Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,968
Taarifa ya Kamati ya Jaffo inakinzana na taarifa ya awali ya Mamlaka ya Bonde la Mali la Ziwa Victoria.
Mamlaka ya Bonde walidai utafiti wa awali wa kimaabara unaonyesha uwepo wa mafuta kwenye maji. Kamati ya Jaffo inasema ni kinyesi (tani 1.8) & mkojo (Lita 1.5 bilioni) wa mifugo pamoja na maozo ya mimea.
Taarifa hizo mbili haziwezi zote kuwa za kweli ni dhahiri moja wapo ni ya uongo. Nani anadanganya? Mwenye akili na afikiri.
Pia, muhtasari wa taarifa ya kamati, kama ulivyosomwa leo, unaeleza kuwa Barrick North Mara hawahusiki na uchafuzi huo.
Swali la msingi ni je, kwanini taarifa ije na utetezi wa mgodi moja kwa moja?, je, kuchunguza kama mgodi unahusika ilikuwa ni moja ya hadidu za rejea?
Taarifa ya Kamati ya Jaffo inaeleza kuwa video za samaki waliokufa na kuelea kwenye maji meusi sio za Mto Mara. Swali ni je, ni video za wapi? Kama ni Tanzania, kwanini zikaliwe kimya?
Pia, nani anawajibu wa kufuatilia ubora wa maji ya Mto Mara? Alikuwa wapi kwa miezi 8 mpaka kinyesi cha mifugo kimechafua mto? Usalama wa Mito mingine nchini iliyoko kwenye jamii za wafugaji ukoje?
Tuna maswali mengi ya msingi; tutauliza wakati sahihi na wakati sahihi u mbioni, umekaribia.
Pia, soma;
Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini