Vifo vya ghafla vya Lemtuz na Membe, naanza kuunganisha nukta!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,793
18,216
Awali ya yote natoa pole kwa familia za Lemtuz na Membe kwa kuondokewa na wapendwa wao. Kifo ni fumbo kubwa. Vifo hivi vimetokea ghafla, hasa kipindi hiki ambacho baridi imeanza kukolea.

1684059956820.png

Le Mutuz na Membe wakati wakiwa hai (Chanzo:Mtandao)

Kwa mujibu wa daktari wa familia, kifo cha Membe inasemekana kimesababishwa na virusi vilivyoshambulia mfumo hewa vilivyopelekea damu kuganda. Na kama tujuavyo, virusi huwa active zaidi wakati wa baridi, kama ilivyowahi kutokea mwaka 2019.

Taarifa za kifo cha Lemtuz hazijaeleweka vizuri lakini nimesikia tetesi kuwa alikuwa na shida ya moyo. Na kwa kuwa virusi hushambulia zaidi wazee na watu ambao afya zao zimedhoofishwa na magonjwa mengine, sasa naanza kuunganisha nukta kuwa ipo haja ya watanzania kuendelea kuchukua tahadhari, kama tulivyowahi kuchukua siku za nyuma, hasa wakati huu tunapoisogelea miezi ya baridi (Juni na Julai).

Turejee utamaduni wetu ule tuliofanya kipindi kile ili kuokoa afya zetu na tumuombe Mungu aendelee kutupigania kwa kuwa Yeye ndiye muweza wa yote. Amina.

Nawasilisha.
 
Kutunza afya zetu ni muhimu, lakini mwisho Kifo ni kifo boss, yaweza kua ni upepo tuu kama wanavyoongozana kwenye familia mda mwingne au mtaani.
Ni kweli kabisa mkuu lakini jitihada binafsi zinahitajika kwani tukiisubiri serikali ije kutusukuma tutakuwa tumechelewa sana.
 
Lemetuz si ameumwa hadi kulazwa mara kwa mara mkuu. Unataka kusema nini.

Kama unadai membe kafa kwa hivyi virusi unahisi membe hakuwai kupata chanjo zote stahiki.

Kifo ni kifo ata hivyo miaka 60+ inatosha kuishi
Mkuu mimi sijakataa usemacho lakini ukumbuke kuwa virusi huathiri zaidi wazee na watu wenye maradhi mengine. Aidha, chanjo inapungua nguvu kadri muda unavyoenda. Ndio maana hata wanyama huchanjwa tena kila baada ya kipindi fulani. Hope umenielewa.
 
ACHA UONGO BHANA, VIRUSI WAPI BHANA WEWE...

HAKUNA CHA COVID WALA NINI....

ACHENI KUWAPA WATU MIPRESSURE

Check TBC1 kuagwa kwà BM, viongozi hawajavaa yale madaso/mataulo ya kuzibia pua na mdomo. Meaning Hakuna Covid

USITUTISHE BHANA!!! MPUUZI MMOJA UMEJAA MI U.T.I UNAINGIA HUMU JF KUANZISHA THREAD ZA KUTISHA WATU!!!

JIHESHIMU BHANA!!

ASEE MODS EEH,..FUTENI HILI LI UZI LAKE! HUYU JAMAA NI KIAZI SANA!!!
 
Mkuu mimi sijakataa usemacho lakini ukumbuke kuwa virusi huathiri zaidi wazee na watu wenye maradhi mengine. Aidha, chanjo inapungua nguvu kadri muda unavyoenda. Ndio maana hata wanyama huchanjwa tena kila baada ya kipindi fulani. Hope umenielewa.

Una hisi membe kwa nafasi yake alikua hafahamu kuhusu kuisha kwa chanjo?. Unapokua mzee kumbuka mtendaji kazi wa mwili unakua hafifu.

Ikitokea ata jambo la kukushitua au lenye kukuchukua mawazo yako kifo kinaweza kukufika
 
Awali ya yote natoa pole kwa familia za Lemtuz na Membe kwa kuondokewa na wapendwa wao. Kifo ni fumbo kubwa. Vifo hivi vimetokea ghafla hasa kipindi hiki ambacho baridi imenza kukolea.

Kwa mujibu wa dakatari wa familia, kifo cha Membe inasemekana kimesababishwa na virusi vilivyoshambulia mfumo hewa. Na kama tujuavyo, virusi huwa active sana wakati wa baridi, kama ilivyowahi kutokea mwaka 2019.

Taarifa za kifo cha Lemtuz hazijaeleweka vizuri lakini nimesikia tetesi kuwa alikuwa na shida ya moyo. Na kwa kuwa virusi hushambulia zaidi wazee na watu ambao afya zao zimedhoofishwa na magonjwa mengine, sasa naanza kuunganisha nukta kuwa ipo haja ya watanzania kuendelea kuchukua tahadhari, kama tulivyowahi kuchukua siku za nyuma, hasa wakati huu tunapoisogelea miezi ya baridi (Juni na Julai).

Turejee utamaduni wetu ule tuliofanya kipindi kile ili kuokoa afya zetu na tumuombe Mungu aendelee kutupigania kwa kuwa Yeye ndiye muweza wa yote. Amina.

Nawasilisha.
Naafikiana nawe inawezekana J&J ilikuwa geresha

230605756_2396685807142940_8252564083641687925_n.jpg
 
Awali ya yote natoa pole kwa familia za Lemtuz na Membe kwa kuondokewa na wapendwa wao. Kifo ni fumbo kubwa. Vifo hivi vimetokea ghafla hasa kipindi hiki ambacho baridi imenza kukolea.

Kwa mujibu wa dakatari wa familia, kifo cha Membe inasemekana kimesababishwa na virusi vilivyoshambulia mfumo hewa. Na kama tujuavyo, virusi huwa active sana wakati wa baridi, kama ilivyowahi kutokea mwaka 2019.

Taarifa za kifo cha Lemtuz hazijaeleweka vizuri lakini nimesikia tetesi kuwa alikuwa na shida ya moyo. Na kwa kuwa virusi hushambulia zaidi wazee na watu ambao afya zao zimedhoofishwa na magonjwa mengine, sasa naanza kuunganisha nukta kuwa ipo haja ya watanzania kuendelea kuchukua tahadhari, kama tulivyowahi kuchukua siku za nyuma, hasa wakati huu tunapoisogelea miezi ya baridi (Juni na Julai).

Turejee utamaduni wetu ule tuliofanya kipindi kile ili kuokoa afya zetu na tumuombe Mungu aendelee kutupigania kwa kuwa Yeye ndiye muweza wa yote. Amina.

Nawasilisha.
Na watu wengi now wanaumwa mafua na kikohozi
 
Back
Top Bottom