Vifurushi vya internet: Ina maana Watanzania tumechezewa akili?

BoManganese

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
979
2,670
Nawasalimu wanajukwaa wote kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pia nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukifu wa Ramadhani.

Niende moja kwa moja kwenye topic, lengo la uzi huu ni kuhusu hili suala zima la vifurushi au mabando katika mitandao ya simu.

Kama tunakumbuka kuna kipindi kulitokea vuguvugu ambapo wananchi walikuwa wakilalamikia bei kwa ya vifurushi hususa ni katika bando za internet.

Hali hii ilipelekea hadi wizara ya habari na mawasiliano kupitia naibu waziri wa wizara hiyo Dr Faustine Ndungulile kutoa tamko kwa Watanzania kuwa tatizo hilo la bei kubwa la vifurushi vya internet litashughulikiwa na mambo yatakuwa shwari.

Ndipo wizara ya habari na mawasiliano pamoja na mamlaka ya mawasiliano Tanzania wakafanya michakato wao na kutoa agizo kwa makampuni ya mitandao ya simu ifikapo 1 April 2021 mabadiliko yafanyike katika hivyo vifurushi vinavyo lalamikiwa na wananchi, hapo Watanzania wakapata matumaini kuwa mambo yanakwenda kuwa sawa sanasana kwenye hizi bando za internet.

Cha kushangaza kama sio kusikitisha ilipo wadia hiyo tar 1 April 2021, mabadiliko yalitokea lakini isivyo tarajiwa bei ya vifurushi hasa vya internet ilipanda zaidi ikawa bora ile ya awali.

Hii ilipelekea Wananchi kulalamika zaidi kwanini bei ipande zaidi wakati hata ile ya mwanzoni ilionekana kuwa juu baada ya malalamiko mengi ndipo wizara ya mawasiliano pamoja na TCRA wakatoa tena tamko la kusikitisha bei hii mpya ya vifurushi na kurudisha ile ya awali.

Hapa sasa ndio wananchi wanaona afadhali wengine wakilalamika kuwa bado baadhi ya mitandao ya simu haijarudisha ile bei ya awali na Mh Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan akasema hili tatizo la vifurushi lisijirudie tena.

KUCHEZEWA AKILI KUNAKUJAJE SASA.

Hapa sasa kama Watanzania wenzangu sijui mtakuwa mmebaini kuwa kuna kadana dana fulani tumepigiwa yaani mwanzo tulidai kuwa bei ya vifurushi ni kubwa, serikali ikatoa tamko baada ya muda bei ikapanda maradafu Wananchi tukalalamika, serikali ikatoa tena tamko bei ya vifurushi irudi ile ya mwanzo, wananchi tukashusha pumzi tukaona afadhali yaani tumesahau kuwa hii bei ya vifurushi iliyo rudishwa ndio tulio kuwa tukalalamikia mwanzoni kuwa ni kubwa, hii trick ya dark psychology, manipulation and NLP wataalamu wa saikolojia watanisaidia hii mbinu kitaalamu inaitwaje.

Yaani kwa mfano rahisi hapa ni sawa na mteja kaenda dukani kununua viatu muuzaji amwambia bei ya viatu ni elfu 10 mteja akalalamika kuwa bei ni kubwa muuzaji akasema basi nitakuuzia elfu 30 mteja akalalamika mbona bei ni kubwa zaidi muuzaji akasema basi nipe elfu 10 sasa mteja anaona fadhali kulipa elfu 10 na kusahau kuwa elfu 10 ndio bei ya mwanzo aliyoiona ni kubwa, kwa kweli inafurahisha sana.

Yangu ni hayo tu.
 
Inasikitisha. Wito wa pamoja kusitisha kununua bando kutatuokoa.

Hapa tunahitaji sitisho rasmi la siku 3 -7 akili mbona itawakaa sawa.

Binafsi nimeacha kununua bando za internet. Nimefika hapa leo shukurani kwa vile vinavyoitwa vi bonus tokea kwenye vifurushi cha maongezi.

Nchi imeendelea kuchezewa sana. Tusiruhusu na sisi kuendelea kuchezewa.
 
Wiki na mwezi ...
Screenshot_2021-04-15-11-12-21.jpeg
Screenshot_2021-04-15-11-12-26.jpeg
Screenshot_2021-04-15-11-12-55.jpeg
Screenshot_2021-04-15-11-13-07.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_2021-04-15-11-13-07.jpeg
    Screenshot_2021-04-15-11-13-07.jpeg
    20.5 KB · Views: 1
Hakuna anayelia ila sema hujaelewa content ya thread

Mentality za mamburula kama unazoziona ndizo zinazo zinazotufanywa kuongozewa nchi kama shamba la bibi.

Binafsi nimejitoa no marekebisho kwenye bei za bando = sinunui tena bando.

Ukhanithi wa nini?
 
Nawasalimu wanajukwaa wote kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pia nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukifu wa Ramadhani.

Niende moja kwa moja kwenye topic, lengo la uzi huu ni kuhusu hili suala zima la vifurushi au mabando katika mitandao ya simu.

Kama tunakumbuka kuna kipindi kulitokea vuguvugu ambapo wananchi walikuwa wakilalamikia bei kwa ya vifurushi hususa ni katika bando za internet.

Hali hii ilipelekea hadi wizara ya habari na mawasiliano kupitia naibu waziri wa wizara hiyo Dr Faustine Ndungulile kutoa tamko kwa Watanzania kuwa tatizo hilo la bei kubwa la vifurushi vya internet litashughulikiwa na mambo yatakuwa shwari.

Ndipo wizara ya habari na mawasiliano pamoja na mamlaka ya mawasiliano Tanzania wakafanya michakato wao na kutoa agizo kwa makampuni ya mitandao ya simu ifikapo 1 April 2021 mabadiliko yafanyike katika hivyo vifurushi vinavyo lalamikiwa na wananchi, hapo Watanzania wakapata matumaini kuwa mambo yanakwenda kuwa sawa sanasana kwenye hizi bando za internet.

Cha kushangaza kama sio kusikitisha ilipo wadia hiyo tar 1 April 2021, mabadiliko yalitokea lakini isivyo tarajiwa bei ya vifurushi hasa vya internet ilipanda zaidi ikawa bora ile ya awali.

Hii ilipelekea Wananchi kulalamika zaidi kwanini bei ipande zaidi wakati hata ile ya mwanzoni ilionekana kuwa juu baada ya malalamiko mengi ndipo wizara ya mawasiliano pamoja na TCRA wakatoa tena tamko la kusikitisha bei hii mpya ya vifurushi na kurudisha ile ya awali.

Hapa sasa ndio wananchi wanaona afadhali wengine wakilalamika kuwa bado baadhi ya mitandao ya simu haijarudisha ile bei ya awali na Mh Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan akasema hili tatizo la vifurushi lisijirudie tena.

KUCHEZEWA AKILI KUNAKUJAJE SASA.

Hapa sasa kama Watanzania wenzangu sijui mtakuwa mmebaini kuwa kuna kadana dana fulani tumepigiwa yaani mwanzo tulidai kuwa bei ya vifurushi ni kubwa, serikali ikatoa tamko baada ya muda bei ikapanda maradafu Wananchi tukalalamika, serikali ikatoa tena tamko bei ya vifurushi irudi ile ya mwanzo, wananchi tukashusha pumzi tukaona afadhali yaani tumesahau kuwa hii bei ya vifurushi iliyo rudishwa ndio tulio kuwa tukalalamikia mwanzoni kuwa ni kubwa, hii trick ya dark psychology, manipulation and NLP wataalamu wa saikolojia watanisaidia hii mbinu kitaalamu inaitwaje.

Yaani kwa mfano rahisi hapa ni sawa na mteja kaenda dukani kununua viatu muuzaji amwambia bei ya viatu ni elfu 10 mteja akalalamika kuwa bei ni kubwa muuzaji akasema basi nitakuuzia elfu 30 mteja akalalamika mbona bei ni kubwa zaidi muuzaji akasema basi nipe elfu 10 sasa mteja anaona fadhali kulipa elfu 10 na kusahau kuwa elfu 10 ndio bei ya mwanzo aliyoiona ni kubwa, kwa kweli inafurahisha sana.

Yangu ni hayo tu.
Ulitaka tufanye nn
 
Mentality za mamburula kama unazoIona ndizo zinazo zinazotufanywa kuongozewa nchi kama shamba la bibi.

Binafsi nimejitoa no marekebisho kwenye bei za bando = sinunui tena bando.

Ukhanithi wa nini?
Sure mkuu aina ya watu kama huyo jamaa ndio mtaji mzuri sana kwa wapigaji, Ufaransa kuna miaka damu zilimwagika baada ya serikali kupandisha bei ya mikate
 
Basi wenye hizo 'akili' ndo wanakuchezeeni.

Si useme tu, wanakuchezea wewe na wenzio kina msukuma mkuu?

Wengine tulishatafakari na kuchukua hatua.

Tangu lini darasa la saba akajidhania ni bora kuliko profesa na bado akashangiliwa?
 
Back
Top Bottom