Vifo vitokanavyo na Ukimwi vyatajwa kupungua Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids), Dk Leonard Maboko amesema vifo vitokanavyo na maambukizi ya virusi vya Ukimwi vimepungua kutoka 80,000 kwa miaka kumi iliopita hadi kufikia 27,000 mwaka 2019.

Dk Maboko alisema hayo jana mjini Morogoro wakati wa warsha ya siku moja ya watekelezaji wa afya za Ukimwi kwa fedha za mzunguko wa kwanza wa mfuko wa Kilimanjaro Challenge Against HIV AIDS.

Alisema kati ya vifo hivyo 27,000 vya wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ni 21,000 huku watoto chini ya umri wa miaka 15 wakiwa ni 5,900.

Alisema maambukizi mapya kwa miaka kumi iliyopita walikuwa watu 130,000 nayo yamepungua hadi 77,000 ambapo wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea walikuwa 68,400, watoto chini ya miaka 15 wakiwa ni 8,600.

Mkurugenzi huyo alisema vijana wenye miaka 15 hadi 24 ndio wanaopata maambukizi mapya kwa wingi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha, hivyo muhimu wakapatiwa.

“Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wanaotumia dawa ni 1.3 milioni na waliosalia hawatumii,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha malengo ya Serikali ya zero tatu yanafikiwa ifikapo mwaka 2030. “ Serikali kupitia mfuko huo wa Kili Challenge wameanza kutoa Sh543,618,700 kwa asasi 20 za kiraia ili ziweze kusaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi i,” alisema.

Mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na virus vya Ukimwi (Waviu) wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Mchungaji Emmanuel Msinga alisema fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliokusudiwa.

“Hizi fedha zitatusaidia kuwafikia watu ambao wameacha kutumia dawa,na hata wale ambao hawana elimu juu ya Ukimwi,” alisema.

Alisema kazi ya ushauri nasaha inahitajika kwa sababu wengi wa wanaokutwa na maambukizi wamekuwa hawakubali hali zao.
 
Back
Top Bottom