Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This

Hayo ni majungu....anayesema ni yule ambaye alikuwa kwenye tukio pale kuwa alitaka kumnyang'anya askar we unakuja na majungu yako hapa..,acha majungu ya kike,,,,polisi wamepigwa sana hivi karbuni au ungependa kusikia polisi nane wauwawa baada ya mahabusu kumnyang'anya askar bunduki??????tuwe wazalendo tuache ushabik usiokuwa na msing,,,polisi wetu wanafanya kazi ngumu sana japo ni ukweli isiopingika raia uwachukia Askar bila kuwepo na sababu za msingi,,,,,Ni majungu ila yakitufika shingoni ndo tuonapo umuhimu....muhasibu wa NMB bank aligundua umuhimu wa polisi na akahapa hatozarau tena polisi,,,wameokoa maisha yake..


TUACHE MAJUNGU POLISI NI WATU KAMA WATU WENGINE
 
Ulichokisema mkuu Pasco kina ukweli mkubwa sana,
na ndio maana na mimi huwa nashangaa kuwa Polisi wakifanyiwa tukio flani (mfano la stakishari)
kinachofta baada ya hapo ndani ya siku 2 -3 utasikia na wao wameua ...yaani ukitathmini sana unakuta
unaona kuna aina ya kisasi ndani yake.

Huwa wanafanya operation maalumu na watakaokamatwa wanafunguliwa jalada la wahusika wa Stakishari wakamatwa, kinachosikitisha mpaka miili inafika hospitali majina yao hayakujulikana kwa maelezo kwamba polisi waliowapeleka sio wao waliokuwa kwenye tukio. (unasafirisha binadamu hata kama wana makosa hata detail zao huna)
 
ndugu ni kwamba polisi/magereza anaruhusiwa kumpiga mfungwa au mahabusu risasi kama atakimbia na hata kama utamlenga kichwani makusudi ni sawa bz utajitetea kua ulitaka umjeruhi tu, JAPO HUTAHOJIWA SANA NA WAKUBWA ZAKO.
ILA KAMA MFUNGWAAU MAHABUSU KAKUKIMBIA UNA HATARI YA KUFUKUZWA KAZI NA KUFUNGWA BADALA YAKE...
so bora umuue kuliko akukimbie na hata vitabu vyao vya mafunzo na sheria zinasema hvyo
​Comment hii sijashangaa na ID name yako, Bongo ni zaidi ya uijuavyo
 
Pasco hii habari yako uliyoianzisha ni nyeti kuliko wanavyodhani watu. Nimepata habari kutoka kwa mwandishi wa habari mmoja kuwa mahabusu hao walikuwa wamefungwa pingu kwa vile walikuwa kwenye gari la wazi. Ni vipi wajaribu kunyanganya silaha? Na zoezi la kunyanganya silaha lilipo anza kwa nini dereva hakusimamisha gari maana wanasema wamekufa kwa majeraha ya kuruka kwenye gari.
Maisha ya wananchi ( hata kama ni watuhumiwa) uchunguzi ufanyike na ndicho kinachofanya wanahofu. Wahudumu wa Hospitali nasikia nao wana kauli tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Pasco alitaka kuendelea kusikia polisi anyang'anywa silaha na mahabusu kisha kuuwawa na mahabusu kufanikiwa kutoroka hapo angekuja na uzi polisi Haina uweledi ktk kazi lkn kwa hili unaona hakuna ushahidi wa hilo tukio la kujaribu kupora silaha bali ni wauaji tu daaah kama kuna watu wenye mazingira magumu ya kazi basi police ni no 1.
 
Hapa tutapigana zogo eee mpaka basi
Kwanza tujue hao wafungwa walikuwa wana kesi Zipi?
Maana msije kuwa mnatetea watu kumbe ndio wale wale wenye kesi kubwa na ndio wengi hufanya majaribio ya namna hii.
Ameachiwa Papa Musofe tumepiga Kelele,hawa wametaka kusepa tunapiga kelele
Na kama wangetoroka basi sie hawa hawa tungelaumu polisi na kusema wamekula dili.

Polisi fanyeni kazi yenu,Raia kulalamika baadhi ya vitu ni kawaida yetu.

Tujuzeni kwanza walikuwa na kesi zipi,hapo ndio tutajua kuchangia kuanzia wapi
 
Wewe huhitaji kupata ban bali unahitaji kibano kwa maneno yako yasiyo yakistaarabu muulize ndugu yako wa FB alitoa maneno kama yako kuhusiana na majambazi ya stakishari akifikiri hawezi patikana saa hizi yuko kwenye kibano ana shindwa hata kujitetea kwa maneno yake ya kifedhuli. Wiseboy chunga ulimi wako utakuponza usifikiri huwezi kufikiwa usifikiri wote humu ni watumiaji wa kawaida Wa mitandao!!!

Usinitishe bana,kwanini nyie mnashabikia mauaji ya raia? Eti kisa mahabusu? Police wameua raia wangapi wasio na hatia? Mungu ameanza kuwaadhibu na wao sasa.
 
Jana nilipoona ile habari nikajiuliza hawa jama walikuwa hawajafungwa pingu!? Yani mtu anapingu alafu gari inaenda kasi amnyanganye police silaha??Hapana kuna namna hapa nakumbuka mauwaji ya wale vijana wa morogoro waliokuwa na Madini..Asante Chakaza kwa kuliona hili...
 
Hongera sana Mkuu kw kuyatoa ya moyoni. Ni jambo jema na zuri tupo pamoja.
Vijana wa Mangu c wapo huku kufuatilia... Wameisoma au wataisoma khs mambo yao against the law.
 
ww pasco ni MPUMBAVU, sasa kama wafungwa wanataka kutoroka mikononi mwa polisi au magereza na badae iwe lawama au polisi kufungwa au kufukuzwa kazi bora UWAFYATUE WAKAFIE MBALI,.,wewe na hao wanaokusapoti kwa MIHEMKO U KUWASHWA KAENI KIMYA hamjui sheria kua mfungwa anapokimbia au mahabusu anatakiwa afanywe nini na askari?

Mkuu anaetaka kutoroka lazima auwawe...? Mbinu nyingi wamefundishwa depot au ndiyo kusema uvivu wa mazoezi...?
Mkuu silaha ni jambo la mwisho kuitumia..
 
Polisi naye ana maadili ya kazi yake, kitendo cha kumpiga risas mtuhumiwa inategemeana na mazingira, madhara ya mtuhumiwa kwa polis au jamii.

Polisi anaweza kumpiga risas mtuhumiwa na hata kama akashtakiwa anaweza kushinda kesi ni yule tu.
Anayeweza kuleta madhara kwa polis au raia endapo atafanikiwa kutoroka. Mfano endapo mtuhumiwa huyo anasiraha.
Au mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, ujambaz wa kutumia siraha, au gaidi huyo kama akijaribu kutoroka polis anaweza kumpiga risas..

Na endapo polis atashtakiwa kwa mauaji anaweza kujitetea na asifungwe
 
Wewe huhitaji kupata ban bali unahitaji kibano kwa maneno yako yasiyo yakistaarabu muulize ndugu yako wa FB alitoa maneno kama yako kuhusiana na majambazi ya stakishari akifikiri hawezi patikana saa hizi yuko kwenye kibano ana shindwa hata kujitetea kwa maneno yake ya kifedhuli. Wiseboy chunga ulimi wako utakuponza usifikiri huwezi kufikiwa usifikiri wote humu ni watumiaji wa kawaida Wa mitandao!!!

Mmeshindwa kuukamata mtandao wa wahalifu wanaopora silaha police mnakimbilia kukamata wachangiaji wa mitandaoni na kuwatesa,hiyo ni poor intelligence system,unadhani mhalifu aliye muuaji katili kama wale wa stakshari anaweza kupata muda wa kuingia humu? Na eti atoe maoni? Mnasomea wapi upelelezi nyie mbona mna aibisha sana?Huna hata aibu kujisifu eti mtumiaji wa FB alikamatwa kisa kaonyesha negativity ktk mawazo yake,we unadhani kila mtu anahuzunika police kuuawa? nyie mmeua raia wangapi wasio na hatia? mmeua waandamanaji,mmeua wafanyabiashara na kupora pesa zao,mlimuua mwangosi.
 
Siku likikukuta la kukuta ndio utafahamu umuhimu wao maana kawaida ya binadamu kama wewe huona umuhimu wa kitu pale anapokihitaji, na siku hiyo ndipo utakapotofautisha polisi na jambazi.
 
Wewe huhitaji kupata ban bali unahitaji kibano kwa maneno yako yasiyo yakistaarabu muulize ndugu yako wa FB alitoa maneno kama yako kuhusiana na majambazi ya stakishari akifikiri hawezi patikana saa hizi yuko kwenye kibano ana shindwa hata kujitetea kwa maneno yake ya kifedhuli. Wiseboy chunga ulimi wako utakuponza usifikiri huwezi kufikiwa usifikiri wote humu ni watumiaji wa kawaida Wa mitandao!!!

hajajua bado yeye anafikir kila mtu yupo kwaajili ya kusoma na kuandika upuuzi
 
Pasco na wiseman sameheanen yaishe.matus di mazur jaman sisi ni wamoja kauli zikipishana tuvumiliane.nitafurahi kama kat yenu mmoja ataomba msamaha.please
 
Back
Top Bottom