Vifungashio vya plastiki visivyo na nembo ya TBS visitumike kuanzia leo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema vifungashio vinavyotokana na malighafi ya plastiki na ambavyo havina nembo ya Shirika la Viwango (TBS), haviruhuwi kutumika kuanzia leo.

Jana, Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Nancy Nyenga, aliiambia Nipashe kwamba, kwa kiwanda kitakachozalisha vifungashio hivyo, kitatozwa faini ya Sh. milioni 20 na isiyozidi Sh. bilioni moja au kifungo cha miaka miwili jela au adhabu zote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo wa NEMC, vifungashio vinavyolengwa ni pamoja na vinavyotumika kufungasha ubuyu, barafu na vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS.

Akizungumzia marufuku hiyo, alisema vifungashio vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS, havitaruhusiwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu, yaani leo, kwa kuwa serikali imeshapiga marufuku na kuelekeza vifungashio vinavyoruhusiwa.
 
Ewe mama muuza ubuyu wa pakiti shilingi mia kwenye pakiti za mifuko ya plastiki, unasemaje? Five again au bado bado?
 
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limesema vifungashio vinavyotokana na malighafi ya plastiki na ambavyo havina nembo ya Shirika la Viwango (TBS), haviruhuwi kutumika kuanzia leo.

Jana, Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Nancy Nyenga, aliiambia Nipashe kwamba, kwa kiwanda kitakachozalisha vifungashio hivyo, kitatozwa faini ya Sh. milioni 20 na isiyozidi Sh. bilioni moja au kifungo cha miaka miwili jela au adhabu zote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo wa NEMC, vifungashio vinavyolengwa ni pamoja na vinavyotumika kufungasha ubuyu, barafu na vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS.

Akizungumzia marufuku hiyo, alisema vifungashio vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS, havitaruhusiwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu, yaani leo, kwa kuwa serikali imeshapiga marufuku na kuelekeza vifungashio vinavyoruhusiwa.

Duuuuh je vitapatikana kwa bei nafuu au majanga tena
 
Watu wamejiajiri wanapata ridhiki kupitia hivyo vifungashio visivyo na nembo ya TBS

Wauza Barafu, miwa, ubuyu ,karanga mnawaweka wapi?

Baadala ya kuwapa elimu ya kutunza mazingira ndio mnataka kuwadidimiza kwenye umasikini.
 
Yaani ishu ni nembo tu ya TBS kwenye kifungashio au mi ndio sijaelewa ipasavyo!?

Yaani nembo tu!? Ikishakuwepo ndio vinakuwa sahihi kutumika bila kuathiri mazingira!? Huu usomi wenu huu!!!?
 
Five more
Tusiingize siasa kila sehemu

Nemc ingefanya kaZi ya kulinda mazingira na binadamu hata kama chams cha ubwabwa ningekua madarakani

Sometimes tunataka regulations za kulinda walaji, and sometimes hatutaki

Chifu ... This shouldn't have come from you
 
Viko salama?
 
Huoni tunaelekea overregulations?

Wakati Bank zinakaribia Ku collpase..
Wafanyabiashara wanapigwa na new regulations juu??Huoni impact yake kiuchumi?
 
Hawa watu awa serikali wanafanyaga maamuzi kama wanaishi sayari nyingne
 
Mheshimiwa Kessy Hili Jambo Lako Kaa Nalo Moyoni
Tukirudi Ulilete Wewe Mwenyewe Hapa Bunge
Tulipitishe, Atawale Milele Daima!!
By Job Ndugai!!!
 
Yaani ishu ni nembo tu ya TBS kwenye kifungashio au mi ndio sijaelewa ipasavyo!?

Yaani nembo tu!? Ikishakuwepo ndio vinakuwa sahihi kutumika bila kuathiri mazingira!? Huu usomi wenu huu!!!?

Ni kichekesho cha mwaka mpya kifungashio kina nembo ya tbs lkn bidhaa ya ndani haina tbs...
 
Tusiingize siasa kila sehemu

Nemc ingefanya kaZi ya kulinda mazingira na binadamu hata kama chams cha ubwabwa ningekua madarakani

Sometimes tunataka regulations za kulinda walaji, and sometimes hatutaki

Chifu ... This shouldn't have come from you
Unatenganisha vipi maamuzi ya taifa na siasa??? Wanaotengeneza na kupitisha regulations ni wakina nani?
 
Back
Top Bottom