Kibunango
JF-Expert Member
- Aug 29, 2006
- 8,251
- 2,022
Napenda kuuliza juu ya sababu zilizopelekea kufa kwa wingi kwa Dolphins katika fukwe za Visiwa vya Zanzibar mwaka 2006. Vifo hivyo viliacha maswali mengi pasipo majibu. Aidha SMZ, ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam viliahidi kutoa sababu ya janga hilo, lakini hadi sasa naona ni kimya.
Mwenye ufahamu kuhusu hili tafadhali nipatie majibu
- Je ni nini kilisababisha vifo hivyo?
- Je ni kweli vifo hivyo vilisababishwa na mazoezi ya kijeshi ya Marekani katika mwambao wa Afrika Mashariki?
- Hatua gani ambazo zimeshachukuliwa kudhibiti kutokea tena kwa vifo kama hivyo katika siku zijazo?
Mwenye ufahamu kuhusu hili tafadhali nipatie majibu