Vifaranga Vya Kuchi...

Hujui thamani yake ndio maana unaongea pumba..ndio maana kuna mbuzi na kuku. Kwanini unanunua Bata Bukini laki 3 paka laki 4 kwa pear? Na Bata maji ni 40,000 kwa pear?
Kaka hizo bei unazosema kwa usawa huu utakesha, hakuna mtu atanunua kwa bei hizo
 
Habari za Jumapili...

Vifaranga Vya Kuchi Vipo sokoni....Vina miezi 4 paka sasa
View attachment 594691
Nadhani jina - kuchi linachanganya pia. Nadhani hawa kuchi ni wa kigeni (exotic), kama ni hivyo ilipaswa wataalamu wetu kutohoa jina linaloonyesha ni aina ya kuku ambayo pamoja na kuwa na baadhi ya sifa zinazofanana na kuchi wetu (indigenous kuchi) lakini zina sifa za ziada, otherwise kuchi tunaowafahamu kijijini kwetu bei yao haiwezi kufika hata nusu ya bei unayotutangazia. Una nina nzuri ya kutangaza biashara, kinachokosekana kwenye tangazo lako ni kumfahamisha customer wako sifa za bidhaa yako. Otherwise wengine tutadhani labda kwa vile uko Arusha huenda watalii hununua kwa bei hiyo kuchi tunaowafahamu sasa unataka hata kina-sisi tununue kwa bei hiyo. Waelimishe watu tafadhali.
 
Mimi nilinunua 50,000 wakiwa miezi 2
Uliuza kwa Shilingi ngapi? Au umewapeleka ulingoni walete mapesa mengi??

Dunia sijui inaenda wapi yaani unafuga kuku ili wakapigane!!!

Huku kwetu ambako hamna ulingo wa kuku sijui nitamuuzia nani bei hiyo.
 
Hao kuku ni mbegu ya singida na kifaranga km huyo wa miezi minne bei yake ni sh.5000 hadi 4000 na akiwa kuku mkubwa kwa jogoo ni 18000
 
bf62abc77830d5aaa637c5bdb84f1ecb.jpg

Huyu wa ukweli sana!
 
Back
Top Bottom