Vifaranga vilivyoingizwa nchini kinyemela kuteketezwa

Sera ya nchi ya viwanda haitatekelezwa ikiwa watu wenye nia wanaangamizwavhivi

Arusha. Vifaranga vya kuku 6,400 vinatarajiwa kuchomwa moto baada ya kunaswa vikiingizwa nchini kupitia Longido mkoani Arusha.
Vifaranga hivyo vilikamatwa juzi vikitokea nchini Kenya.
Taarifa zinasema thamani ya vifaranga hivyo ni Sh12.5 milioni na ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi.
Akizungumza na Mwananchi katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasembwa alisema tangu mwaka 2007 Serikali ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi.
Alisema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwamo wa mafua ya ndege.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa,” alisema.
Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka wa Namanga, Edwin Iwato alisema kwa mujibu wa sheria vifaranga hivyo havikupaswa kuingizwa nchini, hivyo licha ya kuviteketeza, gari lililotumika kuvisafirisha litatozwa faini.
Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mfanyabiashara Matia alikiri kuingiza nchini vifaranga hivyo akisema hakuwa akijua kama uingizaji umepigwa marufuku.
“Naomba wasivichome moto vifaranga, ni bora waniruhusu nivirudishe Kenya kwa kuwa ninadaiwa Sh12.5 milioni nilikovinunua,” alisema.
Hata hivyo, ofisa mfawidhi mkaguzi wa Mifugo, Medard Tarimo alisema kwa muda mrefu yamekuwapo malalamiko ya kuingizwa nchini vifaranga na mayai lakini wamekuwa wakishindwa kuwakamata wahusika.
“Wamekuwa wakipita njia za panya usiku na kuingiza nchini jambo ambalo ni la hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa nchi jirani tu ya Uganda kuna ugonjwa wa mafua ya ndege,” alisema.
 
Umesahau kuwa ccm na kiongozi wake uwa wanapanga watu mf mabango na wakina mama?
Hilo ni dili la magu mama alipangwa kuja kusema hayo.

Swissme
 
Aiseee masikini huyo mama!
Ila kenya kwenye masuala ya ufugaji wako mbele sana Ndio maana watu wanachukua vifanga kutoka Kenya!
 
Hakuna kitu kibaya kwenye nchi kama kuingiza mimea na wanyama bila utaratibu.

Nchi za wenzetu, hata apple huingii nalo airport. Kuanzia spices mpaka kwenye wanyama. Hata kipande cha jani au ua kama liliingia kwenye begi bila wewe kujua, mbwa akanusa, utasachiwa begi zima.

Unless kama ulipata kibali na sample ya hao wanyama au mimea ilishachukuliwa na kuonekana hamna tatizo kwa kibali maalum.

Ukitaka kuona hasara ya kuingiza mimea na ndege hovyo, nenda ziwa Victoria uone magugu maji yalivyoleta shida, tembea dar na zenji uone kunguru wanavyosumbua mpaka ukaja mradi wa kuwaangamiza.

Anayetaka kununua vifaranga, anunue hapa hapa nchini. Kutibu magonjwa ya wanyama yanayotoka nchi nyingine ni gharama na hasara kubwa.
Kabisa, na kwa michango ya wengi humu inaonekana hawana uelewa wa hili. Ukitaka kufanya shughuli yeyote fuatilia taratibu zake zikoje.
 
Haki za wanyama/ndege zinasemaje kuhusu huo uchomaji wa hao vifaranga? It is inhuman bora wawarudishe walikowatoa.
 
Kama ni kinyume cha sheria sawa tu.
Hakuna namna tena.

Kutojua sheria hakufanyi usitiwe hatiani.
 
haki za wanyama zinasemaje??

maana kumuua kwa kumchoma moto mateso ni makali sana.. tena kifaranga.. bora awe kuku mzima
 
Haki za wanyama/ndege zinasemaje kuhusu huo uchomaji wa hao vifaranga? It is inhuman bora wawarudishe walikowatoa.

tax compliant ,

Ukivirudisha, utasikia mamalaka za Kenya nazo zitakataa kuwa tayari vimefika Tanzania hata wanaweza wakasema vifaranga wamebadilishwa.

Kwa hiyo, hicho hakiwezekani tena.

Kuhusu haki za wanyama, kwenye ugonjwa hicho kifungu kinatenguliwa kwa kulinda haki ya binadamu ya kuishi kwa mujibu wa Katiba, mujibu wa Wizara inayohusika na Mifungo na hata WHO.
Kwa hiyo vitachomwa tu moto.
 
Wazee wa EAC ni nani alikula pesa zao....???hao pia wanahitaji msaada mkubwa wa Mh.Rais
 
Kwa siku 2 hizi ningekua Mimi hata Mkuu wa Mkoa, ningeamrisha hao vifaranga wapimwe, kama hawatapatikana na Magonjwa mabaya kama mafua ya Ndege, ningetoa Amri Mama mwenye Kuku alipe Kodi stahiki kwa TRA then arudishiwe Kuku wake!
 
haki za wanyama zinasemaje??

maana kumuua kwa kumchoma moto mateso ni makali sana.. tena kifaranga.. bora awe kuku mzima

FRESHMAN ,

Ha ha ha ha ha , imebidi nicheke kwanza.

Mkuu, Haki za wanyama na za Binadamu za Binadamu zipo juu hasa panapotokea jambo la kuhatarisha uhai wa Binadamu hizo za wanyama tunaziweka kapuni kwanza.

Hicho kinafahamika kwa mfano, kwenye Katiba , Wizara inayohusika na mifugo , na hata WHO wanaelewa hilo zaidi hadi UN.

Mfano, Simba au mnyama yeyote akihatarisha maisha ya watu mtaani/ kijijini basi, huyo mnyama anauwawa ili kuokoa uhai wa wanadamu.

Hivyo , Uhai wa mtu mmoja tu ni bora mara 1+ Bilion kuliko vifaranga hata 10+Billionii.
 
Mkoa wa upinzani wakiwa na shida ndio wanaomba msaada wakikatazwa vitu wanapinga tu!Mrisho Gambo angekusaidia lakini nyie si mna kiburi?Vifaranga vichomwe moto kama anaona ananyanyaswa aende kwa Lema.baada ya hapo gari lipigwe fain,na huyo mama ashitakiwe.
 
tax compliant ,

Ukivirudisha, utasikia mamalaka za Kenya nazo zitakataa kuwa tayari vimefika Tanzania hata wanaweza wakasema vifaranga wamebadilishwa.

Kwa hiyo, hicho hakiwezekani tena.

Kuhusu haki za wanyama, kwenye ugonjwa hicho kifungu kinatenguliwa kwa kulinda haki ya binadamu ya kuishi kwa mujibu wa Katiba, mujibu wa Wizara inayohusika na Mifungo na hata WHO.
Kwa hiyo vitachomwa tu moto.
Asante kwa kunielimisha mkuu ingawa inasikitisha.
 
point yako haitumiwi kwa faru fausta.. anajaliwa sana kuliko binadamu maelfu... ni bora binadamu wafe ila faru fausta abaki

FRESHMAN ,

Ha ha ha ha ha , imebidi nicheke kwanza.

Mkuu, Haki za wanyama na za Binadamu za Binadamu zipo juu hasa panapotokea jambo la kuhatarisha uhai wa Binadamu hizo za wanyama tunaziweka kapuni kwanza.

Hicho kinafahamika kwa mfano, kwenye Katiba , Wizara inayohusika na mifugo , na hata WHO wanaelewa hilo zaidi hadi UN.

Mfano, Simba au mnyama yeyote akihatarisha maisha ya watu mtaani/ kijijini basi, huyo mnyama anauwawa ili kuokoa uhai wa wanadamu.

Hivyo , Uhai wa mtu mmoja tu ni bora mara 1+ Bilion kuliko vifaranga hata 10+Billionii.
 
point yako haitumiwi kwa faru fausta.. anajaliwa sana kuliko binadamu maelfu... ni bora binadamu wafe ila faru fausta abaki

FRESHMAN ,

Huyo faru hajamdhuru mtu huko mbugani, ila hii issue ya vifaranga inajulikana tangia 2003 hadi sasa.

Pia, faru hujasikia kuwa ana magonjwa ya kuambukiza wanadamu.

Kwa hiyo, mfano wako hauna uhalisia na mantiki.
Japo, nami kama mtafutaji naelewa hali uliyonayo na hata huyo mwanamke ambaye vifaranga wake wamekamatwa.

Lakini, ukweli Lazima uwe ukweli kuwa serikali ilikataza uagizaji wa wanyama kama kuku , vifaranga vyake na mayai kutoka nje ya nchi kwa ajili ya afya za binadamu.
 
Back
Top Bottom