Vifo hivi ni matokeo ya Zanzibar kuikataa Sumatra visiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo hivi ni matokeo ya Zanzibar kuikataa Sumatra visiwani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Jul 19, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Tumeshuhudia ajali mbili kubwa za vyombo vya majini vinavyosadikiwa kusajiriwa Zanzibar. Kwanza ilikuwa Spice Island, na sasa ni hii Seagul, ambayo inasemekana ilisajiriwa Zanzibar baada ya Sumatra Tanzania bara kuikatalia usajiri. Na pia tumeona tatizo la meli za Iran zilizosajiriwa Zanzibar.

  Ni wazi kwamba uwajibikaji ulioko Zanzibar katika masuala ya usajiri ni tofauti sana na bara, na ndio maana waliona kwamba Sumatra visiwani ni kikwazo kwao na wakakataa uwepo wa Sumatra Zanzibar.

  Mie nashauri kitu kimoja; hatuwezi kuwa nchi moja yenye viwango viwili tofauti. Kama Zanzibar hawaitaki Sumatra visiwani, basi meli yeyote ya abiria iliyosajiriwa Zanzibar lazima ipate usajiri wa Sumatra Tanzania bara ili kuruhusiwa kutia nanga katika bandari za bara.

  Mwakyembe, nawakilisha.
   
 2. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Huo wako ni ujinga na upeo mdogo wa kufikiri hivi hizo ajali za mabac za kila cku zinazotokea huko danganyika sumatra hawako kwanza nyinyi ni mafisadi mnataka kula na huku hiyo ni chuki binafsi dhidi ya z'bar
   
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Ukweli mchungu eeeeh!
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Ukweli mchungu sana Mkuu! Nina hamu sana kusikia watajitetea vipi na hili ikiwa ni kweli Sumatra waliitolea nje kuisajiri hii meli kwa sababu za kiusalama. Toka lini ukamweka yakhe akawa msajiri wa meli na akaangalia mambo yote muhimu yanayohusu usalama wa maji. Sana sana atasema "bwana eeh, kama laelea liache liende atii".
   
 5. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  sawa hiyo meli imesajiliwa Zanzíbar , meli haina ofisi Dar na SUMATRA wameliruhusu ,je hawana uwezo wa kuzuia meli isifanye safari wakati haijakamilisha vigezo ? Meli imetoka Dar kwenda Zenji ,kwa hiyo wakala wa SUMATRA / bandari Dar lazima akuwepo bandarini kuhakikisha usalama wa abiria. Ile Spice islander ulikuwa uzembe wa bandari ya Zenji ...huu je ? Tuache jazba na kutizama ukweli ulivyo....nchi hii ina mawaziri wawili wa usafiri lakini hii ndo moja ya wizara mbovu nchini.....si Zenji wala bara.....
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ukweli mtupu wote ni wale wale hakuna cha sumatra wala nini!
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Viongozi/wanasiasa wa Z'bar wanadeka. Wanadeka kwa manufaa yao binafsi. Kila wanapoambiwa kufuata sheria na wakati huo wakitaka kufanikisha mambo yao binafsi watasingizia kunyanyaswa na bara.

  Baada ya kuikataa SUMATRA hadi leo wameshasajili meli zaidi ya 100. Upande wa bara hazifikii hata 50! Upande wa bara SUMATRA wakisema lolote, Z'bar huingiza siasa (kumbuka mambo ya TRA). Tunaonewa, muungano una kasoro, n.k. hayo ndo mambo yao. Kila wakati wao wanadhani wanaonewa. Soma michango hii ya hasira hapa JF lakini ukweli uko pale pale, wanadeka na kudekezwa hata kwa mambo ya hatari yanayohitaji utaalamu kuondoa balaa kama hili.

  Sasa kuna meli nyingi, zingine ni kwa ajili ya kusafirisha mchele na mkaa kwenda nchi za kiarabu kinyume cha taratibu. Wakiguswa tu, muungano mbaya. Takwimu zinaonyesha wanachukuwa mchele na mkaa mwingi toka bara zaidi ya mahitaji yao, ziada ni kwenda arabuni.

  Hayo mambo ya kutaka kuwa pekee ndo mavuno yake haya. Ni aibu watu kupoteza maisha na kama unatoka Z'bar tunastahili kuwataka viongozi wetu watueleze kwa nini tunajitenga ili kufanikisha uzembe, badala ya kuwa na jazba za kulinda utaifa wa Z'bar bila sababu.
   
 8. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mchungzi umenena haswaaa! Zanzibar wana tabia ya kimwinyi sana ya kutaka kurahisisha mambo hata kama ina maana sheria zikiukwe. Mie nakuambia ukiwa na meli lako la ajabu ajabu peleka tu Zanzibar bora liende litasajiriwa. Wakibanwa na sheria wanasingizia muungano una mapungufu. Mara zote nimesema Nyerere alifikiri sana aliposema juu ya Zanzibar kuwa kama mtoto mchanga anyekunyea halafu analia yeye!

  Katika mambo ya kodi kwa mfano, wao walitaka wawe free port sijui, bidhaa kuingia kwao zisitozwe kodi ili wa-export na kuingiza fedha. Bara wakasema bwana hii italeta matatizo kwenye mambo ya kodi, wakawa ving'ang'anizi, ooh, sisi hatuna vyanzo vya fedha nk. Mwishowe bara wakasema sawa, kama mnaona itawasaidia uchumi wenu endeleeni na hiyo free port, ila mpeleke hizo bidhaa Kenya na kwingineko, bidhaa yeyote toka Zanzibar ikija bara tunailima kodi zote. Wakaanza kulia ooh, mnatuonea! Can you imagine kukaa mezani kujadili mambo na watu wenye kufikiri kwa namna hii.
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  zanzibar ni zigo, tena zigo la misumari...   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  na ikumbukwe kuwa huko ilikotoka ilikataliwa ndo wa zenji wakaichukua.
   
Loading...