Vifo vingi vya watoto wachanga husababishwa na homa ya manjano

MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,480
944
Tumezoea kusikia kuwa Malaria ndio ugonjwa unaongoza kwa kusababisha vifo kwa watoto, na jitihada za kuudhibiti ugonjwa huo zinafanyika kwa kiwango kikubwa.

Lakini leo naomba tujadili kwa kina juu ya huu ugonjwa wa HOMA YA MANJANO kwa watoto wachanga hata watu wazima wanaweza kuugua. Watu wengi watoto wao hasa uzao wao wa kwanza, wamefariki kutokana na ugonjwa wa HOMA YA MANJANO.

Mara nyingi ugonjwa huu humshika mtoto zile siku za mwanzo baada ya kuzaliwa, na mama akichilewa kumuwahisha mtoto hospitali basi hata wiki haiishi mtoto yule atakufa. Imekuwa kama kafara kwa watu wengi mtoto wa kwanza lazima afe, ila ukichunguza sababu ya kifo ni HOMA YA MANJANO.

SASA TUJADILI, KARIBUNI WALE WATAALAMU WA MAGONJWA YA WATOTO; Nini chanzo cha ugonjwa huu kwa watoto? Wawezaje kumkinga mtoto asipatwe na ugonjwa huu? Ni zipi dalili za ugonjwa huu?

Huduma gani ya kwanza unaweza kumpa mtoto pindi ugunduapo homa hii imempata na amezidiwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom