Vifo vya majini! Namna nyingine ya kuongeza mapepo

Kila roho ina asili yake... Na hiyo asili yake ni makazi katika mwili uharibikao.. Roho huishi milele lakini lifespan ya mwili huwa ni fupi sana.... Mwili unapochoka au kwa sababu nyingine zozote ukaachana na roho...

Kuna mambo mawili hutokea
Jambo la kwanza ni roho kuwa hapo hapo mwii ulipo.. Hasa kaburini... Dhana ya peponi
Jambo la pili ni roho baada ya kuachana na mwili kuanza kutangatanga huku na kule... Huitwa roho ya mahangaiko... Dhana ya kuzimu....

Mwili unaobahatika kuzikwa kwa taratibu zozote zile roho yake huwa na nafasi kubwa na kutulia sehemu moja au kuingia kwenye ulimwengu wa roho katoka mstari ulionyooka sana.. Hakuna mahangaiko yoyote... Mwili ambao haukuzikwa, roho yake ni nyepesi mno kuambaa na kuingia kwenye mstari usio mnyofu hivyo hukutana na vingi

Mapepo ni viumbe roho waishio baharini, nyikani na kwenye majabali au miti mikubwa... Sehemu ya uzao wa mapepo ni roho ambazo miili yake haikutunzwa vema... Kuna vifo hutokea majini yaani Mtoni, ziwani, bwawani au baharini... Na kwa muktadha huu baharini ndio penye kuhusika zaidi

Kima cha maji hasa ya baharini kinajulikana urefu wake... Kinapotokea kifo cha baharini mtu hufa bila hata kufika kwenye sakafu ya bahari... Sana sana baada ya muda mtaukuta mwili wake ufukweni... Huyu roho yake inaweza kuwa salama kidogo.. Lakini wale wanaofia baharini na wasipatikane tena roho zao huingia kwenye mkondo wa kugeuka mapepo ambayo makazi yake huwa ni baharini... Na bahari ndio inaongoza kwakuwa na idadi kubwa ya mapepo kutokana na nguvu yake kubwa ya uvutano na ukweli kuwa maji ndio yanachukua sehemu kubwa ya dunia yaani robo tatu.....

Mtu anapokufa kwa kuchomwa moto au kufa kwa ajali ya moto, roho yake hugeuka pepo la moto

Tunawafanyia marehemu ibada kulingana na imani zetu... Ibada hizi hazisaidii kufuta mabaya yake bali husaidia roho yake kuepuka kuingia kwenye ulimwengu wa mapepo
Zile jumuiya za siri ulimwenguni.. Zile zinazoamua nani awe nani katika nafasi za juu za kutawala duniani huepuka sana kuchagua mtu mwenye asili ya maji au majini kwa maana ya eneo... Watu wa namna hii huwa ni wepesi kuingiliwa na mapepo na kujikuta wanafanya mambo ya ajabu kabisa... Pepo hujificha kwenye kivuli cha wema lakini matokeo ya matendo yake huakisi uhalisia usioutaraji

Niwatakie Jumapili njema....!!!
Mshana...kaka
Umeeleweka Sana.

Sasa wale wanaotenda maovu na kujificha ndani ya nyumba zaibada....wakifa inakuwaje?
Mimi nikifa ibada ya mazishi ikaongozwa na kiongozi mkubwa wa Dini na dhehebu langu.....haitonifanya kutakaswa dhambi na kuingia Peponi....mbinguni?
Niambie ukweli....maana nimeambiwa kwakuwa sijumuiki kila jmos asubuhi...hvyo nikifa sizikwi na faza
 
Naomba kujua,je na wale wanokufa mazingira ya vita,nyikani na miili yao kutozikwa rasmi roho zao hugeuka kuwa nn?!
 
Mshana...kaka
Umeeleweka Sana.

Sasa wale wanaotenda maovu na kujificha ndani ya nyumba zaibada....wakifa inakuwaje?
Mimi nikifa ibada ya mazishi ikaongozwa na kiongozi mkubwa wa Dini na dhehebu langu.....haitonifanya kutakaswa dhambi na kuingia Peponi....mbinguni?
Niambie ukweli....maana nimeambiwa kwakuwa sijumuiki kila jmos asubuhi...hvyo nikifa sizikwi na faza
Mfu hana msamaha wa kifo sana sana ibada inasaidia tu roho yake isigeuke pepo
 
Mr.mshana...naomba unifafanulie hili...baba yangu mdogo alifariki miaka ya 90... But kipindi amefariki na kuzikwa alikuwa anatembea sana usiku...kuna wakati ilifikia alikuja home akagonga dirishani ...akisema "kaka nimekuja kukusalimia maana nimeambiwa umekuja" (alikuja kumsalimu baba yangu Mimi) ...na kuna kipindi alikuwa anakuja jikoni usiku kama mlibakisa chakula basi alikuwa anakula ...kisha asubuhi mnakuta baadhi ya kuji zinakuwa nimechochewa jikoni (alikuwa anaota moto) ...pia kuna siku alikuja usiku baba ananyemelea ili ajue anatokaga mdogo wake...basi marehemu alipogeuka kumtaza baba ....marehemu aligeuka akaaza kuondoka baba alimfukuzia ...basi marehemu Bamdogo alipokata kona ya nyumba yetu akapotea ..baba hakumuona alipoelekea...naomba ufafanuzi wako inakuwaje MTU anakuwa ameshazikwa lakini hutembea na kufanya matendo kama hayo hapo juu niliyoelez?
Iwe alipokata kona alipotea huku baba yangu asijue alipoekea? Nasubiri jibu mkuu.
@Mshana Jr hujampa maelezo huyu mtaalam hapa
 
Back
Top Bottom