Vifo vingi vya Marais wa Kiafrika vinatia mashaka

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,841
2,000
Angalia Laurent Kabila alivyouawa, mlinzi wake Rashid Kasereka, ambaye baadaye alipigwa risasi na Col Eddy Kapendi. Ni kama mchezo wa kuigiza. Maana inasemekana Rashid alikuwa anasubiriwa na mtu nje ya Ikulu huku ngazi ya kuruka ukuta nje ikiwa imeandaliwa. Mpaka leo hii nani alipanga njama za kumuua Kabila ni ndoto.

Mauaji ya Cyprian Ntayaramirwa na Habyarimana yalionesha namna gani ukiwa Rais wa Kiafrika unakuwa unawindwa ili uuliwe kwa nguvu au kwa kutumia akili.

Leo hii Idris Deby Rais wa Chad anauawa akiwa battlefront, jambo ambalo ni mashaka makubwa.

Kwamba Rais wa nchi anakwenda battlefront taarifa kamili za kiusalama?

Duh, watanzania tumuombe Mungu.
 

chef detat

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
15,349
2,000
Habyarimana aliuliwa na wafaransa wakishirikiana na wanyarwanda maana taarifa ilivuja kabla hajaja Tz, akakanywa na Mobutu akaambiw kuna mpango wa kukuua huko ila alilazimisha kuj Tanzania.

kilichofuata ndio hivo, ila ana bahati mbaya,maiti yake licha ya kuungua kwenye ndege ilichomwa tena moto mwaka 1997
 

Mbuyimayi

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
470
1,000
Tatizo lenu mnawapenda Marais wenu kuliko maendeleo yenu...
Acha wafe...!

Ni kweli kabisa, maana huwa hatuweki nguvu kwenye uimara wa taasisi tunaweka nguvu kwa haiba za watu, sasa tukipata vichaa inakuwa balaa maana hakuna ‘balance and check’

Mambo haya ya kutegemea utashi wa kiungozi wa juu tu bila hasa kujua nini jamii/umma unahitaji umefanya sehemu kubwa ya bara letu kuwa kama lilivyo ‘ disorganized society’
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom