Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
Hili ni sikitiko kwa wazazi, ndugu, marafiki na Taifa. Ila tu wazazi inakuwaje wanaruhusu watoto cha kushangaza miaka mitano kwenda disco????? Inabidi tuwe serious na malezi, something wrong here. Child Protection and Safety iko wapi na inaishia miaka mingapi Tanzania???? Hii iwe ni fundisho kwa Familia na Taifa ili kuweka by-laws kwa wazazi na waendeshaji wa maeneo ya starehe.
Sorry kwa wale ambao nitawaudhi but tabia ya kuwaacha watoto kuzagaa ipo sana kwa Waswahili. natumaini kwa wengi mtanielewa nikisema watoto wa USWAHILINI. Wazazi hawa nionavyo mimi wako loose sana na watoto wao kiasi kwamba unajiuliza mama unakuwa na raha gani mwanao wa say under 18 yuko anazagaa tu wala huna wasiwasi sembuse wa miaka mitano na chini ya hapo.
Unashangaa wakati wa sikukuu kubwa kama Eid, Christmass na kidogo Pasaka watoto wanaongozana barabarani kwa makundi mchanganyiko wa miak 2, 3, 4, ..... bila uangali wa watu wazima. Eti mtoto wa miaka 5,6,... anaambiwa mchunge mdogo wako. Sasa hii ni hatari na lichukuliwe kuwa ni tatizo la jamii ili lipatiwe ufumbuzi haraka sana.
Poleni sana wafiwa.
Ok, Kuna uvumi kuwa kulikuwa na harufu kali kama ya sumu kabla ya watoto hao kuanguka na kuanza kuzirai!!!!!