Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 948
- 1,092
Habari Tanzania !
Naomba kutoa ushauri, mawazo na mchango wangu kwa wale wote wapenda mazingira mazuri, afya ya mwili na maisha, ubora wa ardhi na maendeleo kwa taifa.
1. Vifungashio vya plastiki
Fursa hapa ni kuchakata vifungashio vya plastiki vilivyotumika kuwa bidhaa ambayo ni nzuri na rafiki kwa maisha na mazingira.
Mfano; unaweza tengeneza mtambo wa kuyeyusha hizo plastiki na ukatengeneza bidhaa mfanano wa matofali, paveti (urembo wa nyumba), vigae vya maofisini au majumbani mwishoe tutayaokoa mazingira yetu na kuyafanya kuwa bora zaidi.
2. Vifungashio vya chupa
Hapa kuna fursa lukuki. Chupa zikisagwa na kuwa unga unaweza zalisha udongo mzuri wa kupandia mimea au mazao mbalimbali na katika hizo chupa kuna kemikali mbolea nzuri sana na pia unaweza ukatengeneza matofali ambayo ni mazuri kwa ujenzi wa nyumba au ofisi.
Mwisho
Tuchukue fursa hii ili tuokoe mazingira yetu na nchi yetu. Tuipende Tanzania na watu wake.
Karibu.