Vifo kwenye migodi Indonesia vyaongezeka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Idadi ya vifo kufuatia ajali katika machimbo ya migodi kaskazini mwa Indonesia imeongezeka Jumatano na kufikia watu 16 huku matumaini ya kupata manusura yakiendelea kufifia.
Watu 18 wameokolewa wakiwa na majeraha mabaya, kutoka kwa machimbo ya migodi haramu kwenye kisiwa cha Sulawesi.
Baadhi ya mashirika ya uokoaji yameripoti kwamba huenda kulikuwa na wachimba migodi kati ya 50 na 100 wakati ajali ilipotokea na maafisa wamefutilia mbali matumaini ya kuwapata waathiriwa wote.
Haijulikani ni wachimba migodi wangapi walikuwa ndani ya machimbo hayo wakati ajali hiyo ikitokea, Jumanne wiki iliyopita.
Juhudi za uokoaji zimetatizwa na hali ya mwinuko wa ardhi, udongo mwepesi na machimbo hatari ya madini ambayo ni membamba.
Msemaji wa idara ya majanga ya Indonesia Sutopo Purwo Nugroho amesema maafisa wa uokoaji wamekuwa wakifanya kazi masaa 24 tangu Jumatatu, sehemu hiyo baada ya kupewa taarifa kwamba ni eneo salama kuendelea operesheni hiyo ya uokoaji.
Visa vya ajali katika machimbo ya madini haramu, huripotiwa kila mara nchini Indonesia, yenye utajiri mkubwa wa madini.

VOA
 
Back
Top Bottom