzima!!
Kwa YouTube unaweza angalia video za hd?
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,421
2,000
Alaa kumbe! Kimenikumbusha kile cha voda unlimited kipindi kile.. Series nzima una download wiki nzima!!
Kwa YouTube unaweza angalia video za hd?
Hapana YouTube ni 240p, sema Kama una browser ya kisasa ukiangalia video za chanell maarufu utaona kwa 360p. Kwa HD utahitaji angalau 2Mbps.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom