Vifo na migogoro ya ndoa havitaisha hadi pale serikali ikiruhusu hili

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,394
Migogoro mingi ya ndoa ukipitia majarada ya kipolisi na dawati la jinsia utagundua kwamba kwa 70% ni kutokana na ndoa za kikristu na 15% ni ndoa za kiislam, 10% ni ndoa za kimila (unyumba na wengi wao waishio kinyumba ni wakristu) na 5% inachangiwa na ndugu wa wanandoa wenyewe

Hivyo ukichukua ile 70% na ile 10% ya ndoa za kimila za wakristu utaona karibia 80% ya ndoa zenye migogoro ni za wakristo!

Katika kuondoa tatizo hili serikali iruhusu utaratibu rahisi wa kuachana na kuoana kama ilivyo kwa waislam!

Haina maana itaingilia maandiko matakatifu la hasha cha mhimu nikuwaondolea cheti mkononi halafu
Maandiko wabaki wabaki nayo wahusika kwa imani zao lakini serikali ifanye upande wake!

After all cheti cha ndoa hutolewa na serikali ili wachungaji na wanandoa wasaini! Hivyo endapo wanandoa wamechokana. Waachane hata serikali ya mtaa!

Serikali iruhusu kufutwa ndoa hizo kisheria kwa utaratibu rahisi hata kupitia wakili au baraza la serikali ya mtaa.
Kuwepo na fomu katika ngazi ya mtaa inayoruhusu watu kuachana! Na ndoa hiyo kisheria isomeke imefutwa!

Nasema hivyo kwasababu migogoro mingi ya ndoa za kikristo wengi wameachana kimwili lakini hubaki kuwindana kufumaniana kutokana na kile kicheti cha ndoa ambacho huwa kina mlolongo mrefu sana hadi kufikia divorce!

Turuhusu watu waoane hata kwa wakili na waachane hata wakili!

Tutakuja kujua baadae kwamba tumechelewa!

Tabia za watu zimekuwa ngumu!
Sheria ya ndoa imepitwa na wakati!

Vichaa, vilema na mauaji mengi sana yanachangiwa na migogoro ya ndoa!

Serikali ifanye jambo kutokomeza
 
Mahakama ndiyo ina haki ya kuvunja ndoa....
Na huko mahakamani watu wanavutana utakuta mme/mke hataki ku sign talaka, hakubali kuachwa
Hii migogoro kikubwa ni mmja wenu akubali, aushinde moyo
Bila hivyo watu watazidi kuumizana tu

Ova
 
Uelewa wako wa masuala ya ndoa kikristo ni mdogo hivyo achana nayo. Hizo takwimu umetoa wapi?
Mbona kaeleza wazi tu kwamba kwa mujibu wa kesi za wanandoa zilizoko polisi pamoja na madawati ya kijinsia. Kama unaona hizo % alizosema sio za kweli zipinge kwa hoja.

Hebu tueleze sasa uelewa wako kuhusu ndoa za kikristo ukoje? Watu wakichokana wanaweza achana kirahisi bila purukushani?
 
Hayo mambo ya imani zao watabaki nayo, cha mhimu serikali Ione namna ya kuwasaidia
Sasa uwe na Adabu...Unapotaka Kuingilia imani za watu na namna Serikali imekua na mipaka yake juu ya imani hizo. After all nilitegemea uje na taarifa rasmi kutoka kwa Serikali hiyo hiyo unayoishinikiza kutekeleza mawazo yako.
 
Mbona kaeleza wazi tu kwamba kwa mujibu wa kesi za wanandoa zilizoko polisi pamoja na madawati ya kijinsia. Kama unaona hizo % alizosema sio za kweli zipinge kwa hoja.

Hebu tueleze sasa uelewa wako kuhusu ndoa za kikristo ukoje? Watu wakichokana wanaweza achana kirahisi bila purukushani?
Alete chanzo kinachothibitisha hizo takwimu. Ndoa za kikristo zinapata mamlaka yake kwa Bwana Yesu Kristo na sio maoni ya mtu.
 
Mbona kaeleza wazi tu kwamba kwa mujibu wa kesi za wanandoa zilizoko polisi pamoja na madawati ya kijinsia. Kama unaona hizo % alizosema sio za kweli zipinge kwa hoja.

Hebu tueleze sasa uelewa wako kuhusu ndoa za kikristo ukoje? Watu wakichokana wanaweza achana kirahisi bila purukushani?
Kanisa lina Mamlaka ya kutatua changamoto za ndoa...Suala hili huamuliwa na Askofu na baraza lake.

Hii ni baada ya kujadiliana kwa kina na kuwa na sababu za msingi sana.

Ikifikiwa tamati maamuzi ya kuvunja ndoa hufuatia.

Katika ukristo ndoa halijafanywa kama swala la kwenda msalani na kumwaga haja kadri upendavyo.

Mwisho Serikali inatambua mipaka yake katika kuingilia uhuru wa imani za watu. ( Isipo kuwa kwa mvaa kobasi adhaniaye anachokiamini yeye ni lazima kitawale)
 
Migogoro mingi ya ndoa ukipitia majarada ya kipolisi na dawati la jinsia utagundua kwamba kwa 70% ni kutokana na ndoa za kikristu na 15% ni ndoa za kiislam, 10% ni ndoa za kimila (unyumba na wengi wao waishio kinyumba ni wakristu) na 5% inachangiwa na ndugu wa wanandoa wenyewe

Hivyo ukichukua ile 70% na ile 10% ya ndoa za kimila za wakristu utaona karibia 80% ya ndoa zenye migogoro ni za wakristo!

Katika kuondoa tatizo hili serikali iruhusu utaratibu rahisi wa kuachana na kuoana kama ilivyo kwa waislam!

Haina maana itaingilia maandiko matakatifu la hasha cha mhimu nikuwaondolea cheti mkononi halafu
Maandiko wabaki wabaki nayo wahusika kwa imani zao lakini serikali ifanye upande wake!

After all cheti cha ndoa hutolewa na serikali ili wachungaji na wanandoa wasaini! Hivyo endapo wanandoa wamechokana. Waachane hata serikali ya mtaa!

Serikali iruhusu kufutwa ndoa hizo kisheria kwa utaratibu rahisi hata kupitia wakili au baraza la serikali ya mtaa.
Kuwepo na fomu katika ngazi ya mtaa inayoruhusu watu kuachana! Na ndoa hiyo kisheria isomeke imefutwa!

Nasema hivyo kwasababu migogoro mingi ya ndoa za kikristo wengi wameachana kimwili lakini hubaki kuwindana kufumaniana kutokana na kile kicheti cha ndoa ambacho huwa kina mlolongo mrefu sana hadi kufikia divorce!

Turuhusu watu waoane hata kwa wakili na waachane hata wakili!

Tutakuja kujua baadae kwamba tumechelewa!

Tabia za watu zimekuwa ngumu!
Sheria ya ndoa imepitwa na wakati!

Vichaa, vilema na mauaji mengi sana yanachangiwa na migogoro ya ndoa!

Serikali ifanye jambo kutokomeza
Tukifahamu umuhimu wa familia hatutaruhusu hata hizo talaka kutolewa.

Familia legelege huzaa taifa legelege.
 
Back
Top Bottom