Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Arusha.
Vifaranga vya kuku 6,400 vimekamatwa wilayani Longido mkoani Arusha vikiingizwa nchini kutoka Kenya. Vifaranga vilivyokamatwa jana Jumapili Oktoba 29, 2017 vyenye thamani ya Sh12.5 milioni ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Oktoba 30,2017 katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo kanda ya kaskazini, Obedi Nyasembwa amesema Serikali tangu mwaka 2007 ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi.
Amesema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwemo wa mafua ya ndege.
"Kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa," amesema.
Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mpaka wa Namanga, Edwin Iwato amesema kwa mujibu wa sheria vifaranga hivyo havikupaswa kuingizwa nchini, hivyo licha ya kuviteketeza, gari lililotumika kuvisafirisha litatozwa faini.
Mfanyabiashara Matia akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi, amekiri kuingiza nchini vifaranga hivyo akisema hakuwa akijua kama uingizaji umepigwa marufuku.
"Naomba wasivichome moto vifaranga, ni bora waniruhusu nivirudishe Kenya kwa kuwa ninadaiwa Sh12.5 milioni nilikovinunua," amesema.
Hata hivyo, Ofisa Mfawidhi Mkaguzi wa Mifugo, Medard Tarimo amesema kwa muda mrefu yamekuwepo malalamiko ya kuingizwa nchini vifaranga na mayai lakini wamekuwa wakishindwa kuwakamata wahusika.
"Wamekuwa wakipita njia za panya usiku na kuingiza nchini jambo ambalo ni la hatari kwa afya za binaadamu kwa kuwa nchi jirani tu ya Uganda kuna ugonjwa wa mafua ya ndege," amesema.
Amesema vifaranga hivyo vitateketezwa ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine
mwananchi
UPDATE:
Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Arusha, imeteketeza kwa moto vifaranga vya kuku wa kisasa 6,000.
Habari zaidi soma=>Arusha: Shehena ya vifaranga yateketezwa kwa moto baada ya kukamatwa vikiingizwa nchini kwa njia za panya