Vifo vya wanafunzi Tanga: Rais atuma salamu za rambirambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo vya wanafunzi Tanga: Rais atuma salamu za rambirambi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wauguzi katika hospitali ya mkoa ya Bombo wakiendelea kuwahudumia baadhi ya majeruhi wa ajali ya wanafunzi wa Shamsili Maarif waliopata ajali mwishoni mwa wiki. (Picha: Ramadhani Juma, Tanga).  Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Shamsil Maarif cha jijini hapa, Mohammad Abubakar Burhan, kufuatia ajali mbaya ya gari iliyosababisha wanafunzi 19 wa chuo hicho kupoteza maisha.
  Ajali hiyo ilitokea usiku wa Aprili 27 katika eneo la mzunguko la Mabanda ya Papa, ambapo wanafunzi hao waliokuwa wamepakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 757 BDV aina ya Fusso, walikuwa wakitokea katika Kijiji cha Kibafuta walikokwenda kwa ajili ya kuhudhuria mhadhara wa Maulid.
  Katika salamu zake, Rais Kikwete amewataka ndugu waliopoteza wenzao katika tukio hilo kuwa na moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi na kukumbuka kuwa, tukio hilo limetokea kwa mapenzi ya Mungu.
  Salamu hizo zilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Kalembo jana wakati wa mazishi ya mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Omar Chikangila (17) aliyefariki juzi katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo alipokuwa amelazwa.
  Chikangila ambaye ni raia wa nchi ya Malawi alizikwa Chuoni hapo alasiri ya jana, katika eneo ambalo awali walizikwa wanafunzi wengine tisa na hivyo kutimiza idadi ya wanafunzi waliozikwa chuoni hapo kufikia 10.
  Rais alisema msiba huo umemgusa kila mtu na kwamba alikuwa ahudhurie shughuli hizo za mazishi lakini ameshindwa kufanya hivyo kwa kuwa yuko nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki jijini Kampala.
  Naye Mkuu wa Chuo hicho Mohammad Abubakar Burhan, alitoa shukrani kwa wasamaria wema ambao wamekuwa wakitoa misaada tofauti, ikiwemo chakula na madawa kwa ajili ya majeruhi chuoni hapo.
  Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga, Pascal Kanyinyi, hali za majeruhi waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Bombo zinaendelea vizuri ambapo mpaka sasa wamebaki majeruhi 27 wodini kati ya wale 55, ambapo wawili wamesafirishwa kwenda Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280

  Jamani muogopeni Mungu!!!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mungu aziweke roho za marehemu pema peponi amen
   
Loading...