Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This

Mahabusu wangefanikiwa kutoroka mngesema polisi wetu wazembe au wamepewa rushwa, polisi ukijaribu kitoroka lazima aku shoot tu kwani hakuna namna ingekuwa sivyo hivyo mahabusu wangesindikizwa na virungu. Kuweni zuri basi siyo kila jambo ni baya tu.
 
jamani mie nilichelewa kama dakika tano baada ya tukio hilo kutokea, nikiwa natoka shinyanga kuelekea mwanza tulipo fika maeneo hayo nadhani ni usagala tuliona mili ya hao mahabusu ikiwa barabarani,kwa mazingira hayo tu inaonyesha kuwa waliruka gari ilipofika ktk tuta, kwa atakae hitaji picha ani PM
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ni Mathias Chikawe.

mkuu wewe ndio hujaelewa amemtaja saidi mwema na nchimbi kama wazir wa mambo ya ndani si kwa Uzi huu ila anakumbusha kuwa alishawahi kuleta Uzi wao kama tahadhari na sasa kipindi hiki yametokea,si kwamba kachanganya au hajui kama chikawe ndio wazir wa mambo ya ndan wa sasa
 
Pasco unaweza naomba utofautishe kati ya RCO na RSO?
Kwa msaada kidogo ni kuwa RCO huyu ni Polisi yaani Regional Criminal Investigation Officer (mkuu wa upelelezi wa jinai Mkoa) kiutawala yuko chini ya RPC. Na huyo RSO sio Polisi bali ni Afisa Usalama wa Mkoa (wengine wanaita usalama wa taifa) au Regional Security Officer.
Majukumu yao yako tofauti kabisa ingawa kuna sehemu wanashirikiana, na katika ngazi ya Mkoa huyo RCO sio mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kwani mjumbe ni RPC.
 
Ndugu jitahidi kujibu kwa Hekima kidogo,hivi hata km ni matusi Ndo umuhusishe na Mama yake?,Mama yake amekukosea nini wewe??,Ndugu zake nao wamekukosea nini wewe???,Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!,Hao wengine wamekukera nini??,Hapo ukute wengine walishafariki!!!.

umeona alicho comment kwenye thread yangu NLIYOJIBIWA na mtu mwingne? Au na wewe unakurupuka fuatilia uone nani kadandia thread ya mwenzake na kuanza matusi
 
ww pasco ni MPUMBAVU, sasa kama wafungwa wanataka kutoroka mikononi mwa polisi au magereza na badae iwe lawama au polisi kufungwa au kufukuzwa kazi bora UWAFYATUE WAKAFIE MBALI,.,wewe na hao wanaokusapoti kwa MIHEMKO U KUWASHWA KAENI KIMYA hamjui sheria kua mfungwa anapokimbia au mahabusu anatakiwa afanywe nini na askari?

duh we kweli unajuwa sheria, yaani mfungwa au mahabusu anapotoroka kumbe anahukumiwa kifo?
kilicho cha ukweli, askari mwenyejukumu la kumlida mahabusu au mfungwa anaponyang'anywa silaha hapo hakuna jinsi hali kama hii haiwezi kuzuilika, lazima askari ajitetee
 
inawezekana wana familia zao tena humuhumu alafu wanatukana na stahili ya kuficha majina unaweza kua unamtukana mama yako maana mambo yenyewe kila mtu android
 
Pasco kuna mengi sana kuhusu manyanyaso ya polisi. Walimua kijana mahabusu kule arusha kwa kesi za kuzua za kigaidi ati nae alitaka kutoroka.
Kuna matukio mengi ya kutesa mfano uamsho yamesemwa sana kuwa polisi waliwatesa na kuwadhalilisha sana. Jambo moja ni kuwa double standard kusemea haya mambo ndio maana yanakosa uzito. Kuteswa au kuuliwa bila kosa ni jinai tu akiwa uamsho au mwizi wa kuku . Tunapochagua lipi la kukemea tunakosa nguvu ya pamoja kukemea uonevu huu.

Suala la kujiuliza jeee police ni licence to killl ?
Jee anaetoroka kuna sheria ya kumpiga risasi?
Jee mafunzo wanayopata ndio yapo hivo ukizidiwa kumkamata kill him?
Anyway inasikitisha sana ila tuache double standard pia
 
Last edited by a moderator:
duh!! Yaan hii hasira sio bure..
Lazma kuna uhusiano wa kiharifu

Na wewe toa umbumbumbu wako hapa,eti kuna uhusiano na uhalifu,ndo ulivyofundishwa shuleni? Hapa kila mtu anazo hisia zake ktk kuchangia usitake kunichagulia hisia eti kisa nimeenda against basi na mie ni mhalifu,nyie mnapenda sana kuua watu wasio na hatia,mtu anawezaje kuruka kwenye gari iliyo ktk mwendo kasi na kafungwa pingu? Halafu huyu UCD eti anatishia watu,nipo kanda ya ziwa njooni mnikamate mkanitese na mimi,hii ni aibu sana haiwezekani kwanza vituo vya police kuvamiwa kila leo na askari kuuawa na silaha kuporwa,tukio moja tu police wangechukua hatua kali ya kufunga CCTV ktk vituo vyote vya police nchini,kwa uzembe huu wa police wao ndo wanahusika.
 
Hapo hata sijaelewa hii mada ilikuwaje.Binadamu tumwogope Mungu na kutafuta suluhisho wengine huwa tunajifunza kupitia ukurasa huu sasa hapa tunajifunza nini zaidi ya mitusi tu.
 
Kwa maoni yangu polisi wachache wasio waadirifu ndo wanawapaka matoke polisi wengine ambao wanajua sheria na taratibu za kazi. Kwa upande wa hao mahabusu kwa uelewa wangu kama walijaribu kutoroka polisi wameishafundishwa sehemu za kulenga pasipo kumuua mahabusu.
 
Back
Top Bottom