Vifurushi vya Azam tv sio rafiki kwa maskini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,214
2,000
Ni watu wasiokuwa na sh. 28,000 kwa pamoja (maskini) kwa mwezi ambao watalazimika kulipia vifurushi vya wiki kama vile sh. 9,000 ili waweze kuangalia channels pendwa kwao.

Wiki moja ina siku 7 na mwezi mmoja una siku 30. Hivyo basi anaelipa 28,000 kupata kifurushi cha mwezi (tajiri) anatumia 28,000÷30 kwa siku ambayo in sh. 933.3 kwa siku, lakini anaelipa sh. 9,000 kwa wiki (maskini) atalipia sh. 9,000÷7 = 1,285.7 yaani sh 1,285 kila siku.

Hivyo wale masikini wanaolazimika kulipia vifurushi vya wiki huwa wanalipa zaidi kuliko matajiri wanaolipa vifurushi kwa mwezi. Maana yake Azam tv inapenda wenye nacho zaidi kuliko mafukara.

Kwanini sh. 28,000 zisigawanywe kwa 4 ili kujua vifurushi cha wiki kiwe bai gani? Yaani vifurushi cha siku saba kilitakiwa kiuzwe kwa sh. 933 × 7 = 650 kwa wiki.
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,177
2,000
Hata kwenye biashara ukitaka faida chukua mzigo wa jumla reja reja zinakata. Hata voda tu vifurushi vya SMS kwa wiki ni buku lakini kwa mwezi ni 2000 sasa utaamua kuchukua kifurushi cha mwezi au cha wiki wiki.

Kule startimes kifurushi cha juu ni 36000 ambacho kama ukiamua kulipa kwa siku moja ni 3600 sasa chaguo ni lako kama utalipa kwa siku siku ndani ya mwezi unajikuta umelipa zaidi ya laki.
 

wa ukae

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
1,778
2,000
Vifurushi vya Azam TV vikasome kwa vifurushi vya tiGO, ni hatari kwa matumizi ya binaadamu.

Eti Shillingi 3,000/= unapata GB 1 na madakika kibao ya usiku wa manane kama mwanga. Si ujangili huu???
Ahaaaaa ahaaaa Mkuu kwa kweli nimecheka sana hivi vifurushi vya kupiga cm usiku huwa vinawalenga watu wanamna gani haswa?
 

Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,324
2,000
Nchi ya uchumi wa Kati unalalamika kulipa 28,000 ambayo Ni sawa na Dolla 16.


Azam pandisheni Bei Hadi ifike 100,000 kwa mwezi tuko vizuri.


Nasema uongo ndugu zangu
 

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
694
1,000
Kama mtu anamiliki dishi la Azam,huyu so maskini.

Na Kama unashindwa kulipa kifurushi Cha Bei ya 28,000/-wewe hukufikia kumiliki king'amuzi.

Acheni mambo ya kuiga,au kwakuwa mtaa mzima wamefunga madish ukaona na wewe usipitwe,

Tafuta pesa Kwanza vitu vizuri vina gharama zake,Kuna watu wamefunga ving'amuzi zaidi ya vitatu aina tofauti tofauti,
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,214
2,000
TV ni kwaajili ya tajiri
Kule kijijini tofali la kujengea la kuchoma ni sh. 90 hadi 100, maskini anaenunua kifurush cha sh. 9,000 kwa wiki ni sawa na angenunua matoli 13 kila siku sawa na matofali 390 kwa mwezi ambayo ni sawa na matofali ya kuchoma 4,680 kwa mwaka ambayo yangekamilisha ujenzi wa vyumba vyake 3 vya kulala na choo na stoo. Lakini maskini halijui hili na bado ananunua vifurushi vya simu vya halichachi kila siku kuongea yasiyokuwa na tija kwake.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,214
2,000
Ukweli lazima usemwe! Azam ndiyo wana vifurushi vya bei ndogo kuliko wengine! Wanajitahidi kwa kweli!
Hilo halina ubishi lakini kwanini aadhibiwe yule anaelipia kifurushi cha wiki ambae kuna kila dalili kuwa ni yule ambae amekosa sh. 28,000 sio kwa makusudi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom