Vifo vya Wanafunzi Arusha: TBC mmetutia Aibu kubwa

Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
12,422
2,000
Kwanza nianze kuwasifu na kuwapongeza CLOUDS MEDIA kwa kuwa na moyo wa kizalendo kwa kusitisha huduma za matangazo ya kawaida kufuatia msiba wa kitaifa tuliopata watanzania.

Pili niwalaumu na kuwashangaa TBC kwa kushindwa kulitambua hilo na kuamua kuendelea na vipindi vyenu kama kawaida.
Dah...Chief....Kumbe huwa unaangalia TBC?:D:D:D:D:D:D:D
 
Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,264
2,000
c
Jana kuanzia mida ya saa tisa hivi walikuwa wakionesha ila mahojiano na mwakilishi wao kama jina sijalikosea Mark Mkwame hayakuwa yaliyolenga kutoa majibu kwa Watanzania,Mfano badala ya kujikita zaidi kwenye suala la ajali na nini huenda kilisababisha tatizo la ajali hiyo je tahadhari zipi ziwekwe na kipi tujifunze tusije kumbana na msiba mkubwa wa taifa kama huo,wao walibobea kwenye kuelezea ubora wa shule mara kimkoa ilikuwa yangapi,mara kitaifa ilikuwa ni ya ngapi na kuendelea kusifia sifia tu zaidi kama vile kuipromoti kibiashara na wala sio kuombeleza msiba,ok ,hayo yanaweza yakawa ni moja ya mambo ya kuzungumzia ndani ya ajenda za msingi ila sio kuyapa nafasi yamahojiano kwa asilimia 70 ++++,
Tunaona baadhi ya shule mabasi yao ni yale choka mbaya ilimradi yanajikongoja hata kama yanafuka moshi utafikiri wanachoma nyumba na pia yana rangi ya njano basi,watoto wanarundikwa kama senene wa Bukoba,Hakuna care taker ndani ya basi watoto wanakanyagana ovyo tu,kama mnakumbuka kuna mwaka mmoja hapo nyuma kidogo kuna mtoto alidondoka kupitia dirishani kutoka kwenye skuli basi huko Dar es salaam,alipasuka kichwa na kupoteza uhai,Mikanda ya abiria hayana.
Kifupi walininiboa sana.
CHOMBO CHAKO KISIKUBOE
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,446
2,000
Ni kweli,ila TBC iliyokuwa na Tija ni ile ya TIDO,sasa hivi Pumba zimezidi,ubunifu Duni,Hawana hata clips kwenye maktaba zao wakawaangalia watu kama kina Betty Mkwasa walivyokuwa wakiripoti matukio kipindi cha msiba wa baba wa Taifa,au Jerry Muro kipindi akiwa TBC.
Clips zipo ila mtu mwenye uwezo wa kuzichezesha ndiyo hakuna
 
shybubu

JF-Expert Member
Oct 30, 2016
513
500
Kwanza nianze kuwasifu na kuwapongeza CLOUDS MEDIA kwa kuwa na moyo wa kizalendo kwa kusitisha huduma za matangazo ya kawaida kufuatia msiba wa kitaifa tuliopata watanzania.

Pili niwalaumu na kuwashangaa TBC kwa kushindwa kulitambua hilo na kuamua kuendelea na vipindi vyenu kama kawaida.
Haiwezekani media zote zijikite kwenye maombolezo 100% lazima tupate habari zingine pia, hii nchi ni kubwa ,siku moja ni ndefu na ya Mungu ni mengi pengine limetokea janga kubwa kuliko hilo, au Alshababu wanapiga tutapata wapi habari? Punguza chuki, kuwa neutral itakusaidia kuishi vizuri.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,446
2,000
Haiwezekani media zote zijikite kwenye maombolezo 100% lazima tupate habari zingine pia, hii nchi ni kubwa ,siku moja ni ndefu na ya Mungu ni mengi pengine limetokea janga kubwa kuliko hilo, au Alshababu wanapiga tutapata wapi habari? Punguza chuki, kuwa neutral itakusaidia kuishi vizuri.
Akili zako na hao viumbe ulio wapakia kwenye hiyo wheelbarrow zinafanana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom