Vifo vya Dolphins Zanzibar na Majeshi ya Marekani...

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,416
2,264
Napenda kuuliza juu ya sababu zilizopelekea kufa kwa wingi kwa Dolphins katika fukwe za Visiwa vya Zanzibar mwaka 2006. Vifo hivyo viliacha maswali mengi pasipo majibu. Aidha SMZ, ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam viliahidi kutoa sababu ya janga hilo, lakini hadi sasa naona ni kimya.
  • Je ni nini kilisababisha vifo hivyo?
  • Je ni kweli vifo hivyo vilisababishwa na mazoezi ya kijeshi ya Marekani katika mwambao wa Afrika Mashariki?
  • Hatua gani ambazo zimeshachukuliwa kudhibiti kutokea tena kwa vifo kama hivyo katika siku zijazo?

Mwenye ufahamu kuhusu hili tafadhali nipatie majibu
 
Walipeleka na sample kama sikukosea uswidi kwa uchunguzi zaidi.

Sijui waligundua nini maana naona kimya tu
 
ndio ishapita hiyo, tunaangalia mafisadi na wanaogombana ee gombea kenya na huku kwetu
 
ndio ishapita hiyo, tunaangalia mafisadi na wanaogombana ee gombea kenya na huku kwetu
Kama chanzo chake hakukujulikana basi haijapita hiyo... Hayo mambo ya ufisadi na mazagazaga mengine yasie kigezo cha kutufanya sote kuwa ni wanasiasa.

Vifo vile vina mchango mkubwa katika hali halisi ya mazingira ya bahari yetu. Na iwapo vilisababishwa na binadamu hapana budi kujua ili kuweza kudhibiti kutofanyika tena. Na iwapo vilitokana na sababu nyingine ni vema vile vile kujua. Hii itasaidia katika utunzaji wa viumbe wetu wa baharini.

Nasikia kuna kamisheni ya mazingira ya baharini, huko Kiwengwa... sijui nao wanafanya nini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom