Vifaranga vilivyoingizwa nchini kinyemela kuteketezwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Arusha.
Vifaranga vya kuku 6,400 vimekamatwa wilayani Longido mkoani Arusha vikiingizwa nchini kutoka Kenya. Vifaranga vilivyokamatwa jana Jumapili Oktoba 29, 2017 vyenye thamani ya Sh12.5 milioni ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Oktoba 30,2017 katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo kanda ya kaskazini, Obedi Nyasembwa amesema Serikali tangu mwaka 2007 ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi.

Amesema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwemo wa mafua ya ndege.

"Kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa," amesema.

Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mpaka wa Namanga, Edwin Iwato amesema kwa mujibu wa sheria vifaranga hivyo havikupaswa kuingizwa nchini, hivyo licha ya kuviteketeza, gari lililotumika kuvisafirisha litatozwa faini.

Mfanyabiashara Matia akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi, amekiri kuingiza nchini vifaranga hivyo akisema hakuwa akijua kama uingizaji umepigwa marufuku.

"Naomba wasivichome moto vifaranga, ni bora waniruhusu nivirudishe Kenya kwa kuwa ninadaiwa Sh12.5 milioni nilikovinunua," amesema.

Hata hivyo, Ofisa Mfawidhi Mkaguzi wa Mifugo, Medard Tarimo amesema kwa muda mrefu yamekuwepo malalamiko ya kuingizwa nchini vifaranga na mayai lakini wamekuwa wakishindwa kuwakamata wahusika.

"Wamekuwa wakipita njia za panya usiku na kuingiza nchini jambo ambalo ni la hatari kwa afya za binaadamu kwa kuwa nchi jirani tu ya Uganda kuna ugonjwa wa mafua ya ndege," amesema.
Amesema vifaranga hivyo vitateketezwa ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine

vifaranga+pic.jpg



mwananchi

UPDATE:

Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Arusha, imeteketeza kwa moto vifaranga vya kuku wa kisasa 6,000.

Habari zaidi soma=>Arusha: Shehena ya vifaranga yateketezwa kwa moto baada ya kukamatwa vikiingizwa nchini kwa njia za panya
 
Hii nchi imevamiwa na watu wenye roho mbaya. Utaua vipi viumbe hao...eti liwe fundisho!

Nijuavyo mimi, Uganda na Kenya wamepiga hatua kwenye tafiti za mbegu bora za kuku. Uganda wana breed ya Kuroiler na Kenya wana Kari, sisi tuna Porojo. Hii KARI ni Kenya Agricultural Research Institute, wamebreed kuku wazuri na wanafanya vizuri kwa utagaji, watu wanapambana na hali zao leo badala ya kuwasaidia, tunaweka mambo meeeeengi ya kuwakwamisha huku tunahubiri viwanda.

Mi ningeelewa kama marufuku ingehusu mayai na kuku wakubwa wa kula. Vifaranga ni mbegu, wasaidieni wakulima chanjo na tafiti sio kuteketeza. Roho mbaya tu!
 
Nimemsikia huyo msemaji aliyesema kuwa vifaranga na mayai yamekuwa yakiingizwa nchini kwa njia za panya. Sasa huyu mfanyabiashara, kapitia mlangoni wazi wazi badala ya kumwambia rudisha ulikotoa huu mzigo na usijaribu kuupitisha tena, ameambiwa, ujinga wako umekuponza sasa tunaviteketeza.
Ni maajab sana. Angelitaka kuingia bila kukamatwa angeliweza ila aliposema napitia njia halali imekula kwake. Poleni watz. Nadhani kabla hujafanya biashara kubwa kubwa, anza kidogo kikitokomea usizimie ghafla.
Imagine; Anadaiwa 12.5m bado fine, bado asifike nyumbani hadi alipe fine. Je, wanaomdai watamwacha salama?? Ni mawazo tu, si amri. Tumrudishe navyo asivuke mpaka wetu.
 
Mkuu Habari ya watoto imekujaje tena huwezi linganisha binadamu na ndege ni vitu viwili tofauti ungetoa mfano unaolingana ningekuelewa zaidi
Comment yako imejaa maudhi kiasi ungekuwa hapa karibu ningekubaka kabisa. Watu wanaongea kitu serious we unaleta mambo ya hereni poda na hina. We ni wa kike au wa kiume? Ni wapi huko mnakokula vifaranga?

Damu hata iwe ya njiwa inaleta laana. Huwezi wewe uue maelfu ya kuku pasipo sababu za msingi eti kumkomesha mfanyabiashara awe fundisho.
 
Mkuu naona unatetea uhalifu. Vifaranga vyote hivyo kuvichoma kisa kumkomoa mtu haikubaliki
Hapana mkuu sitetei, wao wanachoma kuhofia magonjwa ambukizi kama mafua ya ndege. Ila kama kutakuwa na njia nyingine mbadala wa hiyo wanaweza pia kufunya.
 
Au wavirudishe mpakani na kuviswaga viende upande wa Kenya vilipotoka badala ya kuvichoma moto viumbe visivyo na hatia:).

Vingekuwa ni kuku wakubwa na wakauliwa ili watumike kama kitoweo hapo sawa lakini kwa vifaranga tena ambavyo hata havijathibitishwa kwamba hapo vilipo tayari vina magonjwa kuviondolea uhai kwa staili hiyo naona haijakaa sawa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom