Vifo: Kwanini ni wasanii nguri tu?

Status
Not open for further replies.

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Hivi huyu mungu wetu aliamua kuvuta mafaili ya wasanii nguri mwaka huu tu kuwa ndio watangulie mbele ya kiti chake?! Sielewi kwa nini kifo hiki kimenigusa kuliko vifo vingine vya wasanii waliotangulia! Ila tuna mengi ya kujiuliza, kwa nini wasanii wetu nyota zao zinapong'aa katika medani ya fani zao ndipo nao maisha yao yanakuwa mwisho? R I P Sharo.
 
Kuna watu wanafiwa na watu wanaowategemea kilasiku kwenye familia zao,hiyo ni ahadi na imeshapangwa wafe wao,,,,,hakuna cha unguli wala usuli
 
Wee ulitaka wasanii wasife? we vipi bana! kwani wasanii sio binadamu? watoto wangapi ambao hawajitimiza miaka 5 wamekufa mwaka huu!! Acha hizo bana. Hayo ni mambo ya mwenyezi mungu. Tusitoe suluhisho bila kuwa na ushahidi. Mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.
 
Mtoa mada huna hoja kwa sababu kuna wasanii wengi wanakufa kila siku. Kifo kinachotambulika na kuvuma ni cha mtu maarufu, sasa unadhani kama akifa msanii wa kwenye klabu yenu ya pombe huko Kibondo au Rorya nani atamtangaza? Akitangazwa atamgusa nani? Swali moja, unadhani ikianguka ndege, wakafa watu 400, na rais mmoja, leadline zitawataja watu 400 kwanza au rais yule mmoja? Ukijibu hili swali utajua ni kwanini wasanii maarufu vifo vyao vinavuma!
 
Ni vizuri umetaja Mungu. Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, mbele za Mungu binadamu wote ni sawa na wana haki ya kuishi. Labda kitu cha msingi cha kujifunza kwetu sisi (au muumini yoyote wa dini ya Kiislam au Kikiristo) ambao bado tuko hai ni kutenda mema kila wakati kwani hatujui ni wakati gani maisha yetu yatakoma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom