Vifo vya watoto hawa 2 vichunguzwe!

Tanzania ninayoipenda ni uwanja wa fujo. Utawala usiofuata sheria haya ndio mambo yake.

Ningefurahi sana kama wangepigwa wezi mafisadi na kufa sio vibaka wa kanda mbili, kwani hawa mafisadi ndio chanzo cha huu wizi. uchumi ukidorora vibaka huongezeka.

Taarifa kweli inasikitisha, ila inamambo mengi na maswali kibao.
Mwili ulioshambuliwa na watu wenye hasira unajulikana, na mwili uliowawa na watawala wasio na huruma unajulikana.
Tukio lilitokea vipi sioni jibu kwenye habari.

Ila swala la wizi na watu kuchukua sheria mikononi hilo ni la siku nyingi wapo wengi sana wameuwa wakiwa sio wezi.

Ni nani wa kulaumiwa, ni serikali. Niliwahi kukaa jirani na polisi Dar, na siku moja walifukuza majambazi wa magari, kisha wakawauwa. nilimuuliza kwanini mmeuwa hao majambazi hamkuwakamata na kuwapeleka polisi.

Alinijibu hawawezi kufanya opereshini ya kukamata jambazi kama hawauwi kwani huwa wakifika polisi wanaachiwa huru kwa kuhonga wakubwa halafu kisasi kinakuwa ni binafsi kati ya jambazi na polisi waliokamata. Na baadhi ya polisi ni majambazi hivyo hufanya uhalifu na majambazi.

Tanzania bila utawala wa sheria tutapiga kelele vizazi na vizazi.
Ni lazima viongozi na watendaji waoogope sheria, bila hivyo vita hii ambayo imeanza siku itakuwa kubwa.

Kama nchi imeshindwa kulinda BOT kweli wataweza kulinda watoto wenye umri wa miaka 14 na 15??
kama mkuu wa usalama wa taifa alishiriki kuibia nchi anayoilinda akishirikiana na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hatuoni hapa nchi haina walinzi.

Kama mkuu wa polisi alishirikiana na majmbazi ni nini kinatushangaza??

tatizo kubwa Tanzania hakuna wa kumfunga paka kengele.
Nchi haina utaratibu wala mpangilio. Waziri wa mambo ya ndani kazi yake ni kupanga njama za kufilisi wafanya biashara, Raisi kazi yake kulinda mafisadi, waziri mkuu kazi yake haijui yupo yupo tu..........

Tusipo kuwa tayari kuitetea tanzania kwa vitendo kinachokuja ni kikubwa sana.
 
IO....hio ni Old Story....?Unajua kesi zinavyoendeshwa mahakamani....? Hakimu huwa anakuwepo wakati wa tukio?...unaposema Old....unakusudia nini...miaka? siku? masaa..? dakika?....

so CHUKI ATHUMANI sio "ourselves"...sio "our children"

Nimelihusianisha tukio la chuki Athuman kwakuwa wakati Ule Polisi walihusika...ktk Hii Story iliyokuwa pasted na MKJJ....moja ya wazee anasema Polisi wanahusika kwani walikuwa ktk lindo...

So unachotaka mie nikubali ni nini kaka?

Your ideas are simply idiotic..
 
MKJJ....mauaji yoyote yawe ya Mtoto au Mtumzima kwa style ile hayafai...

Sijui kama una kumbukumbu...Polisi waliwapiga Risasi watoto pale Mwembechai(Rejea Mwembecha Killings)...akina Chuki ATHUMAN...wakadai eti waliwakuta na karatasi za uchochezi....Hivi waliwapiga risasi baada ya kuwaona na karatasi hizo...au waliwapiga risasi then wakawakuta na karatasi hizo...

Hapo Hasira zako hazikuwepo?

nilikuwa na hasira wakati ule kama nilivyonao leo. Mimi siyo miongoni mwa watu waliojaribu kufafanua mauaji ya Mwembechai! Nalaani wakati wowote nguvu inapotumika badala ya hekima. Nahoji wakati wowote watawala wanaua raia; siwapi benefit of the doubt! Ndio maana niliohoji mauaji ya wale "majambazi" kule Moshi wakati makundi ya watu waliniona kihoji kwani "majambazi yameuawa".

Watawala wanapotwaa uhai wa mtu, ni lazima tuhoji sana hadi turithidike. Lakini pia wananchi wanapoamua kumuua mtu kwa tuhuma za wizi wanaadhibu siyo sawa na uzito wa kosa. Haiwezekani mtoto akuchomolee halafu adhabu yake iwe kifo!
 
mkjj, sijabahatika kupata kijarida cha wiki hii, tell me how can i find and print, tried at mkjj.com but couldn't find it..plz help.
 
Mimi nikisema ukweli nashambuliwa. Naambiwa ninajichukia. Naambiwa nina low self esteem (sijui hata kwa Kiswahili tafsiri yake ni nini). Naambiwa natukana watu. Naonekana mtu niliyelosti tu, hohehahe nisiye na mafanikio yoyote yale. Naonekana mjinga nisiye na askili. Naitwa degenerate na majina mengine kibao ambayo siwezi hata kuyakumbuka.

Labda kweli hayo yote ninayoambiwa kuhusu mimi ni ya kweli. Mimi sijui. Mwenye kuamini ninayosemaga na aamini. Mwenye kukataa na akatae. Mwenye kufumbia macho ukweli na afumbie na hata akitaka azibe masikio yake. Mwenye kunikasirikia mimi na kuacha kukasirikia matendo haya maovu na anikasirikie. Mimi nasema kile kilichopo na kila ninachokiona. Situngi wala kuzusha kitu. Kwanza mimi sio mtunzi mzuri wa hadithi. Nikiliona jiwe nitakwambia nimeona jiwe. Nikiona mnazi nitasema ule ni mnazi. Nitasema kile macho yangu yanachoona.

Ni hayo tu machache kwa leo.
 
Duh, ndio maana leo snow yote imeyeyuka na miti kuwa kijani ghafla maeneo haya.
 
Ngabu,

Mimi ni mmoja wa wale wanaokubaliana na mengi unayosema hapa....

I am your biggest fan ....... mmmmwwwwaaaa .... mmmmmcccchhhwaaaaa
 
Bangi na empty stomach ni tatizo...
 
Endeleeni tu kunikasirikia mimi Nyani Ngabu. Kwanza ni mtu gani wa maana mwenye akili timamu ajiitaye Nyani? Huyu lazima zitakuwa zimemruka huyu! Na endeleeni tu kutumiana PM zenu za kunisema. Mnafikiri sijui. Nyie endeleeni tu. Endeleeni tu kunicheka. Endeleeni tu. Endeleeni kutuma maombi na malalamiko yenu kwa uongozi wa hapa kunifungia. Nikasirikieni tani yenu, mnavyotaka. Endeleeni tu kunikejeli.

Watu wanauliwa na watu hamkasiriki kama mnavyomkasirikia Nyani. Tunatendewa maovu na hamkasiriki kama mnavyomkasirikia Nyani. Sawa tu. Nyie endeleeni.
 
Ngabu,

Mimi ni mmoja wa wale wanaokubaliana na mengi unayosema hapa....

I am your biggest fan ....... mmmmwwwwaaaa .... mmmmmcccchhhwaaaaa

Aaaaw! Thank you so much! I feel so lonely sometimes. I feel like everybody hates me. Yes, I know I'm hard to deal with but really, I'm a good natured person. Nobody loves me. Nobody listens to me. I just call things as I see them. No need to be complicated. Sorry I'm rambling but I just had to get things off my chest. I hate to see people being mistreated and when you call out the whole society people get mad at you. I'm just mad. Mad at even myself. If I had my way, no one would die violently like that. Everyone would be treated with dignity and respect. But I'm just Nyani, a monkey. What can a monkey possibly do to change the world?
 
Tanzania inachekesha mbaya kabisa. Fikiria hata Tampa Sallon ni bora kuliko Tz. Soma Hii.
Tanzania Loses Name To Tanning-Salon Chain | The Onion - America's Finest News Source.

Ha, ha haaaaa!! Masikini Tanzania. Mpaka jina tunanyang'anywa mchana kweupe, yaani we acha tu !!!.

Lakini on a serious note kuna kitu kiko extremely wrong with our peoples. Kuna mambo yanasemwa juu yetu yanayoweza yakakutoa machozi. Kusema kweli umasikini wetu, unyonge wetu na uzembe wetu - vyote vinatokana na hulka tuliyojijengea ya kufikiri tuko tofauti na binadamu wengine. The bottom line ni kuwa tumekuwa laughing stock tangia kwa majirani zetu mpaka duniani kote.

Je, tutaweza kujikwamua sisi wenyewe na kwa njia gani. Naamini bila kufanya maamuzi mazito na machungu hatufiki. Lazima tuonyeshe kwa vitendo kuwa tunachukizwa na hali iliyopo na kudai mabadiliko - siyo kuomba. Tujitoe mhanga kupambana na yeyote atakayetaka kutukwamisha bila kujali cheo chake, elimu yake, rangi yake, dini yake, kabila lake na itikadi yake.
 
Nitarudia kusema nilichopata kuandika kabla: Tanzania ni taifa la watu waliochanganyikiwa na kukata tamaa, kutoka walio matawi ya juu mpaka kwenye mizizi.

Mauaji ya albino, na haya ya watoto wadogo ni kielelezo cha watu wenye matatizo katika fikra.

Nikiachana kidogo na mauaji haya, nitawaeleza uendeshaji wa shughuli mbali mbali TZ. Nenda kwenye mabenki, na makampuni kama ya simu, na ofisi nyingi nyingine zinazotoa huduma. Kiwango cha kutoa huduma hakifiki asilimia 50. Yaani watoa huduma wachache (mfano katika kaunta sita benki, utakuta mbili au tatu tu zina watoa huduma), huku wateja wamepanga misururu mirefu. Wenye benki yao hawashituki, wateja hawakasiriki, maisha yanaendelea. Haya ndio maisha ya kila leo Tanzania.

Kwa watu wenye akili na fikra zinazofanya kazi sawa, hali hii haiwezi kuvumiliwa kwa muda mrefu. Kwetu inaonekana ni sustainable. Kwa mnaokaa ughaibuni, siku kampuni ikizidiwa sana na wateja, si ajabu kukuta maafisa wa juu wanasaidia pale(idara) palipozidiwa.

Akili za watanzania zimelemaa au kulemazwa mahali fulani. Nina rafiki yangu mmoja(non-east african) aliniambia katika jumuiya ya afrika mashariki ya nchi tano: watanzania ndio bongo lala kati ya nchi zote hizo. Iliniuma, lakini ukweli niliuona.
 
Uovu ni lazima utimie kwanza na kipimo chake kijae hadi kufrika, ndipo saa ya Ukombozi itakapo kuja.

Kila dakika na saa inayopita katika dunia hii mapambano yetu yanasonga mbele.
Wengi tunafumbuliwa macho, maadui wanajitokeza wenyewe hadharani, matendo yao na maneno yao yanapishana na kutoa siri za uovu wao.
Mapambano ni hatua.
Tatua yeyote duniani ni jambo la makusudi, katika maana kwamba mtu huamua mwenyewe kusogea mbele au kurudi nyuma.
Hatua haipigwi kwa sababu matukio yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu. Hatua inapigwa kwa sababu ya uwepo wa nia, haja na mwafaka wa kupiga hatua.

Ukombozi wa kweli Tanzania utaletwa na watanzania wenyewe.
Ni sisi watanzania tunaokaa pembeni kusubiri mambo yajinyeeshe yenyewe ndio tutakao simama kidete kupambana na uovu huu.
Unyonge wetu utokanao na unyanyapaa wa muda mrefu ufanywao dhidi yetu na viongozi wa serikali ya CCM na kujiweka kwetu nyuma kama mikia ya hayawani, ndiyo mtaji mkuu wa mabaradhuri hawa wa KiCCM.

Watanzania wote hatuna budi kutambua kwamba,hakuna mjumbe wa Mungu atakaye shuka kuja kutukomboa katika minyororo hii tuliyojifunga wenyewe.
Aliye Mkuu na Bwana kuliko wakuu na wafalme wote wa dunia hii, alisha tupa uwezo na haki (sheria) ya kutawala kila kiumbe. Kamwe hakutoa haki hiyo kwa wachache kama wengi tudanganyikavyo na kuamini.

Kundi moja la watu wenye dhamana ya ksierikali lijiwekeapo nguvu nyingi mikononi mwake na kwenda kinyume na Sheria zote za nchi, zaidi katiba ya nchi,na kutumia nguvu hiyo kufungua milango ya Sefu za BOT na kuhamisha Maburungutu ya Noti za Dola Malori kwa Malori, tena mchana kweupe, na kudhani kitendo hicho kitawawezesha kutumia Tani hizo za fedha kutawala milele daima, ni ishara kubwa ionyeshayo kwamba ni kujidanganya kuendelea kutegemea kwamba sauti ya mtu mmoja au watu wawili au watatu zinatosha kutukomboa katika makucha ya nyama ume hawa.
Uharamia wa kiwango hiki ukifanywa na serikali ya chama dola(CCM) ili kununua haki ya ushindi kwa hila na udanganyifu mwingi ni kujidanganya kudhani kwamba siku moja tutaamka na kuambiwa watendaji wakuu wamejipiga pingu wenyewe na kujisweka ndani.
Ukombozi hauji kwa kusubiri wao(CCM) walotutia katika utumwa huu kwa makusudu ktukomboa. Ukombozi wa kweli utakuja tu pale watanzania wengi tutakapo acha tofauti zetu ndogo ndogo na kutoa sauti kwa pamoja kukomesha utawala huu dharimu.

Si kwa kutumia kucha zetu, nyembe, visu vya mfukoni, ngumi, viganja au fimbo.
Watanzania tuna silaha moja kubwa yenye uwezo wa kumwangamiza adui bila hata kumguza.

Kauri yetu.
 
Mimi nikisema ukweli nashambuliwa. Naambiwa ninajichukia. Naambiwa nina low self esteem (sijui hata kwa Kiswahili tafsiri yake ni nini). Naambiwa natukana watu. Naonekana mtu niliyelosti tu, hohehahe nisiye na mafanikio yoyote yale. Naonekana mjinga nisiye na askili. Naitwa degenerate na majina mengine kibao ambayo siwezi hata kuyakumbuka.

Labda kweli hayo yote ninayoambiwa kuhusu mimi ni ya kweli. Mimi sijui. Mwenye kuamini ninayosemaga na aamini. Mwenye kukataa na akatae. Mwenye kufumbia macho ukweli na afumbie na hata akitaka azibe masikio yake. Mwenye kunikasirikia mimi na kuacha kukasirikia matendo haya maovu na anikasirikie. Mimi nasema kile kilichopo na kila ninachokiona. Situngi wala kuzusha kitu. Kwanza mimi sio mtunzi mzuri wa hadithi. Nikiliona jiwe nitakwambia nimeona jiwe. Nikiona mnazi nitasema ule ni mnazi. Nitasema kile macho yangu yanachoona.

Ni hayo tu machache kwa leo.

NN,

Usiwe na wasi, kuna watu wanaofurahia posts zako kama Mpanda Merikebu. You may not be a good author but you are a great writer, humorist. I bet some people hated on Mark Twain his day because they couldn't get his humor and great message that it carried. I like how you put serious matter in sarcastic ways that a bunch of ppl don't get it and decide to hate on you.

Usikonde sana bro/sis, si unajua tena sisi ndivyo tulivyo :)
 
....Lakini pia wananchi wanapoamua kumuua mtu kwa tuhuma za wizi wanaadhibu siyo sawa na uzito wa kosa. Haiwezekani mtoto akuchomolee halafu adhabu yake iwe kifo!

society and values are crumbling;

the government have failed to mobilize its people; and

law enforcement is not there.

Nobody respetcs laws of the land from the top man in office and the society at large is taking by laws on their hands.

poverty and survival have become our norms of life;

anger can no longer be relinguished by love, but by brutal killing.

We are all a party to a society on making; think what will be Tanzania in 20 years.

International Observer, umesema yote! Gap baina ya walionacho na wasionacho inaongezeka, wakati huo huo upungufu wa maadili na imani unaongezeka. Si majambazi, wezi, vijana, wazee wake kwa waume, wote wanaona njia pekee ya kujipatia heshima mbele ya jamii ni utajiri wa haraka haraka, hata ikibidi kuua!

Taifa linaangamia.

Ni hatari kwa kweli.
 
The way I see it is that the problem is deep rooted, all of us are responsible. The government and its state organs are a total failure, but we as citizens have a responsibility of knowing what is wrong and what is right. The legal system in our country does not have a proper way of assigning crimninal responsibilty to the accused and/or suspects. We do not have proper means of investigating crime etc. On our side as citizens we have lost compasion, we have lost our minds, really what do you get out of killing a 14/16 year old. And yet we claim to be believers.
We need to overhaul the police, the CID etc, I can not say much on their training since I have never seen the Police Academy Training manual, but from the way they act I do not think they have sensitivity training and they do not seem to know that they could be prosecuted for police misconduct and other human rights violations..
 
Back
Top Bottom